data:post.body Agosti 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HAYA NDIO MADHARA NANE YA KULA NYAMA.


                                                                              
Ukiangalia historia ya vitabu vitakatifu kama biblia, kabla ya gharika ya nuhu watu walikua hawaruhusiwi kula nyama kabisa,  ila waliruhusiwa kula matunda na mboga mboga za kondeni. Sidhani kama mungu aliwakataza kwa bahati mbaya kwani miaka ya sasa tafiti nyingi zinaonyesha watu wanaokula nyama  wanapata magonjwa mengi kuliko wale wasio kula na pia atu wasiokula nyama huishi muda mfupi kuliko wasiokula na hata kwenye historia ya biblia inaonekana watu wa zamani waliishi miaka mingi sana ukilinganisha na walioishi baada ya gharika yaani sisi.

Lakini hata hivyo historia inaonyesha kwamba hata kabla ya gharika la nuhu watu waliasi na kuanza kula nyama na baadae baada ya gharika mungu aliamua  kuruhusu kuliwa kwa baadhi ya nyama na kukataza baadhi ya nyama. Siku moja nilikua naongea na mchungaji mmoja msabato kuhusu sheria zao za kula nyama na vyakula mbalimbali nikagundua kwamba sio sababu za kibiblia tu kwani kuna vitu wasabato hawatumii vitu kama majani ya chai, soda za cocacola na kadhalika lakini kwa sababu za kiafya zaidi. Leo tutangalia  madhara ya kula nyama… lakini kabla ya kuangalia madhara ya nyama kuna makundi makuu mawili ya nyama yaani nyama  nyekundu na nyama nyeupe.Nyama nyekundu ni ile ambayo ina rangi nyekundu kabla ya kupikwa mfano nguruwe, ng’ombe,mbuzi, na wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne.Nyama nyeupe ni zile ambazo zina rangi nyeupe kabla ya kupikwa mfano kuku, bata, samaki, mbuni na wanyama wote wanaotembea kwa miguu miwili.

Utafiti unaonyesha ulaji wa nyama nyekundu una madhara makubwa sana kuliko ulaji wa nyama nyeupe hata hivyo watu ambao hawali nyama kabisa wako mbali sana na hatari hizi. Lakini kwa kua nyama pia ina faida katika miili yetu basi nyama nyeupe ni salama sana kuliko nyekundu.Hebu tuangalie madhara ya nyama kama ifuatavyo.

Hatari ya kupata magonjwa ya moyo: nyama ina kitu kinaitwa lehemu kitaalamu kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri..hii husababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwnye nyama ni hatari sana.[nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi]
Kansa ya utumbo mkubwa; nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara ya haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.
Ugonjwa wa kisukari; utafiti mpya umeonyesha kwamba watu wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo[cohort studies}… watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana  kuliko wale wasiokula.
Hatari ya kupata ugonjwa wa alzheirs disease;  huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza kumbukumbu kabisa. Wanasayansi wanaamini protini inayopatikana kwenye nyama kwa jina la Tau and beta-amyloid huharibu mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia kwa ugonjwa huu.
Ugonjwa wa kifafa; minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.
Unene uliopitiliza; nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe.unene  na kitambi ni hatari sana kwana husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.
Nyama tunazokula siku hizi sio nyama halisi tena; ukiangaliwa nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na hotel kubwa hapa Tanzania hapa namaanisha kuku sa kisasa, zinakuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji. Lakini kwasababu wamiliki wa biashara za nyama ni watu wenye fedha nyingi sana duniani ukweli huu hufichwa.
Magonjwa ya wanyama husika; miaka ya sasa dunia imekua inakumbwa sana na magonjwa ambayo yanashambulia wanyama. Yameua watu wengi na mengine hayatibiki kabisa. mfano mafua ya ndege, ugonjwa wa ukimwi ambao historia inasema ulitoka kwa kula nyama ya nyani wa porini, na ugonjwa wa ebola ambao virusi vyake huishi kwenye nyama wa popo.
Mwisho; nyama ya nyeupe yaani samaki, kuku, bata na ndege wengine wanaoruhusiwa kuliwa ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama mbuzi, ng’ombe, nguruwe na wengine ni hatari sana. Na kama wewe tayari una tazizo la moyo, presha, kisukari na kansa huu ni wakati sahihi wa kuacha kula nyama nyekundu kabisa kwani hizo nyama zitakupeleka kaburini.

                                           
                                                         STAY ALIVE 
                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                   MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                          
              
ZIFAHAMU SABABU KUU ZA WANAWAKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA NA MATIBABU YAKE…


                                                                      

Utafiti unaonyesha asilimia thelathini ya wanawake wenye umri wa kufanya mapenzi yaani kuanzia miaka 18 mpaka 59 wana tatizo la kuishiwa hamu ya kufanya tendo la ndoa  na hili  ndio tatizo lao kuu inapokuja wenye afya ya tendo la ndoa kitaalamu kama sexual health, hii ni moja ya sababu inayowafanya wanaume wengi wakimblie nje kulala na Malaya au wanawake wengine kwani wawanawake zao kila siku hutafuta sababu ya kutofanya tendo la ndoa.

Lakini tatizo hili ni tofauti kidogo kwa upande wa wanaume kwani ni vigumu sana mwanaume kukataa kufanya tendo la ndoa na pia wanaume  wanaweza kupata hamu kwa kutumia vidonge tu vya aina Fulani lakini wanawake inahitaji mchanganyiko wa njia mbalimbali ili kuweza kutatua tatizo lao yaani njia za ushauri wa kitaalamu na dawa pia wakati mwingine.
Zifautazo  ni sababu za kuishiwa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake…

Matatizo ya kisaikolojia;  linapokuja swala la tendo la ndoa amani ya moyo na uhuru wa kiakili unachangia sana mtu kupata hamu hata kufika kileleni lakini hali huu huweza kua na vikwazo kama  historia ya kulazimishwa kingono au kubakwa hapo kipindi cha nyuma, mawazo mengi hasa ya kazi, matatizo ya kifedha,kutojiamini na kuhisi labda maumbile yake mwanamke hayavutii, magonjwa ya akili na mgandamizo wa mawazo, mtizamo hasi kuhusu ngono kwamba anahisi ni unyanyasaji wa kijinsia na kadhalika.

Matatizo ya kimahusiano; sio rahisi kwa mwanamke kufanya mapenzi kwa mtu ambaye hana hisia naye hata kidogo labda kama anajiuza japokua wanaume wanaweza kufanya ngono na mtu yeyote hivyo shida yeyote  ambayo inaharibu hisia za mwanamke kwa mwanaume wake humfanya kose hamu kabisa ya kufanya ngono, mfano mawasiliano mabovu kati ya wapenzi, ugomvi kati ya wapenzi ambao haujapata suluhisho, kutoaminiana kati ya wapenzi na kuisha kabisa kwa hisia za mapenzi ambazo mwanzoni zilikuepo, ndoa ya muda mrefu sana pia huchosha kabisa linapokuja swala la tendo la ndoa.

Matatizo wakati wa ngono; kama mwanamke anasikia maumivu makali kipindi cha kufanya ngono hujikuta akipoteza hamu kabisa na hakuna siku moja ataweza kusikia hamu kabisa.

Matumizi ya dawa Fulani; baadhi ya dawa mfano dawa za kifafa, dawa za kupunguza mgandamizo wa mawazo na dawa za presha ya damu hupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa kiasi kikubwa.

Magonjwa; magonjwa mengi huchangia kuishiwa hamu ya kufanya tendo la ndoa mfano magonjwa yote yanayosababisha maumivu mfano maumivu makali ya joint, maumivu makali ya kifua, maumivu ya tumbo pia magonjwa ya mishipa ya fahamu, kisukari, ugonjwa wa presha na kadhalika
.
Uchovu: kufanya kazi nyingi na kurudi nyumbani usiku ukiwa umechoka, kazi ya kuwahudumia watoto kama kufua, vyombo, kupika na kadhalika huleta uchovu mwingi ambao hupoteza kabisa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Upasuaji; upasuaji wowote unaohusu matiti ya mwanamke  au sehemu zake za siri unaweza kuathiri kabisa uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa.

Tabia na maisha kwa ujumla; unywaji wa pombe uliopitiliza na uvutaji wa sigara huathiri uwezo na hamu ya kushiriki tendo la ndoa japokua unywaji wa wine kidogo kama glass moja huleta hamu ya kushiriki kingono.

mazoea ya kushiriki aina zingine za ngono;  kuna aina zingine za ngono ambazo si za kawaida mwanamke akishazoea inakua ngumu sana kuacha hata akiolewa inakua vigumu kushiriki ngono za kawaida mfano mazoea ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kufanya ngono na wanawake wenzake, kufanya ngono na mtu zaidi ya mmoja mfano threesome au foursome.

Ujauzito na kunyonyesha: hua kuna mabadiliko makubwa ya viwango vya homoni pale mwanamke anapobeba mimba na wakati wa kunyonyesha hii hupunguza hamu ya kufanya ngono kwa kiasi kikubwa sana.

Umri: kadri umri unavyozidi kwenda hamu ya kufanya ngono inazidi kupungua kwa wanawake na mwanamke anapofika miaka hamsini kitaalamu tunaita menopause homoni inayoitwa oestrogen hupungua sana na kumfanya awe na uke mkavu ambao hua na maumivu kipindi cha kushiriki ngono.

VIPIMO AMBAVYO HUFANYIKA
Kiwango cha homoni; kupima kuangalia kama homoni za uzazi ziko kwnye kiwango sahihi
Pelvic examination;hii hupimwa na daktari kuangalia kama kuna tatizo kwenye viungo vya uzazi vinavyochangia tatizo labda uke kua mdogo sana na kuleta maumivu, ukavu wa uke na magonjwa ya viungo vya uzazi yanayoweza kuleta maumivu kipindi cha tendo la ndoa.

MATIBABU
Ushauri;Kama nilivyosema mwanzoni kuishiwa hamu ya kufanya ngono kwa wanawake huletwa na sababu nyingi na matibabu yake hutegemea sana chanzo cha tatizo husika yaani chanzo kikitatuliwa mtu ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida. Mfano wanawake wenye matatizo ya kisaikolojia wanatakiwa wamuone mshauri aweze kuwasaidia kulingana na matatizo yao na kama kuna shida ya mahusiano kutafuta ufumbuzi wake.

Matumizi ya dawa za  homoni ; dawa za hormone zenye oestrogen peke yake au mchanganyiko wa oestrogen na progesterone husaidia sana  kuongeza mzunguko wa damu kwa wanawake wenye matatizo ya homoni lakini pia wale ambao umri umeenda kwani dawa hizi huongeza mzunguko wa damu kwenye sehemu za uke kupata hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Lakini pia cream za oestrogen na progesterone huweza kutumika pia kwa kupaka kwenye uke.

Matumizi ya virutubisho vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa: mmea wa multimaca ambao unapatikana huko marekani ya kusini umethibitisha kusaidia sana kutibu tatizo hili sugu na kwa sasa hapa nchini virutubisho hivyo vipo, na mimi binafsi nimesaidia wengi kupitia virutubisho hivyo, na kama wewe ni muhanga wa shida hii tunaweza kuwasiliana kutumia namba hapo chini ili uweze kupata matibabu mapema iwezekanavyo kuokoa ndoa yako au mahusianao yako.            

Matumizi ya mvinyo: mvinyo au wine ikitumika kwa kiasi kidogo labda glass moja au mbili huongeza msukumo wa damu kwenye kinembe cha mwanamke na kumletea hamu ya kufanya tendo la ndoa. Mfano amarula, red wine, white wine na kadhalika.

pata likizo na mapumziko; si rahisi kulala na mtu kitanda kimoja na mazingira yaleyale kwa zaidi ya miaka kumi bila kuchokana na hali hii huwatokea sana wana ndoa..hebu jaribuni kusafiri pamoja kubadilisha mazingira na kushiriki tendo la ndoa kwenye mazingira mapya wakati mwingine mwanamke aende kwa wazazi wake hata kwa wiki mbili mpaka tatu kwa mwaka kutembea ili mpate nafasi ya kukumkumbukana. 

MWISHO; mchanganyiko wa njia nilizotaja hapo juu zinaweza kusaidia sana kuliko kuchagua njia moja tu, hivyo unaweza ukatumia njia tofauti tofauti hapo ili kupata suluhisho la kudumu japokua virutubisho vya multimaca zimeonyesha uwezo wa hali ya juu ya kutibu tatizo hilo. kama uko kwenye mahusiano ambayo unajua kabisa moyo wako haupo hapo au hisia zimekwisha hasa kabla ya ndoa  ni bora kua muwazi tu na kuvunja mahusiano kuliko kuendelea  kudanganyana  kwani huko mbele ya safari itakua taabu zaidi na usiolewe kumridhisha mtu, olewa kwasababu hisia zako ziko pale kwa uhakika.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                           
                                                 STAY ALIVE
                           DR KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                    MAWASILIANO 0653095635\0769846183
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]HAYA NDIO MADHARA MAKUBWA YA VITAMBI NA UNENE..


                                                                                 
Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti kwamba zaidi ya watu milioni mbili a laki nane wanakufa kila mwaka sababu ya kua na uzito mkubwa kuliko kawaida na watu milioni thelathini na tano wanapata ulemavu sababu ya unene kila mwaka, ni kweli chakula ni muhmu kwa afya zetu lakini ulajia wa chakula uliopitiliza ni hatari sana na huweza kusababisha magonjwa yasiyotibika kabisa..
unene unaangilia mfumo mzima wa kazi za mwili wa binadamu na kusababisha hali hizo. Kama kawaida ni vizuri kama ukigundua una uzito ambao sio wa kawaida  kuanza kazi ya kuushusha mapema kabla hali haijawa mbaya zaidi,,, ukishaona una kitambi usijiulize mara mbili hayo ni mafuta tayari hivyo lazima uzito wako umezidi.. kawaida mwili wa mwanaume huhifadhi mafuta ya ziada tumboni na mwili wa mwanamke huhifadhi mafuta ya ziada kwenye makalio lakini mafuta yakizidi huweza kuhifadhiwa kote makalioni na tumboni…..yafuatayo ni madhara ya unene yanayobabisha vifo hivyo na ulemavu wa kudumu..
Ugonjwa wa kisukari; hii ni ugonjwa ambao mwili hushindwa kupambana na wingi wa sukari uliopo ndani ya mwili wa binadamu kutoka kwenye chakula anachokula kila siku na hii huweza kusababishwa kutotengenezwa kabisa kwa homoni ya insulin[diabetes type one] au homoni ya insulin kushindwa kuingia ndani ya cell nene[fat cell] ambazo huwepo mtu akiwa mnene sana. Ugonjwa huu unaathiri sana watu wazima kwanzia miaka arobaini kwani wengi wao hushindwa kupambana na uzito.ugonjwa huu unaweza kuanza bila mgonjwa kujua na kuja kujua kama anaumwa katika steji za mwisho ambapo wengi hukatwa miguu baada ya kupata vidonda visivyopona. Hakuna dawa ya kutibu kabisa ugonjwa huu ila kuna dawa za kusaidia kushusha sukari na hutumika kwa maisha  yote.
Ugonjwa wa moyo: mafuta mengi ndani ya mwili wa binadamu hujaa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita kirahisi hivyo moyo hutanuka na kuongezeka ukubwa ili utengeneze presha kubwa ya kusukuma damu ndani ya mishipa hiyo na dakika za mwisho moyo hushindwa kabisa  kufanya kazi. Mgonjwa huyu huhitaji dawa za kuusaidia moyo kufanya kazi kwa maisha yake yote na ikitokea akaacha dawa, moyo unaweza kusimama na kusababisha kifo.
Vifo vya ghafla sana: ukichunguza watu wengi ambao wamekufa ghafla ni wenye uzito uliopitiliza na watu hawa hufa usingizini na kukutwa marehemu asubuhi, hii ni kwasababu unene husababisha hali Fulani inaitwa sleep apnoea ambayo muhusika husimama kupumua kwa muda wakati amelala afu anendelea, wakati mwingine kusimama kwa kupumua kunasababisha kifo kabisa.
kansa za aina mbalimbali; unene hufanya mwili kushindwa kupambana na seli zinazosababisha kansa hivyo mtu hua kwenye hatari ya kupata kansa ya figo, kansa ya kizazi, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya maini, kansa ya tezi dume, kansa ya kongosho, kansa ya koo, kansa ya matiti, kansa ya mlango wa uzazi na nyingine nyingi.
Kuishiwa nguvu za kiume kabisa; kuna kasumba za mtaani wanasema wanaume wembamba wanajua sana kuridhisha wanawake…hii ni kweli kabisa kwani wanaume wanene huchoka sana kwa shughuli ndogondogo na ikifika jioni huwa hawawezi kufanya chochote lakini pia mafuta mengi kwenye mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume hufanya uume  uishiwe nguvu kabisa hivyo matibabu ya nguvu za kiume kwa watu waha ni kupunguza unene tu wala hakuna miujiza yeyote katika hili.
Ugumba kwa wanawake; unene husababisha homoni za wanawake kutokua katika mfumo mzuri[unbalanced] na pia wanawake hawa hupata sana kansa za mifuko ya uzazi yaani fibroids hali hii huweza kusababisha kutozaa kabisa. Ni vizuri kama unaona unashindwa kupambana na unene wako uzae mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
Magonjwa ya jointi za miguu[osteoarthritis}; mwili hubeba uzito kulingana na urefu wa mtu husika, mtu akiwa mnene sana jointi za mwili hasa za miguuni[knee joints] huanza kuasagana na kusababisha maumivu makali mno na mtu hushindwa kutembea kabisa..hali hii hutibiwa na dawa za maumivu kupunguza makali lakini suluhisho la moja kwa moja la hali hii ni kupunguza uzito.
Presha ya damu; kama nilivyozungumzia kwenye tatizo la moyo linavyoanza, pia kitu kilekile hutokea kwenye mishipa ya damu mafuta yanapokua mengi.... yaani moyo hutumia nguvu nyingi kusukuma damu ili ifikie viungo vingine na hapo ndipo presha ya damu inapoanza. Hakuna dawa ya kutibu kabisa tatizo hili ila kuna dawa watu hupewa kupunguza presha na humezwa maisha yote.
Kiharusi[stroke]; hili ni tatizo linalotokea pale ambapo damu inaingia kwa presha kubwa kichwani na kupasua mishipa ya ubongo au mishipa ya ubongo inapoziba na mafuta..hii husababisha upande mmoja wa mwili wa binadamu kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi na hii huleta ulemavu wa muda mrefu sana, japokua watu hawa kuna mazoezi wakifanyiwa huweza kurudi kwenye hali zao za kawaida.
Matatizo ya kijamii; aina ya maisha ya watu wanene hua tofauti kidogo na watu wengine,  watu wanene hushindwa kujishirikisha kwenye shughuli za michezo, kucheza mziki,kuogelea  na hata kupata ubaguzi wakati mwingine wakati wa kutafuta mpenzi au kazi..utafiti unaonesha asilimia arobaini na moja ya wanaume huacha wanawake zao kwa sababu ya kunenepa na asilimia kumi na nne ya wanawake huacha wanaume zao kwa sababu ya kunenepa.
Mwisho; unene na kitambi sio kuridhika au kawaida ya mtu Fulani HAPANA kwani kuna uwezekano wa kupungua kwa asilimia mia moja kama ukiamua kupunguza unene na kuna uwezekano wa wewe mwembamba kua mnene, kwani vyote hivyo huchangiwa na aina ya maisha tunayoishi yaani ulaji wa chakula na mazoezi.
                                                   STAY ALIVE

                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.0653095635\0769846183

JINSI YA KUPUNGUZA UZITO NA KITAMBI.


                                                                         
  
Huenda wewe msomaji umeshakata tama kabisa ya kupungua uzito baada ya kutumia njia mbalimbali bila mafanikio, lakini naomba nikupe matumaini kwamba swala la kupunguza uzito na kutoa kitambi linawezekana kabisa na sio gumu kama watu wanavyofikiria. Leo ntaenda kutoa elimu muhimu sana ambayo ukiifuata kwa makini utapungua uzito.
Kiukweli unene unatesa sana kimwili na kisaikolojia, yaani uchovu mara kwa mara, jamii inakuona tofauti sana na huenda hata kupata mpenzi ikawa ngumu kidogo, kukosa baadhi ya kazi na kushindwa hata kuvaa baadhi ya nguo kwa ajili ya unene lakini hebu tuyaache hayo tuongelee maada kuu.
Formula ya unene ni ndogo sana, ukila sana kuliko shughuli au mazoezi unayofanya unaongezeka uzito, ukila kidogo na kufanya mazoezi sana unapungua uzito, kiasi unachokula kikilingana na shughuli na mazoezi unayofanya unabaki kwenye uzito ule ule.
Kitaalamu chakula huchangia asilimia 70% kupungua uzito wakati mazoezi huchangia asilimia 30% na kazi ya mazoezi sio kukupunguza tu bali kukurudisha kwenye shepu.
Kwa maana nyingine kufanya mazoezi tu bila kuzingazia chakula hakuwezi kukusaidia kabisa.
Kupunguza uzito inatakiwa mtu ubadilishe MFUMO  wako wa maisha kabisa kama ifuatavyo.

Kuhusu ulaji wa chakula;
Epuka vyakula vya kukaanga sana na wanga; vyakula vinavyonenepesha ni vyakula vya wanga na mafuta kama ugali, wali,mihogo,viazi,chapati,maandazi na ngano zote,nyama ya mafuta kabisa,chips na kadhalika..vyakula hivi vinatakiwa viliwe sana na watu wanaofanya kazi ngumu kama wanaolima, kupasua mbao, kubeba mizigo na zingine ngumu kama kazi zako ni kushinda umekaa unatakiwa ule kidogo sana aina hii ya vyakula.yaani badala ya kula ugali mkubwa au wali mwingi na mboga kidogo unatakiwa ule ugali mdogo au wali kidogo na mboga nyingi kama maharage,mchicha,njegere,samaki,nyama ya kuku na kadhalika.
Kunywa maji mengi; hakikisha unakunywa maji mengi kama nusu lita au lita moja nusu saa kabla na nusu saa baada ya kula, hii itakufanya ujaze tumbo maji ujisikie kushiba na ule kidogo pia maji mengi kwa siku kama lita tatu yanasaidia mwili kuchoma mafuta  vizuri na kuondoa sumu mwilini.
Kula milo midogo midogo: utafiti umeonyesha ile milo mikubwa inayojaza tumbo ndio imafanya watu wanenepe sana na milo midogo midogo hata mara nne kwa siku inaongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta, hivyo epuka kula mpaka kulijaza tumbo kabisa, kula kawaida ukina umeshiba acha sio lazima chakula kiishe.
Kula ukiwa una njaa tu;epuka kula kwasababu eti muda umefika, kula ukiwa na njaa tu na ukiona njaa imekubana usiku kula vyakula ambavyo  ni laini  sana  mfano karoti mbichi, matunda, mboga za majani.
Epuka kushindaa njaa; watu wengi hushinda njaa wakidhani eti watapungua uzito , unaposhinda njaa mwili unadhani uko kwenye shida ya chakula hivyo ukila baadae mwili  unahifadhi mafuta mengi zaidi kwa matumizi ya baadae na watu wengi wanaoshinda njaa hula chakula kingi jioni na kuleta shida na hata hivyo huwezi kushinda njaa maisha yote hivyo kinachotakiwa ni kupata mfumo mpya wa maisha ili uuzoee.
Epuka kula kwenye sahani moja na watu wengine; ukila na watu huwezi kujua kiasi gani hua unakula hivyo ni rahisi sana kula chakula kingi bila kujua, hivyo pakua kwenye sahani yako ndogo{achana na sahani kubwa itakufanya upakue kingi] halafu kula peke yako.
Kula taratibu;  mishipa ya fahamu inachukua muda wa dakika 20 kutambua kama umeshiba baada ya kula,  hivyo ukila ndani ya dakika tano ukamaliza kula, utajikuta hujashiba kwasababu mishipa ya fahamu haijatoa taarifa kwenye ubongo lakini ukila kwa dakika ishirini taratibu chakula kilekile unachokula kila siku unaweza ukajikuta unakibakiza. Kula taratibu inaweza kua changamoto kidogo hivyo hakikisha unajipa kila siku muda wa kutosha wa kula yaani usile ukiwa na haraka unawahi sehemu. Lakini pia kama umezoea kula haraka utapata shida kula taratibu hivyo jaribu kufanya mambo mengine wakati unakula kama kutumia simu, kuangalia TV au kuongea na mtu huku ukiangalia saa yako.
Funga kula baadhi ya vyakula; simaanishi kushinda njaa hapana, unaweza ukawa unazitoa siku mbili au moja kwa wiki. Siku hizi kula matunda tu na mboga za majani na maji bila kula chakula kingine chochote, hii huumpa muda mwili wa kujisafisha sumu zote na kupungua uzito kirahisi zaidi.
Epuka vyakula vyenye sukari sana; acha kula biskuti,soda,keki,pipi,jojo, chai yenye sukari nyingi  na mengine mengi ambayo hayana msaada kwenye mwili kwani sukari ni moja ya chanzo kikuu cha unene mwilini na vyakula hivyo havina msaada mwilini zaidi ya kuongeza sumu. sukari hulazimisha mwili kutengeneza sana homoni kwa jina la insulini ambayo kazi yake sio kuvunja sukari tu bali na kuhifadhi mafuta pia.
Punguza unywaji wa pombe; pombe hasa bia ina ngano nyingi ambayo huongeza unene lakini hata pombe ambazo hazina ngano zina mchango ambao moja kwa moja kukunenepesha kwanza kwa kukufanya ule sana na ule vibaya yaani bila kufuata diet yako baada ya kulewa lakini pia maini yako hufanya kazi ya kuondoa pombe mwilini muda huo na kuacha kazi ya kuchoma mafuta hivyo usidanganyike kwamba pombe kali inapunguza uzito.
Punguza ulaji wa chumvi; weka chumvi kidogo sana kwenye chakula chako kwani chumvi huzuia maji yasitoke ndani ya mwili{kumbuka 60% ya binadamu ni maji tu].
Kua na msimamo: wewe ndio unajua unataka nini kwenye mwili wako, usiburuzwe kwenye vikao vya kula sana kwenye sherehe au kitu chochote na kama umeshakula sema umekula.
Piga mswaki baada ya kula mlo wa usiku; hii sio tu itatunza meno yako lakini pia itakufanya usipate hamu ya kula zaidi na mara kawaida ukishapiga mswaki hautakiwi kula tena, mbinu hii itakusaidia sana.
Pima uzito kila wiki; kama hujui maendeleo yako na hujui unataka ufikishe kilo ngapi bila mzani basi unapoteza muda, kua na mzani kutakufanya upate moyo wa kuendelea na mfumo wako wa maisha lakini hata ukipima mwisho wa wiki na kugundua hujapungua usife moyo endelea tu.
 mazoezi; sheria za afya zinasema kama mtu  anakula chakula mazoezi ni lazima, japokua mtu anaweza kupungua kwa chakula tu, mazoezi huweza kusaidia sana kupungua uzito.kufanya mazoezi hasa kwetu afrika ni kama adhabu kwa watu wengi lakini mazoezi ni muhimu sana. Kama kazini unaenda kwa mguu, baiskeli  au kazi zako ni za nguvu sana hii inaweza kua zoezi  tosha. Kulingana na hali ya maisha ya sasa kubana sana, kukosa muda wa kwenda gym au kushindwa kukimbia barabarani sababu ya pikipiki nyingi napendekeza utumie zoezi la kuruka kamba. Fanya hili zoezi nusu saa tu kwa siku ndani ya 3 au 4  kwa siku inatosha sana. Shida ya mazoezi sio kuanza bali kuendelea, wengi wenu mtaanza kwa fujo afu mtaacha. Fanya mazoezi kama sehemu ya maisha yako, ukifanya kidogo kila siku ni bora sana kuliko kufanya  kwa fujo siku moja  na kuacha.
Usikate tamaa; katika mafanikio yoyote ya binadamu sio unene tu hata mafanikio ya kifedha yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu.. wanaokata tama ndio hao kila siku hawafanikiwi, kama umeamua kufanya kitu, usifanye nusunusu fanya kwa akili yako yote na utafanikiwa. Hayo mambo niliyotaja hapo mwanzoni kuhusu chakula na mazoezi  yataonekana magumu mwanzoni lakini baaada ya muda mwili utazoea na wewe ndio utapata kilevi au addiction mwisho itakua ndio maisha yako mapya na vitambi utavisikia redioni. 

.
                                                     STAY ALIVE

                          DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
                                          0653095635\0769846183

                                       www.sirizaafyabora.info