Unene ni nini? Hii ni hali ya mtu kua na uzito mkubwa kuliko
uzito ambao anatakiwa awe nao kulingana na urefu wake, mfano njia nzuri ya kujua
wewe ni mnene ni kutumia njia hii rahisi. Pima urefu wako halafu toa kwa mia. Mfano
kama una urefu wa sentimita 180 toa mia utapata 80. Hivyo wewe hutakiwi
kuzidisha kilo 80. Kama una urefu wa sentimita 170 halafu una kilo 75 yaani
umezidi kilo tano, wewe ni mnene tayari
kulingana na fomula hiyo niliyoisema hapo juu. Watu wengi wako bize wakitafuta
dawa ya kitambi, lakini mimi nasema hakuna dawa ya kitambi duniani wewe kama
una kitambi rudisha mwili wako kwenye uzito wake halali na kitambi kitaondoka
chenyewe.
Mwaka 2013 nchi ya marekani ilitangaza kutambua tatizo la
unene kama magonjwa mengine na mtu mnene akienda hospitali anatakiwa aanzishiwe
matibabu haraka sana ya unene huo kama wagonjwa wa utapiamlo wanavyotibiwa au kama
magonjwa mengine kutokana na madhara
makubwa ya mtu kua mnene.
Tatizo la unene limekua kubwa sana hasa sehemu za mijini,
miaka ya nyuma sana tatizo hili lilikua likiwasumbua hasa watu wa nchi
zilizoendea lakini kutokana na utandawazi na sababu mbalimbali unene umekua
kawaida sana hadi kwa nchi zetu maskini, lakini pia hali ya watu kua maskini
sana kipindi wakiwa wadogo na kupata
fedha ukubwani nalo limechangia sana unene kwasababu ya watu hawa kuishi maisha
kama wanalipiza kisasi cha umaskini wao wa zamani.
Upande wa wanawake wa kiafrika sisi tunawaita wamama yaani
hawa watu baada ya kufika miaka 35 na kuendelea wao huona unene ni halali yao
kwa kisingizo cha uzazi. Lakini tujiulize mbona wenzetu wazungu wenye umri huo
na wamezaa sio wanene? Hapa yunaona kua kuna tatizo kubwa la ulaji wa chakula
na mfumo wa maisha ambao ni hatari sana kiafya.
Sio kweli kwamba kitambi ni fedha ila hizi ni imani
zilizoanzishwa na watu kujaribu kuutetea unene ,Leo ntaenda kuongelea sababu
muhimu zinazosababisha unene ambazo huenda ukiziepuka unaweza kupunguza unene
au kuepuka unene.
Unene unasababishwa na sababu kuu mbili muhimu.
Kula sana kupita kiasi; watu wengi wanene ukiwauliza
watakwambia eti wao wanakula kidogo afu hawajui unene unatoka wapi…lakini
ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho kama unakula chakula kingi kuliko
shughuli unazofanya lazima utakua mnene, mwili utabaki na mafuta mengi na ukose
pakuyapeleka matokeo yake kitambi hakikuishi. Utakuta mtu yupo kwenye
tv au laptop siku nzima kazi yake ni kwenda kupakua na kula tu. Kama wewe sasa
hivi ni mnene afu unakula kidogo maana yake zamani ulikua unakula sana ndio maana uko hivyo na kama
umepunguza sasa hivi maana yake utapungua kidogo kwa uzito na huenda
ungeendelea na tabia yako ya zamani ya chakula ungekua mnene zaidi ya hapo
Kutofanya mazoezi: ni watu wa chache sana hapa kwetu Tanzania
na afrika kwa ujumla wana tabia ya kufanya mazoezi [inaweza kua hata asilimia
mbili tu ndio wanafanya mazoezi} kwa kusingizia eti wako bize sana lakini
ukweli ni kwamba, katika kila masaa 24 unatakiwa ufanye mazoezi hata nusu ili
kuuweka mwili wako katika hali ya kiafya na mazoezi hayo yanatakiwa yawe sehemu
ya maisha yako kama unavyo kula, kuoga na kwenda chooni. Sheria ya afya ni
kwamba kama unapata muda wa kula lazima upate na muda wa kufanya mazoezi kama
uko bize sana mpaka huwez kufanya mazoezi basi uache na kula. Mwili ni kama
gari, ukilijaza mafuta gari lazima litembee ili mafuta yaweze kupungua sasa
kama unajaza gari mafuta afu unalipaki, unategemea mafuta yatapungua? Huu ni
mfano hai wa watu wanaokula na kulala tu bila kufanya chochote. Lakini pamoja
na sababu hizi kuu mbili kuna mambo yanachangia watu kua wanene kama ifuatavyo.
Ukoo[genetics]; vimelea unavyorithi kutoka kwa wazazi
vinaweza kuchangia sana jinsi mwili wako unavyohifadhi chakula, mahali
unapoweka mafuta mwilini, na uwezo wake wa
kuayatumia mafuta.. ndio maaana unaweza ukawa unakula chakula cha aina
moja na mtu Fulani, yeye ananenepa na wewe hunenepi na lakini pia kuna familia
ukizichunguza utakuta ukoo mzima watu ni wanene sana au watu ni wembamba
sana lakini sio kurithi tu, watu wa
familia moja hua na tabia zinazofanana na aina ya ulaji wao huweza kuathiri
ukubwa wa miili yao.
Kutokula kiafya; tabia ya kula sana vyakula vya wanga kama
ugali, viazi, mihogo na wali kwa kiasi kikubwa sana kunachangia watu wengi
kunenepa sana huwezi ukakuta mtu amekula njegere nyingi au maharge mengi na
ugali kidogo, mfumo wetu wa kimaisha ugali lazima uwe mwingi kuliko mboga kitu
ambacho lazima kilete unene tu..chakula cha kawaida cha kiafya ni ugali kidogo,
maharage kidogo, mboga za majani kidogo, tunda kidogo na maji mengi.
Magonjwa ; kuna magonjwa huleta unene kwa binadamu moja kwa
moja mfano ugonjwa wa homoni kitaalamu kama cushing syndrome na magonjwa yote
ambayo yanaweza kufanya mtu ashindwe kutembea au kuzunguka humletea unene. Mfano
magonjwa ya miguu
Dawa: kuna dawa husababisha unene kama usipofanya mazoezi au
kula vizuri kupunguza madhara yake,
mfano vidonge vya uzazi wa mpango, baadhi ya dawa za kifafa, dawa za kisukari,
dawa za presha na dawa za msongo wa mawazo.
Umri: kadri mtu anavyozidi kuongezeka umri ukubwa wa misuli
ya mwili wake hupungua na mafuta huongezeka na kasi na kasi ya kupunguza chakula mwilini hupungua [metabolism], hivyo wingi wa chakula
unachokula unatakiwa upungue kulingana na umri wako hivyo kama hauko makini utaongezeka
uzito.
Kukosa usingizi wa kutosha: hii huweza kusababisha
mabadiliko ya homoni mwilini na kuongeza hamu yako ya kula na kuanza kula ovyo hivyo kunenepa sana.
Kuacha sigara; watu wanaovuta sigara mara nyingi hua hawana
hamu ya kula sana kama watu ambao hawavuti sigara, hivyo kuacha sigara
kutafanya hamu kua kubwa na kuongezeka uzito hivyo kuongezeka uzito. Lakini ni
vizuri kuacha sigara kuliko kuendelea.
Mazingira; marafiki zako na watu unaokaa nao huweza
kuchangia wewe kua mnene kwasababu tu wao ni wa wanene na tabia zao za kula sio
nzuri hivyo unaweza ukajikuta umeingia kwenye mkumbo na kuanza kula kama wao
lakini pia kuishi mazingira ambayo hayana sehemu ya kufanya mazoezi huweza
kuongeza uzito.
Ujauzito:mwanamke akibeba mimba anaongezeka kilo 12.5 na
akizaa anapunga kilo sita tu na kubaki na kilo 6.5 hivyo mwanamke akishindwa
kupunguza huu uzito hujikuta anaongezeka kila akizaa na wanawake wengi hushindwa
kabisa kuupunguza uzito huu na kuwa wanene siku zote za maisha yao.
Mwisho: pamoja na sababu nilizotaja zinazochangia kuongeza
uzito hapo juu bado kuna uwezekano wa
kupambana nazo kushusha uzito kama ukifuata kanuni za afya, makala ijayo ntaongelea njia muhimu za kushusha
uzito, tue pamoja.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni