data:post.body HIZI NDIO NJIA KUU NNE ZA KUONDOA MICHIZIRI YA KWENYE NGOZI... ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO NJIA KUU NNE ZA KUONDOA MICHIZIRI YA KWENYE NGOZI...

                                                                 
                                           
michirizi ya ngozi ni nini?
hizi ni alama ambazo huonekana kwenye ngozi baada ya kuchanika kwa moja ya ngozi ya ndani kitaalamukama dermis. michirizi hii hutokea mara nyingi baaada ya mbadiliko ya mwili ya ghafla kama kunenepa, kunyenyua vyuma chuma, kubeba mimba na kadhalika. alama zake hazina madhara kiafya lakini hazipendwi na watu ambao wanapenda mambo ya urembo hasa wasichana hivyo leo tutaenda kuzungumzia kwa kifupi matibabu ya hali hiyo kama ifuatavyo.

tumia mmea wa aloe vera; mmea huu unapatikana maeneo mengi sana nchini na umekua ukitumiwa na jamii mbalimbali tangu zamani kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, ngozi,tumbo na kadhalika na umethibitika kusaidia watu wengi waliotumia mmea huu.

jinsi ya kutumia..
kata ganda la mmea wa alo evera na chukua maji yake ya ndani kisha paka sehemu iliyoathirika na uache kwa dakika 15 kisha osha na maji lakini pia kama uko sehemu ambayo mmea huu haupatikani au hutaki usumbufu huu basi tumia losheni yenye aloevera ili upake kama mafuta. losheni nyingi zinakua na asilimia kidogo za aloevera hivyo napendekeza lotion za kampuni za FOREVER LIVING kwani losheni zao hua na aloevera kwa zaidi ya asilimia themanini, ikiongoza kama kampuni inayotoa bidhaa bora zaidi za aloe vera duniani, huku zikichanganywa na vitamin nzuri kwa ngozi kama vitamin A, vitamin E, na vitamin C, hivyo ukipata lotion hii unakua unapaka sehemu iliyoathirika kila siku mpaka uone mabadiliko au unaweza kupaka mwili mzima kama mafuta yako ya kawaida tu.

Hakikisha unatibu ngozi yako kutokea ndani: kunywa maji mengi sana ili kuusafisha mwili angalau lita tatu kwa siku hii itafanya mwili kuondoa sumu nyingi sana mwilini ambazo husababisha kua na matatizo ya ngozi kama chunusi,vipele na kadhalika lakini itaiboresha sana ngozi yako kua laini sana na kusaidia kuondoa michirizi. niliwahi kusema watu hua wanafikiri watu wanaoishi dar wana ngozi laini sana sababu ya joto lakini si kweli, ngozi zao ni laini kwasababu wanakunywa maji mengi sana.                                         


jitahidi kula vyakula vya asili; vyakula vingi vinavyotengenezwa kiwandani kama soda, biskuti,chocolate na kadhalika sio vizuri kwa afya ya ngozi ya binadamu, lakini sio kiwandani tu lakini vyakula vya haraka na kukaangwa yaani fast food kama maandazi, chapati, sambusa, chipsi, vitumbua, baga, piza na vingine vingi sio vyakula vizuri na huharibu mifumo mingi ya binadamu ikiwemo ngozi. tumia vyakula asili kama wali, ugali, samaki,maharage,njegere,mihogo,viazi, matunda, mboga za majani na vingine vingi na vitakusaidia sana.
                                                               


shiriki mazoezi; mazoezi ni matibabu ya magonjwa yote duniani kwani huupa mwili afya njema na kutibu mifumo yote ya mwili kama ngozi, moyo, upumuaji, mfumo wa chakula na kadhalika. hii itakufanya upate matokeo mazuri haraka kuliko mtu anayepaka tu bila mazoezi japokua wote mwisho  wa siku watafanikiwa. unaweza kufanya mazoezi ya kutembea, kuruka kamba, kufanya kazi nzito na kadhalika.
                                                         
                                                                      STAY ALIVE

                                          DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 
                                        MAWASILIANO O653095635\0769846183


                                    
                                    


0 maoni:

Chapisha Maoni