data:post.body HIVI NDIO VIPIMO 7 VYA KUPIMA HARAKA UNAPOGUNDUA WEWE NI MJAMZITO.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIVI NDIO VIPIMO 7 VYA KUPIMA HARAKA UNAPOGUNDUA WEWE NI MJAMZITO..

                                                                    
                                                                         
watu wengi hua wakipata ujauzito hukaa na mimba zao nyumbani huku wakidi wanasubirii zikue kidogo halafu waende kliniki kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. kikawaida ukigundua tu una mimba hata kama ina wiki moja au mbili nenda kliniki ambapo utapimwa vipimo kadhaa muhimu ambavyo ni muhimu sana kwa ujauzito wako na lakini pia kuna baadhi ya magonjwa yasipogundulika basi yatasababisha mimba kutoka, mtoto kuzaliwa kabla ya muda, kuzaliwa mfu au kuzaliwa akiwa akiwa hana akili nzuri. hata kama ukiambiwa vipimo hivi havipo basi jitahidi ukavitafute hata hospitali binafsi kwa usalama wako.vipimo hivyo ni kama vifuatavyo.

wingi wa damu; hichi ni moja ya vipimo muhimu sana kwa wajawazito kwani upungufu wa damu kipindi hiki ni moja ya vyanzo vikuu vya kifo cha mama na mtoto.jipindi hiki mama damu yake haitakiwi ipungue chini ya 10g/dl na hutakiwa kutumia virutubisho vya kuongeza damu kama madini ya chuma, folic acid au mchanganyiko wa vyote kwa jina la haemovit.

virusi vya ukimwi; kuna watu wengi ambao ni waathirika wa virusi vya ukimwi lakini hawajui, kipindi hichi ni muhimu sana kujua afya wako kwani mimba inapunguza sana kinga ya mwili na kutafuna virutubisho kwenye mwili wa mama ili mtoto akue. hivyo ikifahamika wewe ni muathirika utapata faida kuu mbili; kwanza kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya mtoto aliyeko tumboni na wewe pia kuishi vizuri pili uweze kuwalinda uwapendao.

kipimo cha malaria: unaweza kua unadharau huu ugonjwa lakini ni moja ya vyanzo vikuu vya kutoka mimba, ndio maana mama hupewa vidonge vya sp katika kipindi fulani cha ujauzito ili kujizuia na malaria. lakini pia malaria inawez a kuua mama na mtoto hivyo kutumia neti kipindi hki ni muhimu sana.

vipimo vya magonjwa ya zinaa; ugonjwa wa kaswende ni mmoja wa magonjwa hatari sana, dalili zake zinaweza zisiwe rahisi kujua lakini hutoa mimba sana. hivyo ni vizuri kupima kaswende na magonjwa mengine ya zinaa kama gonorea na herpes simplex virus ambayo huweza kuleta upofu kabisa kwa mtoto.

kipimo cha choo ndogo na kubwa; choo ndogo hupimwa ili kuangalia kama hakuna ugonjwa wowote wa njia ya mkojo kwani ugonjwa wa uti huweza kuleta uchungu na kutoa mimba lakini pia huwasumbua sana akina mama kipindi cha ujauzito. choo kubwa mara nyingi hupimwa kuangalia minyoo.baadhi ya minyoo hutumia damu kama chakula na inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu mwilini.mfano hook worms..

mwisho; kuna maelekezo mengi na mahudhurio kadhaa mabayo mama hutakiwa ayafanye mpaka kipindi cha kujifungua, hivyo ni vema kwenda kliniki kama ulivyoelekezwa na kupokea chanjo zote muhimu na virutubisho muhimu ili kumpata mtoto mzima na mwenye afya.kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                        STAY ALIVE

                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0653095635/0769846183


0 maoni:

Chapisha Maoni