data:post.body Desemba 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIO NJIA TISA ZA KUFANIKIWA KWENYE MAZOEZI YA KUJAZA MIILI KWA WANAUME..

                                                                     

wanaume wengi wa umri wa miaka 18 mpaka 40 hupendelea sana kufanya mazoezi ya kubeba vyuma au kupiga push ups ili kua na miili mikakamavu, nguvu, kupunguza uzito na kua na miili inayovutia wenyewe wanaita SEXY BODY. sasa katika harakati zakupata miili hiyo kuna makosa mengi hua wanayafanya na wengine hushindwa kupata miili hiyo na kukata tamaa kabisa. lakini kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia ukiamua kufanya mazoezi hao na kufanikiwa.
kua na malengo; mara nyingi watu wanaenda gym bila malengo yeyote, yaani hajui anaka aweje ndani ya muda gani hii huwafanya kupoteza uelekeo baada ya wiki moja tu ya kuanza mazoezi. jipangie kwamba nataka kua na kifua kipana au mikono iliyojaa au kukata tumbo ndani ya muda fulani na hakikisha muda ulioweka haya mambo yanawezekana.. kama unaenda gym ili ufanikiwe kwa muda wa wiki moja ujue unapoteza muda.
chagua kifaa na uzito sahihi;kutumia vifaa vya gharama sana au kwenda gym ya gharama kubwa sana haitakufanya upate mwili haraka ili uchaguzi mzuri wa mazoezi na vifaa. hakikisha uzito uliochagua basi unaweza kupiga mara 15 kwa raundi moja, kama unabebea chuma afu unapiga tano unashindwa basi hiyo sio size yako.
usifanye peke yako; ukianza gym hakikisha kuna mwalimu au mtu mzoefu ambaye atakua anakuelekeza uanzie wapi halafu uishie wapi..kuanza kufanya mazoezi mwenyewe utakua unayafanya vibaya. yaani kushika chuma vibaya, kufanya mazoezi vibaya na kukaa vibaya kwenye zoezi fulani. lakini pia mazoezi ya wengi huleta hamasa ya kuendelea kuliko kufanya peke yako nyumbani.
polepole ndio mwendo; mazoezi yote duniani yanafanyika kwa mwindo mkali kupata mafaniko lakini kwenye kubeba chuma ni tofauti kidogo kwani unatakiwa ufanye taratibu yaani kupandisha na kushusha sio haraka kama wanavyofanya wengi na kama umefanya utafiti utagundua ukifanya taratibu maumivu ndio yanakua makali zaidi na hiyo ni dalili nzuri.
pumzika: hakikisha unapata pumziko la angalau dakika tatu au nne pale unapohama kutoka kwenye zoezi moja kwenda lingine yaani kutoka kwenye zoezi la mkono kwenda kwenye kifua kwani utafiti unonyesha mapumziko yake ni muhimu sana kwa mafanikio.lakini mapumziko sio hayo tu ni vizuri kwenga gym angalau siku tano mfulululizo kwa wiki wanaoanza na kupumzika siku mbili kwa wiki.mapumziko yale yataleta faida kuliko kwenda kila siku.
kua na mpangilio mzuri wa mazoezi; ukienda gym afu ukatumia mashine zote kuna uwezeano mkubwa uko unapoteza muda.weka ratiba kwamba leo nafanya zoezi la mkono. fanya mazoezi yote ya kujaza mkono yanayopatikana pale afu mwishoni ndo unaweza kugusa kifua kidogo na tumbo kidogo. siku ya tumbo fanya mazoezi yote ya tumbo afu mwishoni ndio gusa kidogo na mengine. ukiyafanya yote kwa mpigo kwa kiwango kimoja, matokeo hautayaona.
chakula; umeshaona watu wanabeba chuma kila siku ila bado wana vitambi? au mtu ana bidii sana kwenye mazoezi lakini mafanikio hayaonekani? chakula ndio msingi wa kila kitu kwani mwili ule unaouona kwa baunsa ni chakula kitupu na ukimnyima hicho chakula kwa wiki moja tu utamshangaa atakavyoisha.vyakula vinavyojaza mwili yaani nyama na mifupa ni aina ya protini kama nyama, samaki,dagaa, karanga, korosho, maziwa na kadhalika lakini ukifanya mazoezi haya huku unakula sana ugali,wali,ndizi,mihogo,viazi na kadhalika utaambulia kitambi tu.sijasema usivile hivo ila kula kidogo.
                                                          

virutubisho; kuna virutubisho vinauzwa kitaalamu wanaita protein shake, mchnganyiko huo unakua na protein nyingi sana kuliko ile inayopatikana kwenye chakula cha kawaida na mara nyingi hua kwa mfumo wa unga, hivyo mtumiaji huchota unga ule na kuchanganya kwenye maziwa. matokeo yake hua ni mazuri sana sana.unaweza kununua virutubisho hivi mtandaoni kwa kubonyeza link hii https://amzn.to/346OURi
                                                                    
usikate tamaa; hii ni point ya mwisho na ya msingi sana, kiufupi ukikata tamaa kwenye kitu chochote ndoto zako zimekua zimeishia hapo,  mafanikio yeyote huletetwa na uvumilivu mkubwa wa muda mrefu ambao mwisho wake utakuletea majibu.
                                             

                                                                   STAY ALIVE

                                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                      MAWASILIANO;0653095635/0769846183




YAFAHAMU MADHARA MAKUU MATATU YA KUTUMIA PAFYUMU, DEODERANT NA SPRAY MWILINI.

                                                                  
                                                                 
mtu mmoja rafiki yangu sana, nilisoma naye sekondari miaka ya nyuma kidogo aliwahi kunipigia simu na kuniuliza madhara ya kutumia haya marashi ya kunukia kama perfum, deodorant, body spray na kadhalika. alinigusa sana kwani ni moja ya janga kubwa kwenye jamii ambalo halifahamiki na leo naenda kutumbua jipu hili mapema kabisa ili utumie ukijua..marashi haya yanaleta matatizo magonjwa yafuatayo kutokana na kemikali ya aluminium iliyoko ndani ya aina nyingi za marashi kama ifuatavyo...
kansa ya matiti: utafiti uiofanyika hivi karibuni umegundua kwamba kansa nyingi za matiti yaani kwa wanaume na kwa wananawake zinatokea upande wa juu wa titi kwa nje, karibu kabisa na pale unapopaka marashi yako.. utafiti huu uliongeza kwamba kemikali hizi ikiwemo aluminium huzuia harufu kwa kuziba matundu ya jasho na kufanya mwili ushindwe kutoa uchafu wake, lakini pia kemikali hizi mara nyingi huingia kwenye damu wakati mtu amenyoa na kuacha michubuko kwenye ngozi ya kwapa,  kemikali hizi zikiwa ndani ya damu huingiliana na DNA na HOMONI za mwili na kuzaa kansa.
ugonjwa wa alzeheimers; huu ni ugonjwa unaoshambulia ubongo hasa kipindi cha uzee, mgonjwa hupata hali ya kusahau kia kitu mpaka jina lake wakati mwingine. utafiti uliofanyika nchini marekani ulikuta watu hawa wakiwa na kiasi kikubwa sana cha kemikali ya aluminium kichwani ambazo kwa hali ya kawaida iligundulika wagonjwa hao walizitoa kwenye marashi yao ambayo wakipaka kwa maisha yao yote.
ugonjwa wa figo; ugunduzi huu ulifanyika miaka ya nyuma kidogo ambapo wagonjwa wengi wenye shida ya figo hua wana kiasi kikubwa sana cha phosphorus kwenye damu zao na matokeo yao walianza kupewa alumimium hydroxide kupunguza kiasi cha phosphorus mwilini, lakini baadae wakagundua aluminium ile ilikua haitoki mwilini vizuri hivyo ikaamuliwa na shirika la viwangovya  dawa na chakula marekani, kwamba marashi yote yenye aluminium yawekwe wazi ili watu hawa wasitumie.lakini je? unafikiri wewe ambaye kwa sasa ni mzima hupati madhara yeyote ya figo kwenye aluminium zilizoko kwenye marashi yako?
mwisho; sijaandika maka hii ili watu waanze kunuka. hapana, kuna njia za asili za kuzuia harufu ya kikwapa kwa kutumia vitu asili au kutumia marashi yaliyotengenezwa bila kemikali hizi..zipo kampuni zinatoa marashi yasiyokua na kemikali hizi japokua hapa kwetu ni adimu sana. kampuni nayoifahamu yenye bidhaa hizi ni kampuni ya FOREVER LIVING ambao bidhaa zao wanazitengeneza kiasili na kuweka mmea wa aloe vera. kampuni hii ina wasambazaji mikoa mbalimbali unaweza onana nao na kutumia marashi yao ili kua salama au ukatafuta vyanzo vingine unavyoviamini.
                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                0653095635/0769846183

HIZI NDIO NJIA KUU NNE ZA KUONDOA MICHIZIRI YA KWENYE NGOZI...

                                                                 
                                           
michirizi ya ngozi ni nini?
hizi ni alama ambazo huonekana kwenye ngozi baada ya kuchanika kwa moja ya ngozi ya ndani kitaalamukama dermis. michirizi hii hutokea mara nyingi baaada ya mbadiliko ya mwili ya ghafla kama kunenepa, kunyenyua vyuma chuma, kubeba mimba na kadhalika. alama zake hazina madhara kiafya lakini hazipendwi na watu ambao wanapenda mambo ya urembo hasa wasichana hivyo leo tutaenda kuzungumzia kwa kifupi matibabu ya hali hiyo kama ifuatavyo.

tumia mmea wa aloe vera; mmea huu unapatikana maeneo mengi sana nchini na umekua ukitumiwa na jamii mbalimbali tangu zamani kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, ngozi,tumbo na kadhalika na umethibitika kusaidia watu wengi waliotumia mmea huu.

jinsi ya kutumia..
kata ganda la mmea wa alo evera na chukua maji yake ya ndani kisha paka sehemu iliyoathirika na uache kwa dakika 15 kisha osha na maji lakini pia kama uko sehemu ambayo mmea huu haupatikani au hutaki usumbufu huu basi tumia losheni yenye aloevera ili upake kama mafuta. losheni nyingi zinakua na asilimia kidogo za aloevera hivyo napendekeza lotion za kampuni za FOREVER LIVING kwani losheni zao hua na aloevera kwa zaidi ya asilimia themanini, ikiongoza kama kampuni inayotoa bidhaa bora zaidi za aloe vera duniani, huku zikichanganywa na vitamin nzuri kwa ngozi kama vitamin A, vitamin E, na vitamin C, hivyo ukipata lotion hii unakua unapaka sehemu iliyoathirika kila siku mpaka uone mabadiliko au unaweza kupaka mwili mzima kama mafuta yako ya kawaida tu.

Hakikisha unatibu ngozi yako kutokea ndani: kunywa maji mengi sana ili kuusafisha mwili angalau lita tatu kwa siku hii itafanya mwili kuondoa sumu nyingi sana mwilini ambazo husababisha kua na matatizo ya ngozi kama chunusi,vipele na kadhalika lakini itaiboresha sana ngozi yako kua laini sana na kusaidia kuondoa michirizi. niliwahi kusema watu hua wanafikiri watu wanaoishi dar wana ngozi laini sana sababu ya joto lakini si kweli, ngozi zao ni laini kwasababu wanakunywa maji mengi sana.                                         


jitahidi kula vyakula vya asili; vyakula vingi vinavyotengenezwa kiwandani kama soda, biskuti,chocolate na kadhalika sio vizuri kwa afya ya ngozi ya binadamu, lakini sio kiwandani tu lakini vyakula vya haraka na kukaangwa yaani fast food kama maandazi, chapati, sambusa, chipsi, vitumbua, baga, piza na vingine vingi sio vyakula vizuri na huharibu mifumo mingi ya binadamu ikiwemo ngozi. tumia vyakula asili kama wali, ugali, samaki,maharage,njegere,mihogo,viazi, matunda, mboga za majani na vingine vingi na vitakusaidia sana.
                                                               


shiriki mazoezi; mazoezi ni matibabu ya magonjwa yote duniani kwani huupa mwili afya njema na kutibu mifumo yote ya mwili kama ngozi, moyo, upumuaji, mfumo wa chakula na kadhalika. hii itakufanya upate matokeo mazuri haraka kuliko mtu anayepaka tu bila mazoezi japokua wote mwisho  wa siku watafanikiwa. unaweza kufanya mazoezi ya kutembea, kuruka kamba, kufanya kazi nzito na kadhalika.
                                                         
                                                                      STAY ALIVE





                                          DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 
                                        MAWASILIANO O653095635\0769846183