Huenda wewe msomaji umeshakata tama kabisa ya kupungua uzito
baada ya kutumia njia mbalimbali bila mafanikio, lakini naomba nikupe matumaini
kwamba swala la kupunguza uzito na kutoa kitambi linawezekana kabisa na sio
gumu kama watu wanavyofikiria. Leo ntaenda kutoa elimu muhimu sana ambayo
ukiifuata kwa makini utapungua uzito.
Kiukweli unene unatesa sana kimwili na kisaikolojia, yaani
uchovu mara kwa mara, jamii inakuona tofauti sana na huenda hata kupata mpenzi
ikawa ngumu kidogo, kukosa baadhi ya kazi na kushindwa hata kuvaa baadhi ya
nguo kwa ajili ya unene lakini hebu tuyaache hayo tuongelee maada kuu.
Formula ya unene ni ndogo sana, ukila sana kuliko shughuli au
mazoezi unayofanya unaongezeka uzito, ukila kidogo na kufanya mazoezi sana
unapungua uzito, kiasi unachokula kikilingana na shughuli na mazoezi unayofanya
unabaki kwenye uzito ule ule.
Kitaalamu chakula huchangia asilimia 70% kupungua uzito wakati mazoezi huchangia asilimia 30% na kazi ya mazoezi sio kukupunguza tu bali kukurudisha kwenye shepu.
Kwa maana nyingine kufanya mazoezi tu bila kuzingazia chakula hakuwezi kukusaidia kabisa.
Kupunguza uzito inatakiwa mtu ubadilishe MFUMO wako wa maisha kabisa kama ifuatavyo.
Kuhusu ulaji wa chakula;
Epuka vyakula vya kukaanga sana na wanga; vyakula
vinavyonenepesha ni vyakula vya wanga na mafuta kama ugali, wali,mihogo,viazi,chapati,maandazi na ngano zote,nyama
ya mafuta kabisa,chips na kadhalika..vyakula hivi vinatakiwa viliwe sana na
watu wanaofanya kazi ngumu kama wanaolima, kupasua mbao, kubeba mizigo na
zingine ngumu kama kazi zako ni kushinda umekaa unatakiwa ule kidogo sana aina
hii ya vyakula.yaani badala ya kula ugali mkubwa au wali mwingi na mboga kidogo
unatakiwa ule ugali mdogo au wali kidogo na mboga nyingi kama
maharage,mchicha,njegere,samaki,nyama ya kuku na kadhalika.
Kunywa maji mengi; hakikisha unakunywa maji mengi kama nusu
lita au lita moja nusu saa kabla na nusu saa baada ya kula, hii itakufanya ujaze tumbo maji
ujisikie kushiba na ule kidogo pia maji mengi kwa siku kama lita tatu yanasaidia mwili kuchoma mafuta vizuri na kuondoa sumu mwilini.
Kula milo midogo midogo: utafiti umeonyesha ile milo mikubwa
inayojaza tumbo ndio imafanya watu wanenepe sana na milo midogo midogo hata
mara nne kwa siku inaongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta, hivyo epuka kula
mpaka kulijaza tumbo kabisa, kula kawaida ukina umeshiba acha sio lazima chakula kiishe.
Kula ukiwa una njaa tu;epuka kula kwasababu eti muda
umefika, kula ukiwa na njaa tu na ukiona njaa imekubana usiku kula vyakula ambavyo ni laini sana mfano karoti mbichi, matunda, mboga za
majani.
Epuka kushindaa njaa; watu wengi hushinda njaa wakidhani eti
watapungua uzito , unaposhinda njaa mwili unadhani uko kwenye shida ya chakula hivyo ukila
baadae mwili unahifadhi mafuta mengi zaidi kwa matumizi ya baadae na watu wengi wanaoshinda njaa hula
chakula kingi jioni na kuleta shida na hata hivyo huwezi
kushinda njaa maisha yote hivyo kinachotakiwa ni kupata mfumo mpya wa maisha ili uuzoee.
Epuka kula kwenye sahani moja na watu wengine; ukila na watu
huwezi kujua kiasi gani hua unakula hivyo ni rahisi sana kula chakula kingi
bila kujua, hivyo pakua kwenye sahani yako ndogo{achana na sahani kubwa
itakufanya upakue kingi] halafu kula peke yako.
Kula taratibu; mishipa ya fahamu inachukua muda wa dakika 20 kutambua kama umeshiba baada ya kula, hivyo ukila ndani ya dakika tano ukamaliza kula, utajikuta hujashiba kwasababu
mishipa ya fahamu haijatoa taarifa kwenye ubongo lakini ukila kwa dakika
ishirini taratibu chakula kilekile unachokula kila siku unaweza ukajikuta unakibakiza. Kula
taratibu inaweza kua changamoto kidogo hivyo hakikisha unajipa kila siku muda
wa kutosha wa kula yaani usile ukiwa na haraka unawahi sehemu. Lakini pia kama umezoea kula
haraka utapata shida kula taratibu hivyo jaribu kufanya mambo mengine wakati
unakula kama kutumia simu, kuangalia TV au kuongea na mtu huku ukiangalia saa
yako.
Funga kula baadhi ya vyakula; simaanishi kushinda njaa hapana,
unaweza ukawa unazitoa siku mbili au moja kwa wiki. Siku hizi kula matunda tu
na mboga za majani na maji bila kula chakula kingine chochote, hii huumpa muda mwili wa kujisafisha sumu zote na
kupungua uzito kirahisi zaidi.
Epuka vyakula vyenye sukari sana; acha kula
biskuti,soda,keki,pipi,jojo, chai yenye sukari nyingi na mengine mengi ambayo hayana msaada kwenye
mwili kwani sukari ni moja ya chanzo kikuu cha unene mwilini na vyakula hivyo havina msaada
mwilini zaidi ya kuongeza sumu. sukari hulazimisha mwili kutengeneza sana homoni kwa jina la insulini ambayo kazi yake sio kuvunja sukari tu bali na kuhifadhi mafuta pia.
Punguza unywaji wa pombe; pombe hasa bia ina ngano nyingi
ambayo huongeza unene lakini hata pombe ambazo hazina ngano zina mchango ambao moja kwa moja kukunenepesha kwanza kwa kukufanya ule sana na ule vibaya yaani bila kufuata diet yako baada ya kulewa lakini pia maini yako hufanya kazi ya kuondoa pombe mwilini muda huo na kuacha kazi ya kuchoma mafuta hivyo usidanganyike kwamba pombe kali inapunguza uzito.
Punguza ulaji wa chumvi; weka chumvi kidogo sana kwenye
chakula chako kwani chumvi huzuia maji yasitoke ndani ya mwili{kumbuka 60% ya
binadamu ni maji tu].
Kua na msimamo: wewe ndio unajua unataka nini kwenye mwili
wako, usiburuzwe kwenye vikao vya kula sana kwenye sherehe au kitu chochote na
kama umeshakula sema umekula.
Piga mswaki baada ya kula mlo wa usiku; hii sio tu itatunza meno yako
lakini pia itakufanya usipate hamu ya kula zaidi na mara kawaida ukishapiga
mswaki hautakiwi kula tena, mbinu hii itakusaidia sana.
Pima uzito kila wiki; kama hujui maendeleo yako na hujui unataka
ufikishe kilo ngapi bila mzani basi unapoteza muda, kua na mzani kutakufanya
upate moyo wa kuendelea na mfumo wako wa maisha lakini hata ukipima mwisho wa
wiki na kugundua hujapungua usife moyo endelea tu.
mazoezi; sheria za afya zinasema kama mtu anakula chakula mazoezi ni lazima, japokua mtu
anaweza kupungua kwa chakula tu, mazoezi huweza kusaidia sana kupungua
uzito.kufanya mazoezi hasa kwetu afrika ni kama adhabu kwa watu wengi lakini
mazoezi ni muhimu sana. Kama kazini unaenda kwa mguu, baiskeli au kazi zako ni za nguvu sana hii inaweza kua
zoezi tosha. Kulingana na hali ya maisha
ya sasa kubana sana, kukosa muda wa kwenda gym au kushindwa kukimbia barabarani
sababu ya pikipiki nyingi napendekeza utumie zoezi la kuruka kamba. Fanya hili
zoezi nusu saa tu kwa siku ndani ya 3 au 4 kwa siku inatosha sana. Shida ya mazoezi sio kuanza bali kuendelea, wengi wenu
mtaanza kwa fujo afu mtaacha. Fanya mazoezi kama sehemu ya maisha yako,
ukifanya kidogo kila siku ni bora sana kuliko kufanya kwa fujo siku moja na kuacha.
Usikate tamaa; katika mafanikio yoyote ya binadamu sio unene
tu hata mafanikio ya kifedha yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu.. wanaokata tama
ndio hao kila siku hawafanikiwi, kama umeamua kufanya kitu, usifanye nusunusu
fanya kwa akili yako yote na utafanikiwa. Hayo mambo niliyotaja hapo mwanzoni
kuhusu chakula na mazoezi yataonekana
magumu mwanzoni lakini baaada ya muda mwili utazoea na wewe ndio utapata kilevi
au addiction mwisho itakua ndio maisha yako mapya na vitambi utavisikia
redioni.
.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635\0769846183
0653095635\0769846183
www.sirizaafyabora.info
0 maoni:
Chapisha Maoni