Utangulizi
Kila mtu anafahamu kuvuta sigara ni hatari, japokua kuna
watu wanaendelea kuvuta mpaka leo japokua wanafahamu madhara yake. Siwalaumu wavutaji
kwani kwangu ni wagonjwa kama wengine, yaani kuacha sigara sio rahisi kama
inavyofikiriwa…lakini kwanini uache sigara? Kwasababu itakuongezea urefu wa
maisha,kuishi maisha bora na kuwaongezea ubora wa maisha watu wanaokuzunguka.
kwanini ni ngumu kuacha?
Sigara ina kemikali iitwayo nicotine ambayo inapatikana
asilia kwenye tumbaku ambayo inasababisha mtu aliyeanza kuvuta sigara kushindwa
kuacha.{addiction].
Kemikali hii inasafiri haraka kwenda kwenye ubongo na
kufanya mtu apate hali ya kujisikia vizuri na kupunguza msongo wa mawazo. Lakini
hali hii ni ya muda kwani baada ya muda kemikali hii huisha mwilini na
kukufanya mvutaji utake sigara nyingine. Hali hii itakufanye uvute zaidi na
zaidi maishani mwako na kupata shida sana kuacha.
Lakini leo nina habari njema sana kwako wewe mvuta sigara
ambaye unatamani sana kuacha sigara lakini umeshindwa, njia zifuatazo
ukizifuata kwa bidii na nidhamu kubwa bila kukata tamaa nahuhakikishia siku moja
utapiga simu kunishukuru.
Jua kwanini unataka kuacha sigara: kama una sababu kuu ya
kuacha sigara itakupa moyo wa kuendelea kutovuta sigara mfano hutaki kupata
kansa ya mapafu, hutaki kupata magonjwa ya moyo, unataka kuilinda familia yako
na kuonekana kijana daima.
Usijaribu kuacha kimyakimya: zaidi ya asilimia tisini ya watu
waliojaribu kuacha sigara kimya kimya bila kutumia dawa yeyote au kupata sapoti
na ushauri wa kitaalamu walirudia sigara kwani kemikali hiyo ya nicotine ina
nguvu sana na iko nje ya uwezo wako na ukikaa bila kuipata utaitafuta tu sigara.
Punguza mgandamizo wa mawazo: sababu kubwa inayofanya watu
wengi wavute sigara ni mgandamizo wa mawazo yaani mtu anaona njia pekee ya
kutoa mawazo hayo ni sigara. Hebu jaribu kusikiliza mziki, tembelea fukwe za
bahari au ziwa na fanya mazoezi. Ni rahisi kufanya vitu hivi mwanzoni ukitaka kuacha sigara.
Usinywe pombe: pombe ni moja ya vitamanishi vikubwa vya kumfanya
mtu avute sigara hivyo usinywe pombe kabisa na kama umezoea baada ya kula
unavuta sigara basi jaribu kufanya mambo mengine kama kula jojo au pipi kifua au piga mswaki baada ya kula.
Usikate tamaa: mara nyingi mtu anaweza kuacha sigara mara
kadhaa na kurudi tena kwenye sigara baada ya muda mfupi. Usife moyo, watu wengi walioacha
sigara waliacha sigara kama mara nne au mara tano kabla ya kuacha kabisa. chamsingi uwe
na moyo wa kuendelea kuacha tena na tena na ukiona umerudia kaa ufikirie ni sababu gani ilikufanya urudi kwenye sigara ili ujipange upya.
Kula matunda na mboga za majani kwa wingi; utafiti
unaonyesha ulaji wa matunda kwa wingi na kupunguza vyakula vya nyama kwenye
chakula chako unafanya sigara ionekane ina ladha mbaya sana kwa mvutaji hivyo
humsaidia kuacha.
Usifanye peke yako: washirikishe ndugu, jamaa, mke, ,mme na marafiki
nia yako ya kuacha sigara kwani watakupa moyo na ushauri wao utakupa nguvu za
kuacha kabisa.
Safisha nyumba yako; ondoa vipande vyote vya sigara ndani ya
nyumba, fua nguo zote kwani ukiona kipande chochote kitakupa hamu ya kuendelea
kuvuta sigara tu… hata ukienda kwenye sherehe au disco kaa mbali namaeneo
ambayo yanakushawishi kuvuta sigara, itakua ni ngumu sana lakini vumilia ndio mafanikio yenyewe hayo.
Kaa mbali na marafiki wavuta sigara kwa muda; harufu ya moshi
wa sigara kwa mtu anayetaka kuacha ni sumu kali kwani inamfanya aitamani tena,
unaweza ukazushiwa maneneo mengi na marafiki zako kwamba umekua mtoto wa mama
na muoga lakini nakwambia kuvuta sigara sio ujanja kabisa ni upotezaji wa muda
na fedha.
Weka fedha zote amabazo ungenunua sigara; kama ulikua
unatumia sigara tano kwa siku basi weka shilingi elfu moja kwenye kopo kila
siku na ukiziona pesa zile utapata moyo kwamba sasa pesa yako unaikoa na
inafanya mambo mengine ya maana.
Jaribu dawa za kuacha sigara; kuna dawa zinapunguza kiu kali
ya kuvuta sigara baada ya kuacha na pia kupunguza dalili za ambazo mtu
anaziacha anapoacha sigara kama kutetemeka sana, mkandamizo wa mawazo na hasira
nyingi. Dawa hizi pia hufanya sigara uione sio suluhisho tena kwako. watu wengi wamefaikiwa kuacha kabisa kwa dawa hizi kwani kiu ya sigara ni kali mno na dawa hizi zinaipunguza sana.
Mfano wa dawa na dozi zake;
Bupropion tablets: hizi ni dawa zinasaidia kutibu matatizo
anayopata mtu baada ya kuvuta sigara ikiwemo kupata hamu kali ya sigara na
kutetemeka…dawa hii hufanya kazi vizuri kama ikitumika wiki moja mpaka mbili
kabla ya kuacha sigara.
Varenicline tablets; dawa hii pia huingilia mfumo wa ubongo
wa kutamani sigara sana wakati mtu ameacha na kumpunguzia mawazo hivyo kuacha
sigara kirahisi…dawa hii hutakiwa kutumika wiki moja kabla ya kuacha sigara.
Clonidine: hii ni dawa inayotumika kutibu tatizo la presha
ya kupanda imeonyesha mafanikio mazuri kwa kusaidia watu wanaotaka kuacha
sigara, hutakiwa kutumika siku tatu kabla ya kuacha sigara kabisa.. madhara ya
dawa hii ni kupunguza kasi ya moyo na kushusha presha ya damu hivyo ukianza
kutumia dawa hii lazima upime presha mara kwa mara kuangalia mwenendo wa presha yako.
Nortriptyline: hii hutumika siku 14 kabla ya kuacha kabisa
sigara hufanya kazi vizuri kuliko dawa zote zilizotajwa hapo juu na huendelea
kumezwa zaidi mpaka pale mgonjwa atakapokua tayari kuacha kabisa. Usiache ghafla
ila punguza dozi kwani ina madahara kiafya ikiachwa gafla.
Mwisho:njia zote nilizotaja hapo juu zitumike kwa njia moja
ama nyingine, watu wengine wanafikiri dawa ndio mkombozi wa kila kitu.. ni
kweli dawa hizo zinasaidia lakini usitegemee dawa pekee fuata na njia zingine
nilizoelekeza kwa matokeo mazuri zaidi. kwa maelezo zaidi soma hapa
SECRETS OF GOOD HEALTH
MAWASILIANO 0653095635\0769846183
DR.kalegamye hinyuye mlondo
DR.kalegamye hinyuye mlondo
STAY ALIVE.
0 maoni:
Chapisha Maoni