Kutokana na uhaba mkubwa sana wa wahudumu wa afya hasa nchi za kiafrika na zingine zinazoendelea wazazi wengi hulazimika kuwapa dawa watoto wao pale wanapougua kwa sababu ya usumbufu mkubwa katika hospitali za serikali na gharama kubwa ya kupata huduma za afya katika hospitali za binafsi.
kiafya mtu yeyote hatakiwi kutoa dawa isipokua daktari tu na hasa nchi zilizoendelea sio rahisi kupata dawa hata duka la madawa bila kuandikiwa na daktari lakini kwetu hilo haliwezekani hivyo naomba niwape baadhi ya dawa ambazo ni marufuku mtoto kupewa kulingana na umri wake.
dawa ya mseto ya malaria: hii ni dawa inayotumika sana kutibu malaria na utafiti umeonyesha inafanya kazi vizuri na ndio maana ni chaguo la kwanza kwa matibabu ya malaria tanzania, inapatikana kwa mfumo wa vidonge na maji lakini dawa hii haitakiwi kupewa kabisa kwa mtoto chini ya miezi mitatu au mtoto chini ya kilo tano kwani uwezo wao wa maini kufanya kazi ni mdogo sana na hauwezi kupambana na dawa hii.hivyo watoto wa umri huo wanatakiwa watumie kwinini ya maji au sindano kutibu malaria.
aspirin: hii ni dawa ya muda mrefu sana tangu imegunduliwa, hutumika kutibu maumivu ya mwili na kichwa na kushusha homa kwa rika mbalimbali lakini pia hutumika kutibu matatizo ya moyo ikipewa kwa dozi ndogo lakini dawa hii ni hatari kwa watu wenye umri chini ya miaka kumi na nane, husababisha kuvimba kwa ubongo na maini kitaalamu kama reyes syndrome. hivyo watu wa umri huu ni vizuri wakatumia dawa kama paracetamol, diclofenac, ibuprofen na kadhalika.
ciprofloxacin; hizi ni dawa zinazopatikana kwenye kikundi kinachoitwa quinolones, zingine ni norfloxacin na nalidixic acid. dawa hii hutumika kuua bacteria na mara nyingi hapa tanzania hutumika kutibu typhoid, uti, magonjwa ya zinaa, magonjwa ya kizazi na mengine mengi. dawa hii ni marufuku kwa watoto chini ya miaka 12 kwani husababisha kuharibika kwa misuli inayotengeneza mifupa kitaalamu kama cartilage hali ambayo inaweza ikamfanya mtoto asitembee au asiongezeke urefu kabisa.
doxycline; hii ni dawa inayotumika kuua bacteria kitaalamu kama antibiotics, inapatikana kwenye group la dawa linaitwa tetracycline group. dawa hizi hutumika mara nyingi kutibu matibabu ya uzazi, magonjwa ya zinaa hata uti kwa hapa tanzania, lakini dawa hii ni marufuku chini ya umri wa miaka 12 kwani husababisha kubadilika kwa meno kua rangi ya njano kabisa kwa watoto na rangi hiyo haitoki tena na pia hukaa kwenye mifupa yao na kuzuia ukuaji.
chlorampenicol; hii ni dawa ambayo hutumika kutibu magonjwa yanayosababishwa na bacteria, kwa hapa tanzania dawa hii hutumika kutibu typhoid mara nyingi kwa watoto chini ya miaka 12, lakini dawa hii ni hatari sana kwa watoto chini ya mwaka mmoja kwani huleta hali inayoitwa gray syndome ambayo iliua watoto wengi sana kabla wanasayansi hawajagundua madhara haya. hata hivyo dawa hii inatakiwa itumike sio zaidi ya wiki mbili kwa wakati mmoja hata kwa watu wazima kwani husababisha kansa ya damu na upungufu wa damu kitaalamu kama aplastic anaemia ambayo haiponi kabisa. kwa maelezo zaidi soma hapa
SECRETS OF GOOD HEALTH
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni