data:post.body Novemba 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIVI NDIO UGONJWA WA KIPINDUPINDU UNAVYOUA HARAKA SANA.

                                                                           

ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoua ndani ya muda mfupi sana kama mtu asipopata matibabu haraka, tafiti za shirika la umoja wa mataifa duniani zinaonyesha kwamba kuna wagonjwa milioni moja na laki nne kila mwaka wa kipindupindu na kati ya hao wagonjwa laki moja na elfu arobaini na mbili hufa kila mwaka duniani kote.
zaidi ya asilimia themanini ya wagonjwa huweza kutibiwa kwa kupewa oral rehydration therap[0RS] ya kunywa tu.

ugonjwa huu ukoje?
huu ni ugonjwa wa kuharisha unaosababishwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama vibrio cholerae kwasababu ya kunywa maji au kula chakula chenye bakteria huyu. baada ya kula au kunywa chakula au maji yenye bacteria hao huchukua saa mbili mpaka siku tatu tu kuanza kwa dalili za ugonjwa huu.

dalili za ugonjwa huu ni zipi?
kuna hatua kuu tatu za dalili za ugonjwa huu.
hatua ya kwanza;
mgonjwa huanza kuharisha kinyesi cha kawaida lakini baadae kinyesi hubadilika na kuanza kuharisha vitu kama mchele hivi.
mgonjwa huanza kutapika sana matapishi ya kawaida lakini baadae hua kama mchele hivi lakini baadae tumbo na miguu huanza kuuma sana kutokana na madini anayokua ampoteza mwilini.
hatua ya pili;
mgonjwa huanguka na kupoteza nguvu kabisa kwasababu ya kupoteza maji mengi sana mwilini, mwili huwa wa baridi na ngozi hukauka sana, presha hushuka sana na mapigo ya moyo kukimbia sana. hatua hii mgonjwa huweza kupoteza maisha kwa kwa shock na moyo kusimama.
hatua ya tatu;
hichi ni kipindi ambacho mtu huweza kupona baada ya kupata matibabu, kuharisha na kutapika hupungua sana na mgonjwa  hupata nguvu.

matibabu; 
matibabu ya ugonjwa huu ni rahisi sana kwani mtu huweza kupona kwa kunywa maji ya ORS peke yake na kupona kabisa lakini wagonjwa waliozidiwa sana hupewa mai kwa kupitia mishipa ya damu yaani dripu lakini pia wagonjwa hupewa dawa za kuua bakteria huyo. lakini matibabu haya hufanyika hospitali tu na sio nyumbani..

jinsi ya kuzuia ugonjwa huu.
kwa kipindi cha mlipuko wa ugonjwa huu ni vizuri kunywa maji safi na salama ya kuchemshwa na kula chakula kilichoandaliwa vizuri, ilitokea kuna mgonjwa ndani ya familia ni vizuri apelekwe hospitali mapema ili asiweze kuambukiza watu wengine.
ni hatari sana kula mahotelini kipindi cha mlipuko hasa vyakula ambavyo havipikwi kama kachumbari na matunda na kama kuna ulazima basi kaviandae nyumbani kwa usafi wa hali ya juu.
                                                              
                                           STAY ALIVE

                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                     MAWASILIANO 0653095635/0769846183







HIZI NI NJIA TANO BORA ZA KUJUA KAMA MTOTO ULIYEMZAA HANA TATIZO LA MTINDIO WA UBONGO.

                                                                    

baadhi ya watoto kwenye jamii zetu huzaliwa na mtindio wa ubongo yaani utakuta wazazi wanagundua kama mtoto hana akili nzuri au hawezi kufanya vitu fulani kama wenzake akishakua mtu mzima kabisa. mfano kushindwa kuongea, kutokwa mate mdomoni muda wote, kushindwa kutembea na kadhalika...kuna mambo mengi yanachangia kuzaliwa kwa watoto wa aina hii ikiwemo kuzaa umri mkubwa kwa wanawake,pombe na sigara kipindi cha ujauzito, magonjwa ya akili ya kurithi, matatizo yanayotokea katika ukuaji tumboni na kadhalika. leo tutaangalia njia kuu tano za kugundua kama mtoto wako ana akili nzuri na hana shida ya mtindio wa ubongo baada ya kuzaliwa.yani jinsi ya kumgundua kwa njia za kitaalamu kama ifuatavyo.

