Wengi najua mmeshangaa sana kuona hii post lakini huo ni
ukweli mchungu unaofanya watu wanakana watoto na kuacha ndoa zao kwa kudhani
wamesalitiwa wakati mimba ni zao na watoto ni wa kwao wenyewe.
Kwenye blog hii nimeshaongelea zaidi ya mara mbili mambo
haya ya kuhesabu siku zako za hatari lakini hili sikulizungumzia, basi hebu
twende sawa upate kunielewa vizuri na kama hukusoma hizo za nyuma na hujui kuhesabu siku zako za hatari soma hapa
Nilisema kwamba wanawake wote, siku yao ya hatari ya kubeba mimba ni siku ya
14 kabla ya kuona mzunguko unaofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita kama mnavyodanganyana mtaani.
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku
yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza
kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku
nne kabla ya siku ya kumi na nne na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari, hivyo siku zingine za hatari ni siku ya
10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14
utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, [ hapa ndio mtu anaeza anabeba mimba kwa
kushiriki ngono akiwa kwenye hedhi], mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua
21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu. sasa kama mtu
huyu anaona hedhi kwa siku nne afu akatembea na mwanaume siku ya nne au ya tatu wakati damu inaendelea kutoka basi mbegu
za mwanaume zitaishi mpaka siku ya saba na kukutana na yai la kike ambalo litashuka
siku hiyo ya saba na mimba kutunga, hivyo kama hufuatilii mzunguko wako akibeba mimba siku ya hedhi usishangae.
Mwisho: nimeandika hii makala makusudi kwani najua kuna watu
wanatabia za kufanya ngono kipindi cha hedhi au wakati hedhi iko inaisha au
tarehe za mwanzo baada ya hedhi kuisha wakidhani mimba haiwezekani basi leo
taarifa ni kwamba inawezekana cha msingi fuatilia mzunguko wako vizuri usije
ukaanza kusumbua watu ukishanasa mimba ambayo hukuipanga. unaweza kupitia blog yetu ya kingereza kwa maelezo zaidi soma hapa.
SECRETS OF GOOD HEALTH
STAY ALIVE
DR.
KALEGAMYE HINYUYE MLONDO. 0653095635\0769846183
Hayaaa mbaba...nimekusoma no mistake
JibuFuta