data:post.body Septemba 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIZO SABABU KUU KUMI ZA UGUMBA KWA WANAWAKE.

                                   
ugumba ni nini?  
hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito baada ya kushiriki ngono mbili kinga kwa muda wa mwaka mmoja mfululizo. ugumba unaweza kua primary infertility yaani mtu hajawahi kubeba mimba kabisa   tangu azaliwe au secondary infertility yaani mtu ambaye amewahi kuzaa lakini kwa sasa ameshindwa kubeba ujauzito. utafiti uanonyesha katika kila ndoa tano au mahusiano matano ya kimapenzi basi uhusiano mmoja una matatizo ya uzazi ya kushindwa kuzaa. 

hali hii imekua ikiongezeka kadri miaka inavyosonga mbele kwa sababu mbalimbali kama mionzi ya mawasiliano yaani wi-fi , magonjwa mapya ya binadamu na kadhalika. kwa wanawake utafiti mpya unasema uwezo wao wa kubeba mimba unaanza kupungua baada ya miaka 30 ya umri kutokana na kuanza kuishiwa nguvu kwa viungo vya uzazi. ugumba una vyanzo vingi sana ambavyo vingine havifahamiki mpaka leo  lakini hebu tuone vyanzo muhimu vya ugumba. 

utoaji wa mimba;Huenda hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo kwani siku hizi kila karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba, utoaji wa mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, makovu yanayoletwa na vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi huweza kusababisha ugumba usiotibika.

matatizo ya vizaalishaji vya mayai [ovari]; ovari ni kiungo ambacho kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa na mbegu ya mwanaume lakini kuna magonjwa ambayo yanaweza kusababisha ovari hiyo ikaugua na kushindwa kutoa mayai, mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa ovarian cyst. 

matatizo ya mirija ya uzazi; ovari zimeunganishwa kwenye  mirija ambayo hupitisha mayai kwenda kwenye mfuko wa uzazi..wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba.mfano ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis. 

matatizo ya kizazi; kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi yote tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba. mfano, makovu ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa ya zinaa kama kaswende na kadhalika. 

kansakansa ya kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa kushindwa kujiweka kwenye kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba kuharibika au kutotungwa kabisa. 

matatizo ya mlango wa uzazi; oparesheni za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa huweza kusababisha kuziba kwa mlango wa uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa kabisa kupita kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba. 

magonjwa mengine ya mwili; magonjwa yeyote ya binadamu  ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta ugumba mfano magonjwa ya ini,kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika. 

matumizi ya sigara na pombe;  unywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai kutoka kwenye ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai kutembea kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine husababisha mimba kutunga nje ya kizazi. 

msongo mkubwa wa mawazo; ukiwa unatafuta mtoto tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate husababisha inasababisha mwili kutoa homoni kitaalamu kama cortisol ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi kitaalamu kama gonadotrophin releasing hormone hivyo hali huzidi kua mbaya. 

uzito uliopitiliza; mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji homoni za uzazi hivyo huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo kupunguza uzito ni moja ya njia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuzuia ugumba. 

mwisho; kabla hujaanza kuzunguka kwa waganga wa kienyeji na mahospitalini ni bora kujichunguza kama uko kwenye hatari zilizotajwa hapo juu. hakuna dawa moja ambayo ina uwezo wa kutibu ugumba kwa watu wote bila kutibu chanzo chake kwanza.... hivyo naweza kusema kila mtu ana dawa yake ya ugumba kulingana na historia ya maisha yake na chanzo cha tatizo lake. ugumba unaweza kupona kabisa kulingana na chanzo cha tatizo na hali ya ugonjwa ilivyo na unaweza usipone kabisa kama ugonjwa umeshapea sana, ndio maana kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kifedha, wasanii na wafanyabishara wakubwa lakini wameshindwa kupata watoto pamoja na kwenda mpaka nje ya nchi na kuonana na madaktari bingwa kwenye hospitali za kisasa kabisa.makala ijayo ntaongelea  matibabu ya ugumba kwa kina, usikae mbali. 

karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]
                                                                    STAY ALIVE
                                                 DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                                        0653095635\0769846183

               `


HIZI NDIO NJIA PEKEE ZA MWANAUME KUJUA KAMA MTOTO ANAYEMLEA NI WA KWAKE KWELI.


                                                             
                   
utafiti uliofanyika na mahakama ya harare huko zimbambwe umegundua kua asilimia 72% ya wanaume walioenda kuhakikisha uhalali wa watoto wao waligundua sio wa kwao. wengi wa wanaume hao walikua wameshawalea watoto hao kwa muda mrefu sana na watoto wengine wakiwa watu wazima. hali hiyo imezua hofu kubwa kwa wanaume wengine ambao hawajapima kwa kuhofia majibu. 
vipimo hivi vimevunja ndoa nyingi sana duniani, na mimi nasapoti kuvunjika kwa ndoa hizo kwani sio halali mwanaume  atokwe jasho kulea damu ambayo sio ya kwake bila kujua. 

hali hiyo sio huko tu, hata hapa nchini kwetu kuna watu wengi ambao wanalea familia kubwa bila kujua wanalea watoto wa watu wengine na sio wanaume tu kuna wanawake wengi ambao wamebeba mimba wakiwa kwenye mahusiano ya zaidi ya watu wawili. hali hii hufanya wao kushindwa kujua baba mzazi ni nani hivyo huamua kusingizia mmoja wao ili mtoto apate matunzo. 

nchi kama marekani, chinaspain na israel baba anaruhusiwa kuwapima watoto wake bila kumuhusisha mama husika ila kuna nchi kama ujeremani kipimo hicho hupimwa kwa amri ya mahakama kwenye kesi husika. vipimo vifuatavyo hutumika kujua ukweli. 

kipimo cha dna; kipimo hiki ni kipimo bora kuliko vipimo vyote yaani hakidanganyi hata kidogo, kwa sasa hupimwa kwa kuchukua mate kwa ndani ya mashavu kwa pamba maalumu. mate ya mtoto na mate ya mzazi hupelekwa maabara maalumu kwa ajili ya vipimo. matokeo huweza kutoka ndani ya siku mbili mpaka sita. matokeo hua ni aina mbili yaani asilimia sifuri 0% kama mtoto sio wako na  99.9% kama mtoto ni wako. kipimo hichi hapa nchini tanzania kinapatikana hospitali chache sana na kwa gharama kubwa hivyo ni ngumu kukipata kwa sababu ya gharama yake na hupimwa kwa amri ya mahakama. nchi zilizoendelea kipimo hiki hupatikana kirahisi sana yaani unakusanya mate wewe mwenyewe ukiwa nyumbani kwenye bahasha maalumu kisha unatuma posta na kuletewa majibu ndani ya siku mbili.

kipimo cha group za damu; kipimo hiki pia hutumika kujua uhalali wa wazazi husika hasa kwa nchi masikini sana kama zetu za africa ambazo ni ngumu sana na gharama sana kupata vipimo vya dna. kwa mfumo wa abo system kipimo hiki kinaangalia aina ya damu ambayo mama anayo, baba anayo na kuangalia kama mtoto ni wa kwao. yaani kwa maana nyingine kuna wazazi wa group fulani hawawezi kuwazaa watoto wenye group fulani kama ifuatavyo. 

  • wazazi wenye group A kila mmoja wanaweza kuzaa watoto wenye group A na O na hawawezi kuzaa watoto wenye group B na AB 
  • mzazi mwenye group A na mzazi mwingine group B wanaweza kuzaa magroup yote.
  • mzazi mwenye group A na mzazi mwingine group AB wanaweza kuzaa watoto wenye group A,B na AB lakini hawezi kumzaa group O. 
  • mzazi mwenye group a na mzazi mwingine group o huweza kuzaa group a na o lakini hawawezi kuzaa group B na AB. 
  • mzazi mwenye group B na mzazi mwingine mwenye group B huzaa group B na O na hawawezi kuzaa A na AB. 
  • mzazi mwenye group B na mzazi mwenye group AB huzaa group A, B, na AB ila hawawezi kuzaa group O. 
  • mzazi mwenye group AB na mzazi mwingine mwenye AB huzaa group A, B na AB ila hawezi kuzaa group O. 
  • mzazi mwenye group AB na na mzazi mwingine na group O huweza kuzaa group A na B ila hawawezi kuzaa group AB na 0. 
  • wazazi wenye group O wote huzaa watoto wenye group O tu na hawawezi kuzaa watoto wenye group A,B, na AB. 
  • kipimo hiki kinapatikana nchi nzima hata kwenye maabara ndogondogo nchini tanzania kwa bei ndogo sana. 

mwisho: kuna baadhi ya magonjwa yanaathiri mfumo wa binadamu[genetic diseases] yanaweza kusababisha watu wa group fulani kuzaa mtoto mwenye group ambalo si kawaida lakini ni mara chache sana, lakini pia kupima group la damu  vibaya kunaweza kuleta majibu ambayo sio ya kweli hivyo nashauri ukiona umepima ukakuta uko tofauti na mtoto ni vizuri kurudia vipimo tena au kwenda hospitali kubwa kuhakikisha na dna na pia wakati mwingine mtoto anaweza asiwe wako ila mkaonekana group ziko sawa kwasababu mwanaume aliyetembea na mke wako unafanana naye group za damu. hivyo dna ni ya uhakika zaidi na haina longolongo.
kwa maelezo zaidi soma hapa 

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                             STAY ALIVE 

                                               DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                        0653095635/0769846183


`
`

zifahamu dalili saba za hatari kipindi cha ujauzito.

                                                                             

kipindi cha ujauzito ni moja ya vipindi vizuri sana kwa mama anayetarajia kupata mtoto, kipindi hiki hua na shida mbalimbali ambazo husababishwa na mabadiliko ya mama katika nyanja mbalimbali za mwili wake. kuna mambo ambayo ukisikia mama analalamika kipindi hiki ni kawaida lakini kuna mambo muhimu ambayo ukiyasikia kwa mama mjamzito basi lazima uchukue hatua kama ifuatavyo.

kutokwa na damu sehemu za siri; damu nyingi kutoka sehemu za siri miezi mitatu ya kwanza ni dalili kwamba mimba imeharibika na kama damu hiyo inaambatana na maumivu makali ya tumbo la chini, inawezekana mimba imetungwa nje ya kizazi, lakini pia damu ikitoka kipindi cha miezi ya mwisho karibia na kujifungua ni dalili kwamba kondo la nyuma au placenta imejichomoa kwenye mfuko wa kizazi. hali hizi zinahiaji msaada wa haraka wa daktari hasa hasa mimba iliyotungwa nje ya kizazi, matibabu ya mimba iliyotungwa nje ya uzazi hua ni upasuaji wa haraka bila hivyo kifo huweza hutokea. 

kutocheza kwa mtoto: kawaida mtoto huanza kucheza wiki ya 16 mpaka 25, kama mda huo ukipitiliza bila kusikia chochote au mtoto alikua ameshaanza kucheza baadae ukasikia kimya huu ni muda muafaka wa kuwahi kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi na matibabu huenda mtoto amefariki au ana tatizo fulani.

kupata uchungu kabla ya wakati: wanawake wengi hawajui tofauti ya uchungu wa kweli na ule ambao sio wa ukweli, mfano ukisikia maumivu kwa muda, maumivu hayo hayaongezeki na hayana muda maalumu huo sio uchungu. ila ukisikia maumivu yanayotofautiana angalau kwa dakika kumi na maumivu yanazidi muda unavyozidi kwenda huo ni uchungu wa kweli. wahi hospitali ukasaidiwe kujifungua au kama muda bado nenda hospitali ili wazuie uchungu huo ili mtoto asizaliwe kabla hajakomaa.

kupasuka kwa chupa ya uzazi; hii kitaalamu inaitwa rapture of membrane, halii hii hutokea muda fulani baada ya uchungu kuanza na ni kawaida, lakini ukiona maji yanamwagika ghafla na una mimba kubwa inawezekana chupa hiyo imepasuka hivyo kuhakikisha nenda chooni alafu kojoa mkojo wote, ukiona maji bado yanaendelea kutoka basi maki hayo yanatoka kwenye mfuko wa uzazi hivyo kimbilia hospitali haraka kwani mtoto yuko hatarini. 

maumivu makali ya kichwa, kutoona vizuri, tumbo kuuma na kuvimba miguu; hizi ni dalili za kifafa cha mimba, ugonjwa huu umeua wanawake wengi sana kipindi cha kujiufungua, kuhakikisha hali hii nenda ukapimwe presha na ukiona presha iko juu kuliko kiwango cha kawaida wahi hospitali utibiwe. 

kichefuchefu na kutapika; ni kawaida kwa mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika lakini hali hii ikizidi na mama kushindwa kula na kutapika sana huku akiishiwa nguvu basi akimbizwe hospitali illi aongezewe maji na kuatafutiwa chanzo cha tatizo. kwa maelezo zaidi soma hapa 

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                             stay alive

                                            dr kalegamye hinyuye mlondo

                                                   0653095635/0769846183

HII NDIO NJIA BORA KULIKO ZOTE YA KUZUIA MIMBA KWA UZAZI WA MPANGO.

                                                                           
                                                               
Elimu ya uzazi wa mpango bado haijawafikia vijana wengi sana hasa tanzania, wengi wao hudhani labda
matumizi ya dawa na njia za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya malaya, watu waliokwisha zaa na kadhalika. lakini hii sio kweli kwani njia hizi ni nzuri kwa rika zote yaani vijana na watu wazima ambao wanashiriki ngono ila kwa sasa hawako tayari kupata mtoto.

kutotumika kwa njia hizi kumesababishwa kuzaliwa kwa watoto wengi ambao hawakupangwa, kujiua kwa wasichana kwa kukwepa aibu na utoaji wa mimba wa mara kwa mara.
utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba msichana akiingia kwenye mahusiano kwa miaka mitatu bila kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango anaweza kutoa mimba nne mpaka tano lakini pia asilimia kubwa ya wanachuo wa tanzania ambao huingia kwenye mahusiano vyuoni hawawezi kumaliza chuo bila kutoa mimba hata moja.

kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ikiwemo vitanzi, vijiti, kondomu,kutumia kalenda, sindano,vidonge, upasuaji wa kufunga mirija na kadhalika. kondomu ni njia bora sana kwani huzuia ukimwi na mimba pia lakini ukweli ni kwmba kama kondomu zingekua zinatumika vizuri basi hao watoto tusingewaona mtaani hivyo kama wewe hauko tayari kuzaa sasa hivi kwa sababu yeyote ile nakushauri utumie njia ya kijiti.

njia hii ikoje?
kijiti cha plastiki chenye homoni za uzazi huwekwa kwenye mkono wa mwanamke, homoni ndani ya kijiti hicho huzuia mimba kwa kwa kuzuia yai kutoka kwenye kiwanda yaani ovari kwenda kwenye kizazi . kijiti hiki huwekwa bure kwenye hospitali zote za serikali tanzania.

kwanini njia hii ni bora kuliko zote?

hurudisha uwezo wa kuzaa haraka: kama unatumia kijiti hata kama kiliwekwa wiki iliyopita, ukibadilisha mawazo ukataka mtoto kinatolewa na mwezi huohuo unapata mtoto, tofauti na njia ya sindano ambayo ukichomwa leo kuna uwezekano wa kukaa mpaka miaka miwili bila kupata mtoto.

ni rahisi kutumia: kijiti hiki kikishawekwa hospitali huhitaji kukumbuka chochote tofauti na vidonge ambavyo wakati mwingine mtu huweza kusahau asimeze akajikuta amebeba mimba.

inafanya kazi kwa muda mrefu sana; kama wewe ni binti mdogo au wewe ni mama ambaye una mtoto tayari na hauhitaji mtoto kwa sasa njia hii ni nzuri kuliko zote kwani huweza kuzuia mimba kwa miaka mitano mfululizo kwa asilimia mia.

haiingilii utoaji wa maziwa ya mama; vidonge vya uzazi wa mpango vyenye homoni zote mbili yaani oestrogen na progesterone kitaalamu kama microgynon huweza kupunguza wingi wa maziwa kwani wingi wake kwenye mfumo wa binadamu husababisha kupungua kwa homoni ya maziwa kitaalamu kama prolactin hormone.

haiongezi uzito; inaaminika vidonge vya uzazi wa mpango huongeza uzito kwa kuzuia kiasi kikubwa cha maji kisitoke ndani ya mwili kwa njia ya mkojo na pia kuongeza hamu ya kula, lakini utafiti kwa wanaotumia vijiti haujaonyesha madhara haya.

muda zaidi wa kushiriki tendo la ndoa: matumizi ya kijiti huzuia kutoka kwa damu ya kila mwisho wa mwezi ambayo kwa wengine huambatana na maumivu makali na kukosa raha ya kushiriki tendo la ndoa hivyo ukitumia kijiti utapata faida hii.damu inaweza ikatoka hata mara mbili kwa mwaka tu.

sio rahisi kwa watu wengine kujua: wasichana wengi hasa vijana hawapendi maisha yao ya ngono yafahamike, na hasa njia hizi za uzazi wa mpango watu wakijua unatumia wanakuona muhuni, kitu ambacho sio kweli, hivyo matumizi ya kijiti ni siri sana na sio rahisi kwa watu wengine kujua tofauti na vidonge ambavyo sio rahisi kuvificha.

mwisho; utafiti unaonyesha utoaji wa mimba umewanyima wanawake wengi watoto, msanii maarufu wema sepetu ambaye kwa sasa anatafuta mtoto kwa shida sana aliwahi kukiri kwamba aliwahi kutoa mimba zamani kidogo na huenda anajutia maamuzi yake.hivyo kama wewe ni msichana mdogo na hutaki kuzaa kwa sasa au wewe ni mama hutaki mtoto mwingine kwa sasa tumia njia hii ya uzazi wa mpango itakusaidia sana. kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                                          STAY ALIVE

                                                      DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                                                 0769846183/0653095635