Ugonjwa Kichaa cha mbwa kitalaamu kama rabies ni ugonjwa
unaopatikana nchi nyingi za Africa na bahati mbaya watu wengi hawaujui vizuri
ugonjwa huu na mara nyingi hata mtu aking’atwa na mnyama haoni kama ni tatizo
kubwa sana.
Ugonjwa wa kichaa cha umbwa ni ugonjwa unaoathiri wanyama wa
porini kama fisi na mbwa mwitu kutoka kwenye virusi viitwavo rabies lakini
wanyama hao huweza kuwajeruhi wanyama wa kufugwa kama mbwa, ngombe, paka na
kadhalika hivyo binadamu anaweza kupata ugonjwa huu kwa kujeruhiwa na wanyama hao
wa kufugwa kwani virusi vya ugonjwa huo hukaa kwenye mate ya mnyama husika..
Dalili za ugonjwa huu ni zipi?…Mgonjwa wa shida hii huweza kuonyesha
dalili zifuatazo..
Wasiwasi na kuchanganyikiwa..
Degedege
Kuona vitu ambavyowatu wengine hawavioni..
Kupooza kwa miguu
Kutoa mate mengi mdomoni
Kutokwa jasho sana.
Mgonjwa huanza kuogopa sana maji kwasababu ya maumivu makali
anayopata anapojaribu kunywa maji na pia hupata hali ya kubanwa sana kooni na
kushindwa kupumua na mwishoni mgonjwa hupoteza fahamu kabisa. Mara nyingi kifo
hutokea ndani ya siku kumi.
Utamjuaje mnyama aliathirika na ugonjwa huu?
Mnyama huanza kuonyesha tabia za ajabu, kung'ata mtu ghafla bila
kufoka, pia mda mwingi hujibanza ukutani.
Matibabu;
Ugonjwa huu hauna matibabu na ukishapata dalili hizo nilizotaja
hapo uwezekano wa kifo ni asilimia mia moja.Lakini ugonjwa huu unazuilika kwa
asilimia mia kwamba ukingatwa na mnyama katoe taarifa mapema kidonda kitibiwe
na uanzishiwe chanjo mara moja...
kwa maelezo zaidi soma hapa
SECRETS OF GOOD HEALTH
STAY
ALIVE….
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni