data:post.body vifahamu vipimo na matibabu ya ugumba kwa wanawake. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

vifahamu vipimo na matibabu ya ugumba kwa wanawake.

                                                                           
                        
makala iliyopita niliongelea sababu za ugumba kwa wanawake wengi, kama hukusoma angalia hapaHIZI NDIZO SABABU KUU KUMI ZA UGUMBA KWA WANAWAKE... lakini pia niliahidi kwamba ntaongelea vipimo na matibabu yanayotumika mahospitalini kutibu ugumba. hivyo leo tutaanza na vipimo kama ifuatavyo... 

kufuatulia mzunguko wa hedhi; mzunguko hufuatiliwa kuangalia kama unaenda vizuri na hakuna vitu ambavyo sio vya kawaida ambavyo ni dalili za ugumba kama kuona hedhi mara mbili kwa mwezi, maumivu makali wakati wa hedhi, kupata damu yenye mabonge na harufu isiyo ya kawaida. 

kufuatilia joto la mwili na utando unaotoka sehemu za siri; kama huna uhakika sana na siku yako ya hatari nunua themometer ya digitali ambayo ni rahisi kusoma[inauzwa elfu kumi tu] ya kupima joto kisha pima kila asubuhi. siku zako za hatari ya kubeba mimba joto litaongezeka kwa 0.5 degree na utando huo kama wa yai bichi utatoka. 

endometrial biopsy; hichi ni kipimo ambacho huchukuliwa kuangalia kama kuna tatizo lolote kwenye kuta za za kizazi. hivyo kiasi kidogo cha nyama hukatwa na kwenda kuchunguzwa. 

upimaji wa kiwango cha homoni; mwili wa binadamu una homoni nyingi sana, baadhi ya homoni kama oestrogen na progesterone huhusika moja kwa moja kwenye mfumo wa uzazi, hivyo ili mtu aweze kubeba mimba lazima homoni hizo ziwe kwenye kiwango fulani sahihi. yaani zisiwe kwa kiasi kikubwa sana au kidogoga sana. hivyo vipimo hivyo ni muhimu kwenye kutibu ugumba. 

hysterosalpingiography; kipimo hiki hupimwa siku saba mpaka kumi kabla yai halijashuka, hutumika sana kuangalingalia kama mirija ya inayopitisha mayai ya uzazi imeziba au vipi. 

laparascopy; kipimo hichi hutumika kuangalia kama kizazi, mirija ya mayai na mayai yanapozaliwa kama ni pazima au vipi. 

utrasound; hii ni mashine ya picha inayopatikana sehemu nyingi sana, huangalia kama kama kuna uvimbe wa kizazi, ugonjwa wa kizazi,, uvimbe wa ovari na kadhalika. ina uwezo wa kuona vitu vingi kwa wakati mmoja. 

MATIBABU YA UGUMBA.
matibabu ya ugumba ni magumu sana na yanaumiza kichwa kwani kila mtu hupatiwa dawa kulingana na chanzo cha ugumba wake, ukisikai kuna mganga ana dawa moja ya kutibu ugumba kwa watu wote huyo ni muongo, kimbia mbali hakuna kitu kama hicho. kimsingi ni kwamba mtu asipewe dawa yeyote bila kufanya vipimo na kugundua chamzo cha tatizo lake lakini pia matibabu hayatakamilika bila mwanaume kupimwa kujua kama ni mzima au vipi. matibabu yanaweza kua kama ifuatavyo; 

weka mazingira ya kupata mimba; yaani punguza uzito, acha kuvuta sigara, shiriki tendo la ndoa kila siku isipokua siku ya hedhi tu kwa mwezi mmoja mfulululizo. 

multimata; hii ni huenda ni dawa bora kuliko zote kwani imetengenezwa bila kua na kemikali hata moja kwa kutumia magome ya miti, matunda na mizizi huko nchini marekani. dawa hii nimeshuhudia ikiwasaidia waliokata tamaa kabisa kupata watoto kwa kurudisha mfumo mzuri wa homoni na kutibu baadhi ya magonjwa yaletayo ugumba. dawa hii haiko madukani mwa madawa na husambazwa na watu maalumu tu kwa kazi hiyo.

dawa za kusaidia kushuka mayai; dawa kama clomiphene citrate hutumika kusaidia yai kushuka kwa wanawake ambao hawana tatizo lolote la kiafya lakini mayai yao hayashuki kwenda kwenye kizazi. 

gonadotrophins; hii ni dawa ambayo hutumika iwapo clomiphene citrate niliyotaja hapo juu  ikishindwa kusaidia kazi vizuri. 

ugumba usiofahamika chanzo chake. wakati mwingine mtu anaweza kua mgumba na akapima kila kitu kikaonekana kizima, hawa hufanyiwa kitu kinaitwaa artifiacial insermination yaani mbegu za mwanaume zinaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa uzazi. 

kuhamisha kizazi; mwaka jana mwezi wa kumi mwanamke wa kwanza alijifungua mtoto nchini sweeden baada ya kuwekewa kizazi cha mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka sitini ambaye alikua hahitaji tena kuzaa. utafiti huo umeleta mwanga mkubwa kwenye ulimwengu wa uzazi. sasa hivi wanawake mia moja wameandikishwa kwa ajili ya uparesheni hiyo tena. kama tekinolojia hiyo ikifika africa huweza itakomboa wanawake wengi waliokata tamaa kabisa ya kuzaa.

mwisho: tatizo la uzazi linaweza likachukua miaka kupona na bahati nzuri kama shida yako haiwezekani, madaktari watakwambia ukweli mapema japokua waganga wa kienyeji hua sio wepesi kusema ukweli na lakini pia baadhi ya dawa nilizozitaja hapo juu hutolewa tu na daktari bingwa wa uzazi baada ya kujiridhisha kwamba unazihitaji kweli.

                                                                     stay alive...

                                                   dr.kalegamye hinyuye mlondo...

                                                      0653095635/0769846183
  

0 maoni:

Chapisha Maoni