kushika kitu; hii huwepo mtoto anapozaliwa mpaka kufikisha miezi sita au saba, mtoto kipindi hiki ukimpa kitu chochote mfano kalamu lazima atakamata kwa nguvu bila kuachia lakini mtoto mwenye tatizo ukimpa kitu hataweza kushika na atabaki anakushangaa tu.
                                                              

kujaribu kutembea; dalili hii huonekana utotoni wakati wa kuzaliwa lakini lakini hua haina nguvu sana mpaka mtoto afikishe miezi sita mpaka mwaka mmoja. kipindi hiki ukimshika mtoto kama unataka kumtembeza atapiga hatua mwenyewe, hii ni dalili njema.
                                                         


kunyonya; wakati wa kuzaliwa mtoto akipewa ziwa la mama ananyonya mwenyewe bila kufundishwa kabisa, ikitokea mtoto anashindwa kunyonya siku ya kuzaliwa basi inawezekana anaumwa au ana mtindio wa ubongo na anashindwa kugundua vitu hivyo.
                                                       


parachute; hii hutokea hasa kwa watoto wenye angalau miezi sita mpaka mwaka mmoja, ukimbeba moto huyu afu ukamgeuza kichwa chini miguu juu kama unataka kumuangusha atanyoosha mikono kama anataka kuzuia ule muanguko.hii inaonyesha kwamba mtoto ni mzima.
                                                             


rooting; hii hutokea mtoto anapozaliwa mpaka miezi sita yaani kipindi hiki mtoto ukimgusa na kitu chochote kwenye shavu atageuka kufuata kitu hicho na mdomo akidhani labda ni ziwa la mama ili anyonye.dalili hii ni dalili nzuri na huonyesha kwamba mtoto ni mzima.
                                                                   



mwisho;kuna vitu vingi sana vya kuangalia kujua kama mtoto hana mtindio wa ubongo wakati wa kuzaliwa na anavyoendelea kukua lakini hivi ni baadhi tu ambavyo ni rahisi kuvijaribu hata ukiwa nyumbani. nakutakia afya njema wewe na familia yako.

                                                        STAY ALIVE

                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO


                                MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                               

ZIFAHAMU SABABU KUMI MUHIMU ZINAZO SABABISHA MIMBA KUHARIBIKA...

                                                                     
utafiti unaonyesha kati ya mimba 100 zinazobebwa ni 80 tu ndio zinafika kuzaliwa, yaani asilimia
 ishirini ya mimba zinazobebwa huharibika hata kabla ya kufika mezi watatu. kuna sababu nyingi zinazoweza sababisha mimba kutoka lakini leo nteanda kongelea zile muhimu ili kila mtu kama iko ndani ya uwezo wake aweze kuzuia pale anpopata mimba.

matatizo ya vimelea vya urithi: kawaida mbegu za mwanaume huchangia pea 23 za vimelea vya urithi yaani chromosomes na yai la kike hichangia vimelea 23 pia kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa, lakini kwenye hali isiyo ya kawaida namba hiyo ikiongezeka au kushuka husababisha mimba kutoka ndani ya muda mfupi.

magonjwa; kuna magonjwa mengi endapo hayatatbiwa wa muda muafaka husababisha mimba kutoka muda wowote ule yaani inaweza kua mwanzoni au mwishoni.mfano. malaria, kisukari, pressure, kaswende, virusi vya ukimwi, U.T.I, toxplasmosis,rubella, na herpes simplex virus.

matatizo ya kizazi; kuna magonjwa mengi yanayoahiri kizazi moja kwa moja na huweza kuleta kutoa mimba kirahisi sana mfano wa magonjwa hayo ni uvimbe wa ndani ya kizazi,ulegevu wa mlango wa uzazi na kadhalika.

matumizi ya dawa; ukiwa mjamzito hutakiwi kutumia dawa yeyote bila kuandikiwa na daktari, kuna dawa nyingi sana zinaweza kutoa mimba mfano fragile, albendazole,misoprostol, dawa ya mseto ya malaria, doxycline, na nyingine nyingi.

utapiamlo;  mwanamke mwenye upingufu wa madini muhimu mwilini kama calcium, potassium na sodium lakini pia wanga, protini, vitamini na kadhalika. upungufu huu humfanya mwanamke ashindwe kubebeba mimba mpaka kujifungua na hata akijifungua huweza kuzaa mtoto mwenye mapungufu fulani ya kiakili.

matatizo ya homoni; mwanamke ana kiwango maalumu cha homoni za uzazi ambacho anatakiwa awe nacho ili mimba iweze kutungwa na kukua. kiwango hiki kikiwa juu sana au chini sana husababisha mimba kuharibika.

aina ya maisha ya mjamzito; matumizi ya pombe na sigara kipindi cha ujauzito ni hatari sana kwani huingilia mfumo wa homoni na uzazi na kusababisha mimba kuharibika.

umri mkubwa; kubebe mimba kwenye umri mkubwa huchangia sana mimba kuharibika kwani kipindi hiki viungo vya uzazi na mfumo wa homoni unakua umepungua nguvu sana hivyo mimba za ukubwani sana hasa zaidi ya miaka 35 hutoka kirahisi kuliko mimba za vijana wadogo.

mazingira ya kuishi; maeneo mengi karibu na viwanda au huduma za mionzi ya hopitali hua kuna mionzi hatari ambayo huweza kuingia kwa mama na kuharibu mtoto aliyeko tumboni lakini pia uwezo wa kuzaa huko mbele ya safari.

upungufu wa damu; kipindi cha ujauzito akina mama wengi hua na damu chini ya kiwango kutokana na mabadiliko ya kimaumbile, lakini upungufu huo ukizidi zaidi husababisha uchungu kuanza kabla muda na mimba kuharibika.

mwisho; kila mtu anahitaji mtoto katika kipindi fulani cha maisha yake hivyo ni vizuri kujilinda na vyanzo hivyo kabla na baada ya kupata ujauzito kwa kufuata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya na kukaa mbali na mazingira hatarishi ya kuharibu ujauzito. kwa maelezo zaidi bofya maneno hayo ya kijani kusoma

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                             STAY ALIVE

                DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0769846183\0653095635


ZIFAHAMU NJIA KUU NNE ZA KUPATA MTOTO WA KIKE.

                                                                         

dunia inakwenda kasi sana siku hizi, kiasi kwamba imefika hatua mtu akizaliwa mwanaume sio lazima kwamba atakufa mwanaume. teknolojia imefika mbali sana kiasi kwamba watu wana maamuzi juu ya maisha yao, miili yao, watoto wao na machague mengi tofauti tofauti. moja ya maswali ambayo nimekua nikiulizwa sana ni jinsi ya kuchagua jinsia ya mtoto. nimeshawahi kuongelea jinsi ya kupata mtoto wa kiume leo ntaongelea wa kike. hivyo leo naenda kuongelea njia za kitaalamu zinazoweza kukufanya kuongeza uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike.

fanya mapenzi siku moja, mbili au tatu kabla ya siku ya yai kushuka: yai la mwanamke hua linashuka mara moja tu kwa mwezi kulingana na mzunguko wa mtu husika, mfano mzunguko wa siku 28 siku ya 14, mzunguko wa siku 30 siku ya 16, mzunguko wa siku 32 siku ya 18 na kadhalika. kufanya mapenzi siku hizi kutafanya mbegu za mtoto wa kiume ambazo siku zote hufika mapema kwenye kizazi, zikute yai la mama na kurutubisha hivyo kutoa mtoto wa kiume hivyo jinsi ya kupata mtoto wa kike hapa ni kufanya mapenzi siku mbili au tatu kabla ya hii siku hii ile mbegu za mtoto wa kiume ambazo huishi muda mfupi zife zibaki zile za mtoto wa kike.kama mzunguko wako haueleweki ni bora kuangalia kama kuna tatizo ili uweze kuusoma vizuri.unaweza kutumia virutubisho vya kufanya kazi hii kwanza.

mwanamke ajizuie usifike keleleni; uke wa mwanamke una tindikali nyingi sana ambazo huua kirahisi mbegu za jinsia ya kiume na kuacha zile za jinsia ya kike hivyo mwanamke akifika kileleni tindikali hiyo hupotea sababu ya maji mengi kumwagika na hii huweza kushindwa kuua mbegu za mtoto wa kiume.

fanya mapenzi mara kwa mara; mwanaume anayefanya mapenzi mara kwa mara anapunguza ukomavu wa mbegu zake hivyo anakua kwenye nafasi nzuri ya kutengeneza mbegu ambazo zinatoa mtoto wa kike kuliko mtoto wa kiume ambaye anahitaji kupatikana kwa mbegu zilizokomaa sana.

tumia staili za ngono zenye muingilio mdogo; staili za zanye muingilio mdogo kama mwanamke kutangulia chini na mwanaume kuja juu hua na muingilio mdogo hivyo mbegu za mwanaume humwagwa juu juu sana na kusababisha zile za kiume kushindwa kusafiri na vizuri na kufa hivyo za mtoto wa kike kuwahi na kuleta mtoto wa kike.
kwa maelezo zaidi fungua hapa usome

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                               STAY ALIVE
                                           DR. KAEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                      0653095635/0769846183




FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA KUISHIWA NYWELE KICHWANI AU KIPARA[ALOPECIA]

                                                              

kuna vijana wengi ambao hawana hata miaka 40 lakini tayari wana vipara kwenye vichwa vyao na nywele hazioti tena. ni hali ambayo inakosesha raha kidogo na wengi wao huamua kunyoa nywele zote ili kipara ionekane ndio staili yake. wengine huvaa kufia, kuvaa wigi au kuficha na kifaa chochote cha urembo. tatizo hili husababishwa na vyanzo vikuu viinne.
mabadiliko ya homoni ndani ya mwili; binadamu ana homoni nyingi sana ndani ya mwili wake...kuna kiwango maalumu cha homoni ambacho kila binadamu anatakiwa awe nacho.kiwango cha homoni fulani kikizidi au kikipungua huleta shida katika mwili wa binadamu.
magonjwa fulani; kuna baadhi ya magonjwa ya ngozi kama fangasi, mabayo yakishambulia eneo la kichwa huweza kuleta kipara mara moja.
matumizi ya aina fulani ya dawa; dawa hasa zile zinazotumika kutibu kansa, yaani vidonge na mionzi hua na madhara ya kumaliza nywele za mwili mzima.
vipara vya urithi; kuna baadhi ya koo ambazo hupata vipara mapema sana katika ukuaji, hivyo ukiona ndugu zako wengi wana vipara katika umri mdogo basi achana nacho kwani hautafanikiwa kupona ila kama ni wewe peke yako ukoo mzima basi pambana mpaka upone.

vipimo vya kufanya ukienda hospitali;
vipimo vya damu; dokta atakupima damu kuangalia magonjwa ambayo yanaweza kusababisha nywele kuisha hasa upungufu wa homoni na magonjwa ya ngozi.
vipimo vingine; kuna vipimo vingine huweza kupimwa kuangalia kama nywele zenyewe ziko vizuri kiafya kwa kutumia darubini ya hospitali lakini bahati mbaya vingi havifanyiki hapa nchini kwetu.

matibabu;
siku zote matibabu hutegemea chanzo cha ugonjwa husika.. kama ni fangasi mgonjwa atapewa dawa husika, kama ni ugonjwa wa ngozi atapata dawa husika, kama ni sababu ya mionzi au dawa za kansa itabidi avumilie tu kwani hawezi kuacha matibabu ya kansa.

dawa za kutumia; kuna dawa kuu mbili ambazo hutumika kutibu tatizo hili yaani finasteride na minoxidil, bahati mbaya dawa hizi nchini kwetu hazipo kabisa.

upasuaji; kuna aina za upasuaji hufanyika kupandikiza nywele, ni ghrama sana na hazipatikani kwenye nchi maskini kama zetu.mcheza mpira maarufu duniani kwa jina la wayne rooney alifanyiwa upasuaji huu.

tiba mbadala;
kama chanzo hakionekani inaweza kua ni tatizo la homoni na lishe mbovu, mtu huyu hutibiwa kwa kupewa virutubisho vya kunywa na kupaka kwenye nywele ili kushtua homoni za ukuaji na kushtua mizizi ya nywele kitaalamu kama hair follicles.
virutubisho hivyo huweza kuleta maibu ndani ya miezi mitano mpaka mwaka mmoja kama picha inavyonyesha hapo chini.
                                                         


jinsi ya kuzuia hali hii;
  • kula chakula bora chenye virutubisho vyote.
  • usisuke nywele kwa kuzibana sana na misuko
  • chana nywele taratibu na usitumie nguvu sana.
kwa maelezo zaidi fungua hapa usome

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                                STAY ALIVE

                                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                    0653095635/0769846183



ZIFAHAMU FAIDA KUMI ZA MMEA WA ALOE VERA KWA BINADAMU...

     
                                                                    
mmea wa aloe vera ni mmoja ya mimea ambayo imejizoelea umaarufu miaka hii ya karibuni  baada ya kuonyesha kutibu na kuzuia aina mbalimbali za magonjwa, lakini pia kurefusha maisha na kupunguza makali ya magonjwa yasiyopona kama kisukari, presha, magonjwa ya moyo, pumu, kifafa, ukimwi na mengine mengi, lakini mmea huu ulikua ukitumika tangu miaka ya zamani sana na watu waliishi miaka mingi wakiwa na nguvu na akili kupitia mmea huu. kwa faida za mmea huu ni bora kumiliki hata bidhaa moja tu ambayo utakua unaitumia siku zote za maisha yako ili kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa hatarishi..kwa sasa kampuni ya forever living product ndio inaongoza kwa mauzo hayo duniani, ikiwa imetapakaa zaidi ya nchi 150.hapa tanzania ikiwa  imeuaza zaidi ya bilioni ishirini kwa mwaka jana tu  na kulipa kodi serikali zaidi ya bilioni tano za kitanzania, hii inaonyesha watanzania wameamka na wanatumia sana bidhaa hizi. lakini pia ni bidhaa ambazo kama daktari naweza kuzitetea kwani wagonjwa wangu wengi wamefaidika kwa matumizi yake. zifuatazo ni sababu 10 kwanini utumie bidhaa zitokazo na mmea huu..

umekubalika na wanasayansi  duniani; zaidi ya tafiti mia moja za kitaalamu zilizofanyika zimegundua kwamba mmea huu wa aloe vera ni moja chakula bora vya asili kwa mwili wa binadamu na hufanya mtu kuishi kwa afya tele akitumia kama moja ya vyakula vyake.kumbuka hizi sio dawa kama watu wanavyofikiri kwani hazina sumu na hata ukinywa zaidi hudhuriki na ni vema kutumia kama sehemu ya chakula cha maisha yako kwa matokeo mazuri na sio kama vidonge vya malaria.

ni kinga ya mwili: bidhaa za mmea huu hutoa kinga asilia kwa mwili wa binadamu, tafiti zinaonyesha kwamba wagonjwa wengi waathirika wa virusi vya ukimwi walifaidika sana baada ya kutumia bidhaa hizi na kuongeza kiasi cha CD4 count,  kwa wale ambao walikua na hali mbaya sana na kuwafanya waendelee kuishi maisha kama kawaida.

hupambana na dalili za uzee; muanzilishi wa moja ya kampuni zinazofanya  kazi ya kuuza bidhaa hizi kwa kiasi kukubwa ulimwenguni ana umri wa miaka 80. binafsi nilipomuona nilifikiri labda ana miaka 50 au 60. amekua akitumia bidhaa hizi maisha yake yote nadhani yeye tu ni moja ya ushahidi kwamba bidhaa za aloe vera zinafanya uwe kijana kwa muda mrefu.

ni kinga na tiba kwa magonjwa ya meno;magonjwa ya kuoza na meno kutoka ni moja ya magonjwa yanayosumbua watu wengi duniani, lakini dawa za meno za mmea huu zimethibitisha kupambana na tatizo hili kwa asilimia kubwa sana.mdogo wangu anayenifuata alianza kutumia dawa za meno za kampuni hii baada ya kuhangaika sana kwa madaktari wa meno na ndio ilikua mwisho wa yeye kung'oa meno mpaka leo.

zinasaidia sana kupunguza uzito; virutubisho vingi vya aloe vera husaidia kuondoa sumu nyingi mwilini na  kuongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta. hii humfanya mtumiaji ambaye anataka kupungua uzito kupungua kirahisi sana huku akifanya mazoezi rahisi kama ya kutembea tu.

hupa mwili nguvu, madini na vitamini; bidhaa za mmea huu zina madini na vitamini karibia zote muhimu kwa mwili wa binadamu, ambazo mtu akizikosa huweza kuugua magonjwa ya aina mbalimbali.mfano calcium, magnesium, sodium, iron, pottasium, chromium, magnesium, manganese, copper, zinc and vitamins A,B1,B2,B12,C,E folic acid na niacin.

husaidia mifumo yote ya mwili; mmea huu wa aloe vera husaidia mfumo wa damu, mfumo wa upumuaji, mfumo wa chakula, mfumo wa mkojo na kadhalika na kwa namna hii huufanya mwili kufanya kazi muda mrefu bila kuchoka lakini pia virutubisho vya kuongeza nguvu za kiume na kutibu tatizo la ugumba vya kampuni hii vimeleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya afya.

husaidia uponyaji; vitamin c nyingi iliyopo kwenye mmea huu husaidia kupona kwa vidonda, kuungua, michubuko, allergy na hali zingine nyingin ambazo hupata mwili wa binadamu.lakini pia matibabu ya shida za ngozi kama chunusi, harara, upele na kadhalika..

ubora wa hali ya juu; watengenezaji wa bidhaa hizi kupitia kampunia ya forever living wametengeneza bidhaa za mmea huu  kwa ubora wa hali ya juu na kufanya uaminike dunia nzima na nchi zote.

fursa za kibiashara; kampuni hii inayoongoza kwa mauzo, inatumia mfumo wa mtandao ambapo watumiaji huweza kuanza kuwauzia watumiaji wengine na kupata faida kuu mbili yaani faida ya kuuza virutubisho hivyo na faida ya kuingiza watu wapya kwenye biashara.. ambapo, walioingizwa kwenye biashara humfaidisha kwa asilimia kadhaa mtu aliyewaingiza na kwa maana hiyo miaka yote yule mtu wa juu atapata faida, hivyo watu wengi zaidi chini yako uliowaingiza ni faida zaidi kwako. hapa tanzania kuna watu ni matajiri sana na hawahitaji kufanya kazi tena sababu ya biashara hii.hii ni moja ya biashara za kisasa sana ambazo matajiri wakubwa sana duniani kama bill gait, wanashauri watu wazifanye kwani ni chanzo cha uhuru wa kifedha yaani ni biashara pekee ambayo ipo siku utaacha kufanya lakini unapata fedha na imewafaidisha watu wengi sana duniani ambao walikua masikini sana.
angalizo;kama umeamua kutumia bidhaa hizi kama mteja ni tumia bila wasiwasi wowote ila kama umeamua kuzitumiana  kama mtumiaji na  mjasiriamali, usisikilize watu walioshindwa  watakukatisha tamaa kabisa, ongea na waliofanikiwa. ni moja ya biashara rahisi na huanzwa na mtaji mdogo...zaidi ntakuashauri usome kitabu cha BUSINESS OF 21st CENTURY kilichoa ndikwa na tajiri wa kimarekani kwa jina la robert kiyosaki.kwa maelezo zaidi bonyeza maneno ya kijani hapo chini kusoma.
                                 tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                                       
                                                     STAY ALIVE

                 DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0653095635\0769846183
                                                              
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]














UFAHAMU UGONJWA WA SIKOSELI NA MATIBABU YAKE.[SICKLE CELL ANAEMIA]

                                                                    

sickle cell ni nini?
huu ni ugonjwa wa kurithi wa kupungukiwa damu, ambapo mgonjwa hua hana damu ya kutosha kwa sababu ya seli zake za mwili sio imara kubeba hewa ya oksijeni kupeleka sehemu mbalimbali za mwili.
kwa hali ya kawaida seli za binadamu hua na umbo la kama yai na linalovutika kiasi kwamba huweza kupita kirahisi kwenye mishipa ya damu na seli hizo huishi siku 120 yaani miezi mitatu kisha hufa kupisha zingine lakini seli za mgonjwa wa sikoseli ni ngumu yaani zipo kama shepu ya  mwezi, huishi siku ishirini tu, na huweza kukwama kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita na hichi ndio chanzo kikuu cha matatizo.wagonjwa hawa husumbuliwa na mashambulio ya maumivu mara kwa mara sababu ya kukwama kwa seli hizo na kuzuia oksijeni kwenda sehemu za viungo vya mwili.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa huu husababishwa na kubadilika kwa mfumo wa mwili wa kutengeneza vimelea vya kutengeneza damu yaani haemoglobin. haemoglobin hii husababisha seli zinazotengenezwa kua na shepu ambayo sio ya kawaida.
ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa wazazi wote yaani baba na mama kitaalamu tunaita carriers.. mama na baba wanaweza kua hawana dalili yeyote  lakini wamebebea vimelea vya ugonjwa huo kwenye damu zao na kumzaa mtoto mgonjwa.
mgonjwa wa sickle cell akioa au akiolewa na mtu ambaye sio mgonjwa hawezi kuzaa wagonjwa ila atazaa watoto waliobeba vimelea hivyo. watoto wenye vimelea hivyo[carriers] wakioana wanaweza kuzaa mtoto mgonjwa.
mume na mke wagonjwa wakioana watazaa wagonjwa watupu hivyo ni vizuri kuliangalia hili kabla ya kuamua kuzaa.

dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mgonjwa wa sikoseli haonyeshi dalili yeyote mpaka afikishe miezi minne ya umri tangu kuzaliwa na huanza na dalili zifuatazo.
kuishiwa damu; kama nilivyosema mwanzoni seli za sikoseli huishi sio zaidi ya siku ishirini hivyo vifo hivi vya seli  husababisha sehemu kubwa ya mwili kukosa hewa ya kutosha ya oksijeni na kusababishwa mwili kua na uchovu sana.
 maumivu makali ya mwili; kukwama kwa seli hizi ambazo shepu zake zimekaa vibaya huzuia damu nyingi kupita kwenda sehemu mbalimbali za mwili. sehemu hizo zikikosa hewa ya oksijeni na kusababisha maumivu makali sana. maumivu hayo hua ya jointi, kifua na tumbo mara nyingi.
kuvimba vidole; hali hii pia husababisha na kukwama kwa seli hizo za mgonjwa na kusababisha ukosefu wa oksijeni ya kutosha  kwenye vidole vya mikonoo hivyo vidole huvimba na kuuma sana.
kuchelewa kukua kwa watoto; ukosefu wa hewa ya kutosha kwenye mfumo wa damu huukosesha mwili vitamini na madini ya kutosha na hali hii husababisha kuchelewa kukua na kuchelewa kubalehe au kuvunja ungo.
kutoona vizuri: mishipa midogo ya damu ya kwenye macho huweza kuziba na kufanya uwezo wa kuona kua mdogo sana.

vipimo vinavyofanyika  kugundua ugonjwa huu.
kipimo cha damu; kipimo kidogo cha damu huchukuliwa na kupimwa na majibu hutolewa baada ya masaa 24. vipimo hivi ni rahisi na hupatikana karibia kwenye maabara zote nchini.
vipimo kipindi cha ujauzito; nchi zilizoendelea mtoto aliyeko tumboni huweza kugundulika kama ni mgonjwa au sio mgonjwa na mama kuamua kama anataka kuendelea na ujauzito au vipi.

matibabu ya sikoseli;
kubadilisha kwa vitoa damu ndani ya mifupa[bone marrow transplant] huweza kutibu ugonjwa huu kabisa lakini upasuaji huu ni mgumu sana, sio rahisi kumpata mtu atakayekutolea ambaye atafanana na wewe kwenye vipimo vitakavyotakiwa, lakini pia kuna hatari kubwa ya kupata madhara makubwa hadi kifo na upasuaji huu hufanyika nchi zilizoendelea kwa gharama kubwa sana.
hivyo  matibabu ya siko seli mara nyingi hulenga kupunguza makali ya ugonjwa mara nyingi ili kumfanya mgonjwa aishi maisha ya kawaida..dawa ambazo hutolewa ni kama zifuatazo.
folic acid; hivi ni virutubisho ambavyo hutolewa kuongeza damu kwa mgonjwa huu na dose hua ni kidonge kimoja yaani 5mg kila siku kwa maisha yake yote. hii kidogo ni virutubisho vya zamani kidogo na hutolewa sana kwani serikali hujaribu kubana matumizi.
 
 B12 PLUS and FOLIC ACID; hivi virutubisho vingine ambavyo ni bora kuliko folic acid peke yake kwani huachanganywa ni vitamini zingine ambazo pia ni maalumu kwa ajili  kuongeza damu. hii hapa ina folic acid na vitamin b12, imechanganywa pia na virutubisho vya aloe vela na watumiaji wa hii mara nyingi hua na damu nyingi na hua mashambulio machache ya ugonjwa huu[crisis] kwa mwaka.ni moja ya virutubisho vya kisasa sana.nb unatakiwa uchague moja kati ya hizi, huwezi kutumia zote.

dawa ya korokwini; dawa hii humezwa kila wiki na mgonjwa wa sikoseli kuzuia ugonjwa wa malaria. dozi hutegemea na uzito wa mgonjwa.
                                                                 
matibabu mengine; mgonjwa huyu huonyesha dalili hizo akipata ugonjwa mwingine kama malaria, UTI, na mengine mengi hivyo mgonjwa hutibiwa kama watu wengine akiwa na shida hizo japokua hushambuliwa mara kwa mara kuliko watu wengine. mara nyini mgonjwa huongezewa maji haraka akifikishwa hospitali ili kufanya seli hizi zipite kirahisi.

jinsi ya kuzuia mashambulio ya mara kwa mara kwa mgonjwa;
kunywa maji mengi: angalau glass nane kwa watu wazima kwani ukosefu wa maji mwilini huchangia kupata mashambulio ya maumivu mara kwa mara kwa wagonjwa.
epuka joto kali au baridi kali; hali hizo mbili huweza kubadilisha PH[ kiwango cha tindikali na nyongo} kupanda sana au kushuka sana na kusababisha shambulio la maumivu.
fanya mazoezi mara kwa mara: mazoezi huongeza mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kufanya kinga ya mwili iwe vizuri.
usitumie dawa bila kuandikiwa na daktari; baadhi ya dawa zinazotumika kwenye maduka ya madawa kama ephedrine za mafua huweza kusababisha mishipa ya damu kubana sana[vasoconstriction] na kusababishwa kukwama kwa seli za mgonjwa ndani ya mishipa ya damu.
epuka kupanda ndege inayoruka angani sana;  kadri unavyozidi kupanda juu ndivyo hewa ya oksijeni inazidi kua kidogo hivyo unaweza kupata shambulio kwenye ndege.

madhara ya ugonjwa huu kama usipofuatilia matibabu vizuri;
upofu; mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye macho huweza kuzibwa na seli hizo na kuharibu baadhi ya sehemu za macho na kuleta upofu kabisa.
kuharibika kwa viungo vya mwili: ukosaji wa damu kwenye viungo kama bandama, figo na maini huweza kusababisha kushindwa kazi ka viungo hivyo na kupelekea kifo.
kiharusi; kuziba kwa seli ndani ya mishipa ya damu ya kichwa huzababisha kupooza kwa upande mzima wa mwili kitaalamu kama kiharusi.
pressure ya ndani ya mapafu: hii hutokea mara nyingi kwa wagonjwa watu wazima huonyesha kwa dalili ya kushindwa kupumua, na kuishiwa nguvu. mara nyingi huua haraka.[pulmonary hypertension]
vidonda; baadhi ya sehemu za mwili kukosa damu huchangia kutokea kwa vidonda kitaalamu kama ulcer.
mwisho;hakuna mganga wa kienyeji anaweza kukutibu huu ugonjwa ukapona kabisa, usipoteze pesa zako huko kabisa...kama kuna mtu anadai anayo dawa basi ajitangaze apewe tuzo ya dunia.fuatilia masharti ya madaktari na utaishi maisha ya kawaida kama wengine.
                                 tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                           STAY ALIVE

                   DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0653095635/0769846183

karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]