data:post.body Oktoba 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIVI NDIO VIPIMO 7 VYA KUPIMA HARAKA UNAPOGUNDUA WEWE NI MJAMZITO..

                                                                    
                                                                         
watu wengi hua wakipata ujauzito hukaa na mimba zao nyumbani huku wakidi wanasubirii zikue kidogo halafu waende kliniki kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. kikawaida ukigundua tu una mimba hata kama ina wiki moja au mbili nenda kliniki ambapo utapimwa vipimo kadhaa muhimu ambavyo ni muhimu sana kwa ujauzito wako na lakini pia kuna baadhi ya magonjwa yasipogundulika basi yatasababisha mimba kutoka, mtoto kuzaliwa kabla ya muda, kuzaliwa mfu au kuzaliwa akiwa akiwa hana akili nzuri. hata kama ukiambiwa vipimo hivi havipo basi jitahidi ukavitafute hata hospitali binafsi kwa usalama wako.vipimo hivyo ni kama vifuatavyo.

wingi wa damu; hichi ni moja ya vipimo muhimu sana kwa wajawazito kwani upungufu wa damu kipindi hiki ni moja ya vyanzo vikuu vya kifo cha mama na mtoto.jipindi hiki mama damu yake haitakiwi ipungue chini ya 10g/dl na hutakiwa kutumia virutubisho vya kuongeza damu kama madini ya chuma, folic acid au mchanganyiko wa vyote kwa jina la haemovit.

virusi vya ukimwi; kuna watu wengi ambao ni waathirika wa virusi vya ukimwi lakini hawajui, kipindi hichi ni muhimu sana kujua afya wako kwani mimba inapunguza sana kinga ya mwili na kutafuna virutubisho kwenye mwili wa mama ili mtoto akue. hivyo ikifahamika wewe ni muathirika utapata faida kuu mbili; kwanza kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya mtoto aliyeko tumboni na wewe pia kuishi vizuri pili uweze kuwalinda uwapendao.

kipimo cha malaria: unaweza kua unadharau huu ugonjwa lakini ni moja ya vyanzo vikuu vya kutoka mimba, ndio maana mama hupewa vidonge vya sp katika kipindi fulani cha ujauzito ili kujizuia na malaria. lakini pia malaria inawez a kuua mama na mtoto hivyo kutumia neti kipindi hki ni muhimu sana.

vipimo vya magonjwa ya zinaa; ugonjwa wa kaswende ni mmoja wa magonjwa hatari sana, dalili zake zinaweza zisiwe rahisi kujua lakini hutoa mimba sana. hivyo ni vizuri kupima kaswende na magonjwa mengine ya zinaa kama gonorea na herpes simplex virus ambayo huweza kuleta upofu kabisa kwa mtoto.

kipimo cha choo ndogo na kubwa; choo ndogo hupimwa ili kuangalia kama hakuna ugonjwa wowote wa njia ya mkojo kwani ugonjwa wa uti huweza kuleta uchungu na kutoa mimba lakini pia huwasumbua sana akina mama kipindi cha ujauzito. choo kubwa mara nyingi hupimwa kuangalia minyoo.baadhi ya minyoo hutumia damu kama chakula na inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu mwilini.mfano hook worms..

mwisho; kuna maelekezo mengi na mahudhurio kadhaa mabayo mama hutakiwa ayafanye mpaka kipindi cha kujifungua, hivyo ni vema kwenda kliniki kama ulivyoelekezwa na kupokea chanjo zote muhimu na virutubisho muhimu ili kumpata mtoto mzima na mwenye afya.kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                        STAY ALIVE

                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0653095635/0769846183


KAMA UNASUMBULIWA AU UNA NDUGU YAKO ANASUMBULIWA SANA NA MAUMIVU MAKALI YA JOINTI NA MIFUPA SOMA HAPA.

                                                                   
 ugonjwa wa maungio au jointi za binadamu sasa hivi unasumbua watu wengi sana hasa wazee japokua hata baadhi ya vijana siku hizi wanasumbuliwa pia. kitaalamu husababishwa na aina kuu tatu za vyanzo kama ifuatavyo.

HAYA NDIO MADHARA KUMI NA TANO YA DAWA ZA MENO USIYOYAJUA.

                                                           
katika dunia hii ya viwanda na biashara kuna mambo mengi tunayatumia kwenye miili yetu kama mafuta ya kujipaka, mafuta ya kula,perfum, bodspray, vyakula  na kadhalika ambavyo vinatuathiri sana kiafya na kusababisha vifo vingi duniani. hivi majuzi marekani wametengeneza mahindi ya kupunguza uwezo wa kuzaa na wana mpango wa kuyaleta africa kama msaada wakati tatizo la kutozaa limeshakua kubwa huku africa. leo ntaongelea dawa za meno tunazotumia kila siku ili niionyeshe dunia madhara yake kwani pamoja na madhara makubwa ya kiafya yatokanayo na dawa hizo za meno hakuna anayeweza kupaza sauti kwani ataua bishara za watu. dawa zote za meno zimechanganywa na kitu kinaitwa floride isipokua dawa moja tu ya forever toothpaste ndio imewekewa vitu asili tu bila kemikali hizi.
   flouride ina madhara yafuatayo;
  • husababisha cancer za aina mbalimbali.
  • huharibu ubongo kwa mtoto ambaye yuko tumboni.
  • hupunguza homoni za uzazi
  • huleta matatizo ya jointi za mifupa.
  • hupunguza uelewa wa watoto darasani.
  • husababisha kusahau sana.
  • hupunguza kinga ya mwili
  • inapunguza uwezo wa kuzaa kwa mwanaume na mwanamke.
  • hupunguza urefu wa maisha.
  • husababisha figo kushindwa kazi
  • inaua seli za ubongo.
  • inapunguza uzalishaji wa damu.
  • inaharibu kuta za tumbo la chakula.
  • huweza kusababisha ugonjwa wa akili.
  • inaharibu fidhi za meno.
ushauri; dawa zote za meno zinaonya kwamba mtoto akiimeza kwa bahati mbaya au mtu mzima akimeza nyingi kwa bahati mbaya akimbizwe hospitali haraka. sisi wote tunafahamu kwamba watoto wote humeza dawa za meno wakiwa wanapiga mswaki lakini pia hata watu wazima huwezi kutema dawa yote, lazima kuna kidogo sana itabaki mdomoni ambayo utaimeza tu. ni dawa ya forever toothgel pekee ambayo unaruhusiwa kuimeza bila shida yeyote kwani ikimezwa ina uwezo wa kutibu shida zingine za ndani ya tumbo. hivyo tuache kukwepa kununua dawa bora ya elfu kumi na tano au ishirini huku tukiandaa mamilioni ya pesa ya kwenda kutibiwa hospitali baada ya kupata madhara hayo hapo juu. kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                   STAY ALIVE

          DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0653095635/0769846183

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUPUNGUA MPAKA KILO TISA KWA SIKU TISA TU KWA KUTUMIA VIRUTUBISHO HIVI.

                                                                   
                                                   
hongera kwa kuingia kusoma makala hii kwani kwa mara ya kwanza kwenye maisha yako unaenda kusoma vitu ambavyo vinaenda kubadilisha maisha yako kabisa... yaani kama una kitambi au ni mnene anza kukiaga.
kwakweli uzito umezidi kua mzigo kwa watu wengi sana kwa sasa,  na wengi wao wameshakata tamaa kabisa baada ya kujaribu kila mbinu na kushindwa. wengine wanapungua na baada ya muda wanarudi katika hali yako yao ya zamani. kampuni ya forever living product ambayo hata madaktari wengi duniani wametokea kuiamini na kufanya nayo kazi sasa imezindua virutubisho kutoka kwenye mimea mbalimbali ya asili vinavyoweza kukupunguza uzito wa kilo tisa ndani ya siku tisa tu.

unaweza ukawa huamini lakini nimewashuhudia waliopungua na sasa wanaishi maisha safi kabisa wakiwa na uzito kidogo wa wao wa zamani bila hofu ya kunenepa tena. sasa wanaweza kwenda beach, kucheza mpira na kufurahia maisha kama watu wengine.

mchanganyiko;
mzigo wa clean 9 unakua na vitu vifuatavyo; juice ya aloe vera chupa tatu, forver lite au vanila chupa moja, vidonge vya forever garcinia plus 70, vidonge vya forever bee 100, t shirt moja na tepu ya kujipima.

jinsi inavyofanya kazi
virutubisho hivi huanza kwa kusafisha mfumo wa chakula na kuondoa sumu zote ambazo hubaki baada ya kula vyakula hasa vya mafuta mengi, sukari na kukaangwa sana kama chips, maandazi,chapati, sambusa na kadhalika kisha hupunguza hamu ya kula na kumfanya mtu ale kidogo na kuridhika  na pia huongeza kasi ya kuchoma mafuta mwilini  na huu ndio mwanzo wa maisha mapya ya bila kitambi na unene.

jinsi ya kutumia;
siku ya kwanza na ya pili.
hizi ni siku ambazo mwili utakua unasafishwa na kuondoa sumu au kemikali zozote zilizoganda ndani ya mwili wako na ukimaliza siku hizi mbili ukaenda kupima uzito utakua umeshapungua. kitu muhimu cha kuzingatia ni kwamba ndani ya siku hizi mbili utakua hautumii chakula chochote zaidi ya hizi bidhaa hivyo usijisahau ukaharibu mpango mzima.

  • asubuhi utakunywa vidonge viwili vya lishe vinaitwa garcinia[ ni kwenye kopo la maandishi ya blue imeandikwa garcinia kama umeshanunua product kwa msambazaji]
  • baada ya dakika ishirini utakunywa robo glass ya juice ya aloevera kwenye chupa la njano na hkikisha umeitikisa kwanza. kisha kunywa maji nusu lita na yasiwe ya baridi sana na ukiweza kunywa ya uvuguvugu.
  • baada ya hapo fanya mazoezi kwa dakika ishirini yaani inaweza kufanya usafi, kukimbia, kuruka kamba ni nzuri za na rahisi zaidi kwa mazingira yeyote. lakini hakikisha zoezi lolote utakalofanya likutoe jasho.
saa nne asubuhi
meza vidonge viwili vya bee pollen na maji robo tatu ya glass.

       mchana
  • vidonge viwili vya garcinia, dakika 20 baadae aloe vera robo glass na maji robo tatu ya glass kisha fungua kopo kubwa la kijivu kwa jina la forever lite ultra ndani yake kuna kijiko cha plastic. sasa changanya unga huo na glass ya maziwa yasiyo na mafuta au tumia maziwa ya soya kisha changanya unywe.kisha meza tena vidonge viwili vya bee polen.
wakati wa usiku
vidonge viwili vya garcinia plus na dakika 20 baadae unywe aloe vera robo glass na vidonge viwili vya bee pollen kisha wakati wa kwenda kulala kunywa aloe vera robo glass na maji robo tatu ya glass.

kumbuka; dosi hyo hapo juu ni ya siku ya kwanza na ya pili na siku hizo hutakiwi kula chochote zaidi ya
hivyo ninavyokuelekeza hapo juu.




siku ya tatu na ya hadi tisa;
hapa tayari mwili ushaanza kupokea mabadiliko na ukipima uzito utakuta umeshaanza kupungua, hapa unaweza kuaanza kula kidogo sio kama siku ya kwanza kama ntakavyoelekeza.

  • asubuhi ukiamka utakunywa vidonge viwili vya garcinia kisha dakika ishirini baadae utakunywa robo glass ya juisi ya alovera. hakikisha umeitikisa kwanza kisha maji robo tatu ya glass. kisha chukua vanila ultra changanya na glass moja ya maziwa ambayo hayana mafuta au maziwa ya soya na ukikosa kabisa tumia majia ya moto ila maziwa ni muhimu sana.
  • kama kawaida fanya mazoezi  kwa dakika ishirini kama nilivyoelekeza hapoa mwanzo mpaka utokwe jasho.
saa nne asubuhi
vidonge vinne vya bee poleni na maji robo tatu ya glass.

wakati wa mchana;
  • tumia vidonge viwili vya garcinia na baada ya dakika ishirini fungua kopo hilo la kijivu  lililoandikwa forever lite ultra ndani yake kuna kijiko cha plastic, chota unga uliopo humo kisha changanya na maziwa  yasiokua na mafuta au maziwa ya soya kisha koroga glass moja unywe.
  • kisha vidonge viwili vya bee pollen na maji robo tatu ya glass, hapa unaweza kula matunda kama tikiti maji, machungwa, apple na machenza lakini usile parachichi, ndizi au maembe.
wakati wa usiku;
akunywa aloe vera gel robo glass na maji robo tatu glass, garcinia vidonge viwili na dakika ishirini baadae ule chakula kidogo sana kama kipande cha samaki na wali au ugali kidogo sana kisha meza vidonge viwili vya bee pollen na wakati wa kwenda kulala tumia maji robo tatu ya glass tu.


mwisho; baada ya siku tisa kama umefuata maelekezo yote utakua umepungua kilo tisa, programu hii sio rahisi sana, usije ukaagiza virutubisho hivi kisha ukaanza kutumia huku ukijificha na kula vitu ambavyo hujaelekezwa kwani utakua unajidanganya mwenyewe, baada ya program hii maisha yako tunategemea yabadilike na utaanza kula kiafya yaani kutokula vyakula vingi sana ambavyo ni hatari kwa mwili wako. ni vizuri sana kutunza afya yako katika dunia hii ya sasa yenye vyakula vingi vilivyokaangwa na kemikali nyingi na kujifunza kula matunda, mbogamboga na protini kama samaki na dagaa huku ukila sukari na wanga kama ugali, viazi, mihogo, bidhaa zote za ngano kwa kiasi kidogo sana kwani ni moja ya vyanzo vikuu vya unene uliopitiliza. baada ya kupungua uzito huu wa kilo tisa kwa watu wengi wanakua wako vizuri ila kama wewe ni mnene sana na unataka uendelee kupungua kuna program inaweza kuendelea hapo kwanzia siku ya kumi mpaka thelathini inaitwa lifestyle 30 na utapungua zaidi. lakini pia bidhaa hizi zinaweza kua ni gharama kulingana na hali ya watanzania wengi lakini tunatakiwa kufahamu afya kwanza kisha mali zinafuata, kama unalimbikiza ujenge nyumba na na kununua gari ukiwa bado na kitambi na unene basi ugonjwa wa moyo utakuua kabla hujatimiza ndoto zako hivyo nakushauri uweke afya kwanza.lakini pia kama wewe ni mjasiriamali unaweza kutumia fursa hii kujiunga na kampuni ununue kwa bei ya chini na zingine uwauzie wapendwa wako na kisha utaendelea kupata bidhaa zaidi za kampuni hii nzuri na za ubora wa hali ya juu zilizothibitishwa na viwango vya ubora dunia nzima ikiwemo halal ya kiislam ambayo ni moja ya bodi ngumu sana kupata baraka zao duniani.

onyo; program hii ni marufuku kwa wagonjwa wa kisukari au itumike chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari kitu ambacho hapa tanzania ni kigumu kwani wao wanatakiwa wapunguze uzito taratibu na wakitumia program hii kuna hatari ya kupata hali inaitwa ketoacidosis ambayo inaua haraka sana.
kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                                 STAY ALIVE

            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. MAWASILIANO 0653095635/0769846183







HAYO NDIO MAMBO KUMI YA SIRI AMBAYO HAYASEMWI KUHUSU JUISI ZA ALOE VERA.

                                                                           
                                               
Aloe vera sio mmea mpya masikioni mwa watu kwani umetumika kwa miaka mingi sasa kutibu magonjwa mbalimbali na kuzuia vifo vingi ambavyo vingesababishwa na magonjwa mbalimbali. huku kwetu afrika watu wanafikiri bidhaa zinazotokana na mmea huu adimu ni dawa tu kwa binadamu. lakini ni kosa kusema hivyo kwani dawa ni kitu ambacho ukitumia kinakutibu na kuacha baadhi ya sumu zake...lakini bidhaa za mmea huu ni virutubisho ambavyo vinakutibu na kukuzuia na magonjwa mbalimbali. kiufupi wenzetu huko nje wanatumia bidhaa hii kama sehemu ya chakula lakini sisi tunatumia tukiugua tu, huenda ni sababu ya ugumu wa maisha yetu lakini kama unaweza bidhaa hizi zisiishe ndani kwako.
leo naomba nikupe siri kumi kumi usizozijua za  juice hii inayotokana na mmea wa alo evera ikiwa imetengenezwa bila kuwekewa kemikali hata moja.

kuondoa sumu mwilini: kama umeshawahi kuona mmea wa aloe vera yale maji yake ya ndani  ni mazito kama mlenda hivi, kwa hiyo ukinywa juice yake haitoki haraka tumboni kama maji ya kawaida hivyo kutoka kwake taratibu kunaifanya inyonye sumu zilizoko kwenye mfumo wa chakula  na mfumo wa damu ili kutoka nazo nje na kukuacha mpya.

hupunguza uzito; kuondoa sumu mwilini ni sawa na kufuta baadhi ya faili kwenye computer iliyojaa kwani computer hiyo itaanza kufanya kazi kwa haraka sana, hivyohivyo kwenye mwili sumu zikitoka mwili hufanya kazi kwa haraka sana na kupunguza mafuta yaliokua yameuelemea.

hulainisha choo; mara nyingi watu hupata choo ngumu sana kwa sababu ya kula vyakula visivyo na maji ya kutosha kama nyama nyingi na wanga bila kula matunda hivyo juice hii hulainisha na kusafisha njia ya choo kubwa, hii itakusaidia kupata choo kilaini sana.

ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari; kama unasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari juice ya aloe vera inasaidia sana kushusha sukari ya mwili na kukufanya uishi maisha safi sana.

matibabu ya magonjwa ya kinywa; utafiti unaonyesha juice hii huua bacteria wa mdomoni ambao huweza kusababisha magonjwa ya meno na ndio maana kuna dawa za meno zinatengenezwa kwa mmea huu.

hutibu magonjwa ya ngozi na chunusi; juice hii huupa mwili kiwango cha madini na vitamini za kutosha pia kuongeza maji mwilini, hii hulainisha ngozi yako na kukufanya ue na ngozi laini sana na yenye afya.

huongeza urefu wa nywele; kama unataka kua na nywele ndefu hasa kwa wasichana huu ni wakati wa kutumia juice hii kwani huweka mwili katika kiwango kizuri cha acid na base yaani ph na kusaidia ukuaji wa viungo vya mwili ikiwemo nywele zenye afya.

hupunguza cholestrol mwilini: utafiti unaonyesha beta sitisterol inayopatikana kwenye mmea huu inaweza kurudisha katika hali ya kawaida cholestrol nyingi inayokua imejaa mwilini, ambayo ni hatari sana na ndio chanzo kikuu vya magonjwa ya moyo.

inaongeza kinga ya mwili; juice hii inaondoa vimelea huru ndani ya mwili maarufu kama free radicals ambazo ni hatari kwa mwili kwani husababisha kansa. kimiminika hii kina vitamin e ambayo ni maalumu kwa kazi hiyo.

inatibu matatizo mbalimbali ya tumbo; kila mtu kwa wakati wake mwenyewe katika maisha hupata kiungulia, tumbo kusokota, kutapika ghafla, tumbo kuunguruma na kadhalika. juice hii hutuliza mihangaiko hiyo na husaidia sana katika kutibu madonda ya tumbo.

                                           jinsi ya kutumia;
mimina nusu glass ya juice hii ikiwa kawaida au baridi  na unywe mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni na moyo wako utakushukuru.

mwisho; juice hii unaweza ukanywa zaidi ya kiasi kilichotajwa kama una uwezo mkubwa wa kua na juice nyingi  zaidi lakini kiasi kilichotajwa hapo ndio cha chini kabisa kwa siku ili kiweze kukusaidia, lakini pia kama wewe ni mjasiriamali unaweza kujiunga na kampuni ukazipata nyingi kwa bei ya chini na kua msambazaji wa kampuni kwa kuwauzia watu wengine wawe na afya bora kama wewe. kampuni itakulipa kwa kuuza na kuingiza watu wapya kama wewe kwenye biashara yake.
kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                       STAY ALIVE

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.0653095635/0769846183






HAYA NDIO MAAJABU YA VIRUTUBISHO VYA MULTI MACA KWENYE KUTIBU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA UZAZI KWA WANAWAKE NA WANAUME.

                                                                 
ukisoma historia ya dunia, miaka 2000 iliyopita huko nchi ya peru ya marekani ya kusini, wanawake na wanaume walikua wakitumia mzizi huu kwa matibabu mbalimbali ya kibinadamu kama kuishiwa nguvu za kiume na kuwezesha wanawake kuzaa mpaka miaka zaidi ya arobaini bila shida. lakini pia kuwasaidia walioshindwa kuzaa sababu ya shida ya uzazi..

baada ya miaka mingi wataalamu wakaifanyia utafiti tena na kugundua mmea huu unafanya kazi kweli ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote na kutibu tatizo la ugumba liletwalo na matatizo mbalimbali, na njia pekee kuufikisha dunia nzima ni kuweka kwa mfumo wa kopo na tembe  ili isiweze kuharibika... leo hii virutubisho hivi muhimu viko tele nchini kwetu na kwa bei rahisi tu.

mwanzoni niliwahi kusema dawa ya kutibu nguvu za kiume duniani haipo... ni chakula tu na kuishi maisha bora ndio suluhisho pekee na msimamo wangu haukubadilika, nilipoona virutubisho hivi nikasoma mchanganyiko wake kwa makini sana na niliwasifu sana waliotuletea afrika kwani asilimia kubwa ya virutubisho hivyo hata huku afrika hakuna kabisa na hakuna kemikali hata moja kwenye mchanganyiko wake.

kukamilisha utafiti wangu nilimpa rafiki yangu mmoja wa kiume akajaribu na akaipenda sana na akanipigia  simu kwamba anataka nyingine ahifadhi kwani imemfanyia maajabu, lakini pia kuna dada yangu alikua na shida ya uzazi akiwa na umri wa miaka 35 bila mtoto alikua amekata tamaa kabisa baada ya kupima kila kitu na kuambiwa yuko sawa hospitalini, yeye na mume wake walipotumia virutubisho hivyo hawakumaliza wiki sita tayari mke alikua mjamzito.

virutubisho hivi vinafanya kazi vipi?
umri unavyozidi kwenda na mawazo yanapokua mengi , mwili unapunguza kasi ya kutengeneza homoni za binadamu na hii huleta uchovu, kunenepa, usingizi sana au kukosa usingizi, kuchoka, hisia za joto na baridi ndani ya muda mfupi kitaalamu kama hot flushes hivyo virutubisho hivi vikitumika hutoa taarifa kwenye ubongo kwamba utengenezaji wa homoni hizi uanze upya vizuri.

mchanganyiko wa virutubisho vilivyomo ndani ya virutubisho hivyo.
mzizi wa maca; mzizi huu huleta nguvu za mwili, huondoa uchovu, huondoa mgandamizo wa mawazo na hurutubisha uwezo wa  uzazi kwa wote mwanamke na mwanaume.
tunda la tribulus terestris; tunda hili huongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa jinsia zote kwa kushtua homoni za adrogens kwenye ubongo.
mzizi wa muira puama; hupunguza kiasi cha lehemu mwilini yaani cholestrol. wataalamu hivi karibuni wamegundua inazuia kansa ya ngozi na kansa ya kansa ya tezi dume.
magamba ya miti ya cuaba; magamba haya hufanya kazi ya kusaidia sana mfumo wa fahamu.
l -arginine; hii ni aina ya protini inayoleta misuli  yenye nguvu  na mifupa migumu, pia huleta nguvu za mwili, stamina na kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
tunda la saw palmetto; ni nzuri kwa ovari za mwanamke na tezi dume, lakini pia huzuia kipara cha uzeeni kwa wanawake na wanaume.
pygeum africana; hili ni gamba la mti linalotibu tezi dume iliyovimba.
coenzyme q 10; hii ni enzyme ambayo inatengeneza sana nguvu za mwili, imehusishwa na kusaidia kuishi maisha marefu, kushusha presha, ugonjwa wa moyo, kutibu maumivu ya kichwa na matibabu ya kansa.
soya; hii huweka sawa homoni za kiume na kuzuia dalili za uzee.

matumizi ya dawa hii kwa wanawake;
dawa hii hutumika sana tatizo la mvurugano wa homoni kwa wanawake ambao mara nyingi huleta maumivu ya tumbo, chunusi, hali ya joto kali na baridi kali wakati mmoja, hasira za mara kwa mara na mgandamizo wa mawazo hivyo kirutubisho hiki huamrisha mwili kutoa kiwango sahihi cha homoni.

kwa wanandoa au wachumba wanaotafuta mtoto virutubisho hivi hufanya kazi vizuri wakiitumia wote na sio kwamba inaongeza nguvu za kiume na mbegu tu ila inapambana na matatizo ya uzazi yanayoweza kuzuia mimba kama uvimbe wa ovari na kadhaliaka.

jinsi ya kutumia;
kopo moja lina tembe sitini za rangi ya chocolate  hivyo humezwa mbili kila siku kama chakula na maji mengi na matokeo yake huonekana ndani ya muda mfupi sana.

upatikanaji;
 kuna baadhi ya mikoa sio rahisi kuvipata kabisa virutubisho hivyo lakini kwa dar es laam vipo na ukihitaji unaweza kupata kwa wasambazaji maalumu na ukatumiwa mkoani sio maduka ya madawa au wasiliana na sisi tukuelekeze.

mwisho; dunia sasa hivi imejazwa na dawa nyingi kali na zenye sumu ambazo kama madhara yake yangetajwa hadharani wagonjwa wetu wangekataa kumeza dawa.  hivyo ni vizuri kumeza dawa za hospitali kama unaumwa kweli na unapoandikiwa na daktari tu, lakini pia ni vizuri kutumia sana virutubisho vya asili ili kujikinga na magonjwa mengine nyemelezi.lakini pia kama wewe ni mjasiriamali unaweza ukajiunga na kampuni hii  ukauziwa kwa bei ya chini ili uwasambazie na wengine uwapendao wenye matatizo kama haya. kampuni itakulipa kwa mauzo yako na kuongeza wasambazaji wapya kwenye biashara hii.
kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                       STAY ALIVE

                          DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 0653095635\0769846183[tuma meseji tafadhari]


JINSI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO YAWE MEUPE ZAIDI UKIWA NYUMBANI TU.

                                                                       
meno ni afya, mtu ambaye ana meno mabavu kikawaida hua hana afya nzuri na huteseka sana hasa wakati anapopata maumivu makali ya meno. lakini pia meno ni moja ya sehemu za mwili za urembo kwani mtu mwenye meno meupe sana hupendeza akitabasamu kuliko mwenye meno yenye unjano kwa mbali. kila mtu anatamani kua na meno meupe sana lakini kuna sababu mbalimbali zinazuia watu kufikia malengo hayo. leo tutaona jinsi ya kufanya meno yawe meupe sana, lakini siongelei meno ya watu wa arusha, moshi na manyara mabayo yameunguzwa na madini fulani hapana yale hayatibiwi kwa njia hii na hata ukisema uyatibu kwa njia yake yanapungua upana wake na kua rahisi kuvunjika muda wowote. naongelea meno ya watu wa kawaida ambao utotoni kama kawaida ya watu wote yalikua meupe lakini kwa sasa yamebadilika rangi.

vitu vinavyohitajika,
  • hydrogen peroxide mouth wash[inapatikana kwenye maduka ya madawa]
  • maji masafi.[nunua ya dukani]
  • mswaki
  • dawa ya meno nzuri.
jinsi ya kufanya.
  • nunua chupa ya hydrogen peroxide mouth wash, kisha changanya kiasi na maji masafi kwa uwiano sawa. yaani ile chupa ya dawa kama mils 100 hivyo changanya na mils 100 za maji.
  • baada ya mchanganyiko huo weka mdomoni kiasi cha mils 30[sawa na vijiko vitatu vya kulia chakula]. sukutua mdomoni kwa dakika moja kisha utahisi povu linatokea mdomoni hapo utajua dawa infanya kazi kwani kikemia dawa hiyo ikikutana na bacteria wamdomoni inatengeneza povu.
  • tema mchanganyiko wa mdomoni kisha safisha na maji ya kawaida tu baada ya hapo piga mswaki sio chini ya dakika tano ukisugua sehemu zote za meno yaani ya mbele ya nyuma na katikati, watu wengi hupiga mswaki dakika moja tu kitu ambacho ni makosa.
  • tumia dawa hii kila siku asubuhi tu mpaka utakapoona umeridhika na matokeo na hakuna madhara yeyote ya kutumia dawa hii.
njia nyingine ukishindwa hiyo hapo ya dawa; nunua dawa ya meno ya forever living toothpaste na iwe dawa yako kila siku maishani mwako na utaona mabadiliko kwani hung'arisha meno, huleta harufu nzuri mdomoni, huzuia kuoza meno na ni dawa bora kwa sasa kuliko dawa zote za meno zinazotangazwa dunia nzima kwani haina kemikali hata kidogo. na kama wewe ni mjasiriamali hii ni fursa kubwa, unaweza ukajiunga na kampuni ili uuzie wengine unaowapenda wawe kama wewe na kupata bidhaa zingine bora za kampuni hii ambayo mwaka jana iliongoza kwa mapato makubwa katika biashara za mtandao duniani.

mambo muhimu ya kuzingatia..
epuka kutumia vyakula vinavyoyapa rangi meno yako;  yaani kama soda, chai, red wine, kahawa na kuvuta sigara. unaweza kutumia soya kuweka kwenye chai badala ya majani ya chai.

piga mswaki mara mbili kwa siku; piga mswaki asubuhi na jioni baada  ya chakula na sio kabla ya chakula kama watu wengi wanavyofanya. kulala bila kupiga mswaki husababisha vyakula vilivyoko mdomoni kushambuliwa na bacteria usiku  na matokeo yake mtu hutoa harufu kali asubuhi. watu wanaopiga mswaki usiku hua hawanuki mdomo asubuhi.

kula vyakula vya asili; matunda kama karoti, maepo, machungwa, na kadhalika husaidia meno sana kutoa mabaki ya uchafu kuliko kula nyama kia siku ambazo huacha mabaki kwenye meno. vyakula vyote vyenye sukari nyingi kama keki, pipi, ice cream,chocolate, biskuti na kadhalika sio vizuri kuvitumia kwani ni hatari sana kwa afya ya meno na rangi ya meno yako.

toa uchafu katikati ya meno; kuna kamba nyembamba sana maalumu kwa meno, hutumika kitaalamu kutoa uchafu wa meno, hizo ni nzuri sana kuliko hizi toothpick zinazotumika na watu wengi.

onana na daktari wa meno; kawaida hautakiwi kwenda hospitali wakati unaumwa meno tu, ila unatakiwa uende umuone daktari wa meno angalau mara nne kwa mwaka ili aweze kugundua tatizo lolote la meno lililoanza bila wewe kufahamu, hivyo usisubiri ukose usingizi nduio uende hospitali.
 tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                                                                
                                                               STAY ALIVE

        DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO    MAWASILIANO 0653095635/0769846183



vifahamu vipimo na matibabu ya ugumba kwa wanawake.

                                                                           
                        
makala iliyopita niliongelea sababu za ugumba kwa wanawake wengi, kama hukusoma angalia hapaHIZI NDIZO SABABU KUU KUMI ZA UGUMBA KWA WANAWAKE... lakini pia niliahidi kwamba ntaongelea vipimo na matibabu yanayotumika mahospitalini kutibu ugumba. hivyo leo tutaanza na vipimo kama ifuatavyo... 

kufuatulia mzunguko wa hedhi; mzunguko hufuatiliwa kuangalia kama unaenda vizuri na hakuna vitu ambavyo sio vya kawaida ambavyo ni dalili za ugumba kama kuona hedhi mara mbili kwa mwezi, maumivu makali wakati wa hedhi, kupata damu yenye mabonge na harufu isiyo ya kawaida. 

kufuatilia joto la mwili na utando unaotoka sehemu za siri; kama huna uhakika sana na siku yako ya hatari nunua themometer ya digitali ambayo ni rahisi kusoma[inauzwa elfu kumi tu] ya kupima joto kisha pima kila asubuhi. siku zako za hatari ya kubeba mimba joto litaongezeka kwa 0.5 degree na utando huo kama wa yai bichi utatoka. 

endometrial biopsy; hichi ni kipimo ambacho huchukuliwa kuangalia kama kuna tatizo lolote kwenye kuta za za kizazi. hivyo kiasi kidogo cha nyama hukatwa na kwenda kuchunguzwa. 

upimaji wa kiwango cha homoni; mwili wa binadamu una homoni nyingi sana, baadhi ya homoni kama oestrogen na progesterone huhusika moja kwa moja kwenye mfumo wa uzazi, hivyo ili mtu aweze kubeba mimba lazima homoni hizo ziwe kwenye kiwango fulani sahihi. yaani zisiwe kwa kiasi kikubwa sana au kidogoga sana. hivyo vipimo hivyo ni muhimu kwenye kutibu ugumba. 

hysterosalpingiography; kipimo hiki hupimwa siku saba mpaka kumi kabla yai halijashuka, hutumika sana kuangalingalia kama mirija ya inayopitisha mayai ya uzazi imeziba au vipi. 

laparascopy; kipimo hichi hutumika kuangalia kama kizazi, mirija ya mayai na mayai yanapozaliwa kama ni pazima au vipi. 

utrasound; hii ni mashine ya picha inayopatikana sehemu nyingi sana, huangalia kama kama kuna uvimbe wa kizazi, ugonjwa wa kizazi,, uvimbe wa ovari na kadhalika. ina uwezo wa kuona vitu vingi kwa wakati mmoja. 

MATIBABU YA UGUMBA.
matibabu ya ugumba ni magumu sana na yanaumiza kichwa kwani kila mtu hupatiwa dawa kulingana na chanzo cha ugumba wake, ukisikai kuna mganga ana dawa moja ya kutibu ugumba kwa watu wote huyo ni muongo, kimbia mbali hakuna kitu kama hicho. kimsingi ni kwamba mtu asipewe dawa yeyote bila kufanya vipimo na kugundua chamzo cha tatizo lake lakini pia matibabu hayatakamilika bila mwanaume kupimwa kujua kama ni mzima au vipi. matibabu yanaweza kua kama ifuatavyo; 

weka mazingira ya kupata mimba; yaani punguza uzito, acha kuvuta sigara, shiriki tendo la ndoa kila siku isipokua siku ya hedhi tu kwa mwezi mmoja mfulululizo. 

multimata; hii ni huenda ni dawa bora kuliko zote kwani imetengenezwa bila kua na kemikali hata moja kwa kutumia magome ya miti, matunda na mizizi huko nchini marekani. dawa hii nimeshuhudia ikiwasaidia waliokata tamaa kabisa kupata watoto kwa kurudisha mfumo mzuri wa homoni na kutibu baadhi ya magonjwa yaletayo ugumba. dawa hii haiko madukani mwa madawa na husambazwa na watu maalumu tu kwa kazi hiyo.

dawa za kusaidia kushuka mayai; dawa kama clomiphene citrate hutumika kusaidia yai kushuka kwa wanawake ambao hawana tatizo lolote la kiafya lakini mayai yao hayashuki kwenda kwenye kizazi. 

gonadotrophins; hii ni dawa ambayo hutumika iwapo clomiphene citrate niliyotaja hapo juu  ikishindwa kusaidia kazi vizuri. 

ugumba usiofahamika chanzo chake. wakati mwingine mtu anaweza kua mgumba na akapima kila kitu kikaonekana kizima, hawa hufanyiwa kitu kinaitwaa artifiacial insermination yaani mbegu za mwanaume zinaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa uzazi. 

kuhamisha kizazi; mwaka jana mwezi wa kumi mwanamke wa kwanza alijifungua mtoto nchini sweeden baada ya kuwekewa kizazi cha mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka sitini ambaye alikua hahitaji tena kuzaa. utafiti huo umeleta mwanga mkubwa kwenye ulimwengu wa uzazi. sasa hivi wanawake mia moja wameandikishwa kwa ajili ya uparesheni hiyo tena. kama tekinolojia hiyo ikifika africa huweza itakomboa wanawake wengi waliokata tamaa kabisa ya kuzaa.

mwisho: tatizo la uzazi linaweza likachukua miaka kupona na bahati nzuri kama shida yako haiwezekani, madaktari watakwambia ukweli mapema japokua waganga wa kienyeji hua sio wepesi kusema ukweli na lakini pia baadhi ya dawa nilizozitaja hapo juu hutolewa tu na daktari bingwa wa uzazi baada ya kujiridhisha kwamba unazihitaji kweli.

                                                                     stay alive...

                                                   dr.kalegamye hinyuye mlondo...

                                                      0653095635/0769846183