Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti kwamba zaidi ya
watu milioni mbili a laki nane wanakufa kila mwaka sababu ya kua na uzito
mkubwa kuliko kawaida na watu milioni thelathini na tano wanapata ulemavu sababu
ya unene kila mwaka, ni kweli chakula ni muhmu kwa afya zetu lakini ulajia wa
chakula uliopitiliza ni hatari sana na huweza kusababisha magonjwa yasiyotibika
kabisa..
unene unaangilia mfumo mzima wa kazi za mwili wa binadamu na kusababisha
hali hizo. Kama kawaida ni vizuri kama ukigundua una uzito ambao sio wa kawaida kuanza kazi ya kuushusha mapema kabla hali haijawa mbaya
zaidi,,, ukishaona una kitambi usijiulize mara mbili hayo ni mafuta tayari hivyo lazima uzito wako umezidi.. kawaida mwili wa mwanaume huhifadhi mafuta ya ziada tumboni na mwili wa mwanamke huhifadhi mafuta ya ziada kwenye makalio lakini mafuta yakizidi huweza kuhifadhiwa kote makalioni na tumboni…..yafuatayo ni madhara ya unene yanayobabisha vifo hivyo na ulemavu wa kudumu..
Ugonjwa wa kisukari; hii ni ugonjwa ambao mwili hushindwa
kupambana na wingi wa sukari uliopo ndani ya mwili wa binadamu kutoka kwenye
chakula anachokula kila siku na hii huweza kusababishwa kutotengenezwa kabisa
kwa homoni ya insulin[diabetes type one] au homoni ya insulin kushindwa kuingia
ndani ya cell nene[fat cell] ambazo huwepo mtu akiwa mnene sana. Ugonjwa huu
unaathiri sana watu wazima kwanzia miaka arobaini kwani wengi wao hushindwa
kupambana na uzito.ugonjwa huu unaweza kuanza bila mgonjwa kujua na kuja kujua kama anaumwa
katika steji za mwisho ambapo wengi hukatwa miguu baada ya kupata vidonda
visivyopona. Hakuna dawa ya kutibu kabisa ugonjwa huu ila kuna dawa za kusaidia
kushusha sukari na hutumika kwa maisha yote.
Ugonjwa wa moyo: mafuta mengi ndani ya mwili wa binadamu
hujaa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita kirahisi hivyo moyo hutanuka
na kuongezeka ukubwa ili utengeneze presha kubwa ya kusukuma damu ndani ya
mishipa hiyo na dakika za mwisho moyo hushindwa kabisa kufanya kazi. Mgonjwa
huyu huhitaji dawa za kuusaidia moyo kufanya kazi kwa maisha yake yote na
ikitokea akaacha dawa, moyo unaweza kusimama na kusababisha kifo.
Vifo vya ghafla sana: ukichunguza watu wengi ambao wamekufa
ghafla ni wenye uzito uliopitiliza na watu hawa hufa usingizini na kukutwa
marehemu asubuhi, hii ni kwasababu unene husababisha hali Fulani inaitwa sleep
apnoea ambayo muhusika husimama kupumua kwa muda wakati amelala afu anendelea,
wakati mwingine kusimama kwa kupumua kunasababisha kifo kabisa.
kansa za aina mbalimbali; unene hufanya mwili kushindwa
kupambana na seli zinazosababisha kansa hivyo mtu hua kwenye hatari ya kupata
kansa ya figo, kansa ya kizazi, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya maini, kansa
ya tezi dume, kansa ya kongosho, kansa ya koo, kansa ya matiti, kansa ya mlango
wa uzazi na nyingine nyingi.
Kuishiwa nguvu za kiume kabisa; kuna kasumba za mtaani
wanasema wanaume wembamba wanajua sana kuridhisha wanawake…hii ni kweli kabisa
kwani wanaume wanene huchoka sana kwa shughuli ndogondogo na ikifika jioni huwa
hawawezi kufanya chochote lakini pia mafuta mengi kwenye mishipa ya damu
inayopeleka damu kwenye uume hufanya uume uishiwe nguvu kabisa hivyo matibabu ya nguvu za kiume kwa watu waha ni
kupunguza unene tu wala hakuna miujiza yeyote katika hili.
Ugumba kwa wanawake; unene husababisha homoni za wanawake
kutokua katika mfumo mzuri[unbalanced] na pia wanawake hawa hupata sana kansa
za mifuko ya uzazi yaani fibroids hali hii huweza kusababisha kutozaa kabisa.
Ni vizuri kama unaona unashindwa kupambana na unene wako uzae mapema kabla
mambo hayajawa mabaya zaidi.
Magonjwa ya jointi za miguu[osteoarthritis}; mwili hubeba
uzito kulingana na urefu wa mtu husika, mtu akiwa mnene sana jointi za mwili
hasa za miguuni[knee joints] huanza kuasagana na kusababisha maumivu makali mno
na mtu hushindwa kutembea kabisa..hali hii hutibiwa na dawa za maumivu kupunguza
makali lakini suluhisho la moja kwa moja la hali hii ni kupunguza uzito.
Presha ya damu; kama nilivyozungumzia kwenye tatizo la moyo
linavyoanza, pia kitu kilekile hutokea kwenye mishipa ya damu mafuta yanapokua
mengi.... yaani moyo hutumia nguvu nyingi kusukuma damu ili ifikie viungo vingine na
hapo ndipo presha ya damu inapoanza. Hakuna dawa ya kutibu kabisa tatizo hili
ila kuna dawa watu hupewa kupunguza presha na humezwa maisha yote.
Kiharusi[stroke]; hili ni tatizo linalotokea pale ambapo
damu inaingia kwa presha kubwa kichwani na kupasua mishipa ya ubongo au mishipa ya ubongo
inapoziba na mafuta..hii husababisha upande mmoja wa mwili wa binadamu kupoteza
uwezo wake wa kufanya kazi na hii huleta ulemavu wa muda mrefu sana, japokua watu
hawa kuna mazoezi wakifanyiwa huweza kurudi kwenye hali zao za kawaida.
Matatizo ya kijamii; aina ya maisha ya watu wanene hua
tofauti kidogo na watu wengine, watu
wanene hushindwa kujishirikisha kwenye shughuli za michezo, kucheza mziki,kuogelea
na hata kupata ubaguzi wakati mwingine
wakati wa kutafuta mpenzi au kazi..utafiti unaonesha asilimia arobaini na moja
ya wanaume huacha wanawake zao kwa sababu ya kunenepa na asilimia kumi na nne
ya wanawake huacha wanaume zao kwa sababu ya kunenepa.
Mwisho; unene na kitambi sio kuridhika au kawaida ya mtu
Fulani HAPANA kwani kuna uwezekano wa kupungua kwa asilimia mia moja kama
ukiamua kupunguza unene na kuna uwezekano wa wewe mwembamba kua mnene, kwani
vyote hivyo huchangiwa na aina ya maisha tunayoishi yaani ulaji wa chakula na
mazoezi.
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.0653095635\0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni