Magonjwa ya kurithi ni yapi?
Haya ni magonjwa ambayo yapo kwenye koo za watu fulani na
hurithiwa kutoka kizazi mpaka kizazi lakini pia magonjwa haya huweza kutoka kwa
mwanamke na mwanaume ambao kwa macho ni wazima kabisa na kuzaa watoto wenye
matatizo ya kiafya.
Kwenye jamii zetu za kiafrika ni jambo la kawaida sana kuzaa
tu bila kupima kujua kama kuna hatari ya kuzaa mtoto mwenye matatizo makubwa ya
kiafya kutokana na vimelea vya kurithi yaani DNA ambazo wazazi husika
wamezibeba, mimba nyingi zimekua zikisingiziwa kwamba hazikupangwa na wakati
kila mtu anajua mwisho wa ngono zembe bila njia yeyote ya uzazi wa mpango ni
mimba.
Hii ni tofauti na nchi zilizoendelea ambapo wazazi hupima
vipimo hivi kabla ya kuamua kuzaa na hata ikigundulika mtoto anayekuja atakua
na matatizo mimba hiyo hutolewa ili kuepusha maumivu ambayo mtoto huyo
angeyapata kama angezaliwa na maumivu ya kisaikolojia na kiuchumi ambayo wazazi
wanaozaa watoto kama hawa wanayapata, hii ni kwasababu ya kulazwa mara kwa mara
kwa mtoto husika na kushindwa kufanya kazi maisha yake yote.
Hivyo nchi zilizoendelea watoto wanaozaliwa na magonjwa ya
kurithi wametokomezwa kwa kiwango kikubwa sana tofauti na afrika ambapo watoto
hawa ni wengi sana na kila siku wanazidi kuzaliwa, wakati wangeweza kuzuilika
kama sisi wahusika na serikali ingechukua hatua kukomesha hili kwa kuingiza
vifaa vya kitaalamu ya kuyagundua magonjwa haya muhimu.
Ni kweli vipimo vingi havipatikani hasa maeneo ya vijijini
na hata mijini lakini kuna watu ambao wako kwenye nafasi kubwa ya kuzuia na
kupunguza idadi ya watoto hawa wanazaliwa kila siku, hasa watu wanaoishi mijini
na wenye uwezo kifedha lakini hata wewe ambaye huwezi kupata vipimo hivi hebu
jaribu kwenda ukweni kwa mumeo au mkeo unaweza ukaona ugonjwa wa kurithi ambao
sio wa kawaida huko na kufanya maamuzi vizuri au unaweza ukamuuliza mumeo au
mkeo ili awe muwazi kabla ya kufunga ndoa kwani magonjwa mengine yanaonekana
kwa macho tu.
Magonjwa haya ni kama yafuatayo…
Sickle cell disease;{siko seli] huu ni ugonjwa wa kurithi
ambao mtoto hurithi kutoka kwa baba na mama ambapo wazazi wawili ambao wanakua
hawana dalili yeyote hubeba ugonjwa huu kwenye damu zao yaani carrier na
wanakua na uwezekano wa 25% ya kumzaa mtoto huyu ambae ataugua na kua na dalili
zote za ugonjwa huu. Ugonjwa huu ni hatari sana. Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua
watu laki mmoja na elfu sabini na sita duniani kote wengi wakitokea Africa hasa
chini ya jangwa la sahara. Watoto hawa huanza na dalili za kuvimba vidole
wakiwa na umri wa miezi mitatu, kuvimba vichwa, kua na miguu na mikono mirefu
na miembamba, kulalamika maumivu makali, kuishiwa damu sana na kadhalika ukubwani. Kama wapenzi wakipimwa
wakakutwa wote wameubeba ugonjwa huu kwenye damu zao yaani carriers ni vizuri
wakaairisha ndoa hiyo kwani watakaribisha matatizo makubwa kwenye maisha yao.
Kama unataka kujua umebeba ugonjwa huu ukienda hospitali kubwa za rufaa wana
uwezo wa kuwapima na kujua. Ugonjwa huu pia unaweza kupimwa kwa kuchukua maji
kwenye tumbo la mama kabla hajazaliwa hivyo kuamua kuendelea na mimba au
kuitoa. Japokua kutoa ni kosa kisheria nchini Tanzania. Watoto hawa huishi kwa
mateso makali na 50% watakufa kabla ya miaka 40 kwa nchini kwetu Tanzania
hakuna data kamili za watu hawa lakini wasichana wengi wenye ugonjwa huu hufa
wanapoanza kuziona siku zao kwani damu hupungua zaidi na viungo vingi kushindwa
kazi.
Haemolytic diseases of the new born; kuna
aina kuu nne za group za damu yaani A, B, AB, na O ambazo group hizo mtu
anaweza kua positive au negative mfano mtu mwingine anaweza kua A positive na
mwingine akawa A negative au B positive
na mwingine B negative.Sasa swala ni kwamba watu wa negative wakioana hakuana
shida au watu wa positive wakioana hakuna shida LAKINI mwanaume wa positive
akioa mwanamke wa negative mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri lakini ataacha vitu
vinaitwa antibodies ambavyo kazi yake itakua ni kuharibu mimba zote
zitakazofuata kutoka kwa mwanaume huyu. Kipimo hichi ni rahisi sana na
kinapatikanakaribia hospitali zote Tanzania na hata kama mmeshaoana tayari na
mna tatizo hili kuna dawa maalumu inaitwa RHoGAM mama mjamzito anachomwa wiki
ya 28 mpaka 32 kuzuia vifo hivyo.
Albinism{Ualbino]: huu ni ugonjwa wa kurithi ambao motto
huzaliwa bila vimelea vya melanin au kua na uchache wa vimelea hivyo ambavyo
humfanya mtu apate rangi ya ngozi yake. Mara nyingi wazazi wote wawili wa mtoto
huyu hubeba ugonjwa huu kwenye miili yao bila kua na dalili yeyote na wao
kumzaa mtoto ambaye ni albino lakini pia kuna aina za ualbino ambazo mzazi
mmoja anaweza kusababisha albino kuzaliwa bila mama kua na vimelea vya
ualibino.Mtoto huyu huzaliwa akiwa na matatizo ya kutoona vizuri na makengeza,
ngozi na nywele nyeupe sana. Kua albino sio ugonjwa lakini watu hawa hua kwenye
hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kansa ya ngozi. Sio rahisi kupima kujua kama
mtu anabeba vimelea vya ualbino kwenye mwili wake lakini inawezekana kupima mtoto
aliyeko tumboni na kugundua kama nia albino au sio kwa nchi zilizoendelea au
unaweza kumjua mwenzako kwa kuona albino kadhaa kwenye ukoo wao.
Magonjwa ya akili: katika jamii kuna watu hua wanafanya vitu
ambavyo sio vya kawaida mpaka unajiuliza huyu mtu amechanganyikiwa au
vipi..yaani ni mtu wa fujo, hajifunzi kwa makosa ya nyuma, unasikia mtu kamuua
mzazi wake,anavunja sheria mara kwa mara, kunywa pombe sana, anakasirishwa na
vitu vidogo sana au maisha yake ya mahusiano yanakua ni ya ugomvi kila siku
yaani kwa kifupi anakua tofauti na wengine. Dalili hizi sio za kupuuzia kuna
uwezekano mkubwa sana wa kuzaa watoto wa aina hii ambao huanza kusumbua tangu
wakiwa shule ya msingi na kupata matatizo makubwa ukubwani. Shida hizi
hazihitaji vipimo ni wewe kutoa maamuzi mapema kabla hamjaamua kuzaa naye kwani
mambo hayo yanarithiwa na mimi nimeshashuhudia familia nzima ya watu waliokua
hawana akili nzuri yaani walikua wehu kabisa.
Magonjwa ya kansa; ugonjwa wa kansa haurithiwi lakini kuna
baadhi ya koo zina vimelea{genes] ambazo baadae husababisha kansa. Ni vizuri
kujua vyanzo vya vifo vya ndugu wa mwenza wako kabla ya kuamua kuzaa naye kwani
ugonjwa huu unaweza kua ni mbaya zaidi kuliko magonjwa yote ya kurithi. Kuna
familia naifahamu nyumba ilifungwa kwani watu wote waliuawa na kansa yaani mume
na watoto wote waliozaliwa, dada na kaka wote wa mume isipokua mke tu aliyekua
ameolewa pale.
Ugonjwa wa kisukari; ugonjwa huu yaani diabetes mellitus
type 2 unawapata sana wagonjwa watu wengia ambao kwao kuna ugonjwa huu. Yaani
kama baba yako na mama yako wana kisukari uwezekano wa wewe kupata kisukari ni
asilimia hamsini. Maana yangu ni kwamba ukioa au ukiolewa na mtu ambao kwao
kuna wagonjwa wa kisukari ujue kuna uwezekano wa mtoto wenu mmoja kuugua
ugonjwa huo miaka ya baadae. Hivyo hua tunashauri kama wazazi wako wana
kisukari kuepuka kua mnene kwani utakikaribisha mapema.
Ugonjwa wa asthma au pumu; ugonjwa huu ambao hushambulia
mfumo wa upumuaji hufuata sana ukoo fulani wa watu japokua pumu zipo za aina
mbili ile ya kurithiwa na ile ambayo sio ya kurithiwa hivyo kama ukoo unaoenda
kuoa au kuolewa una wagonjwa wawili au watatu wa asthma kuna uwezekano mkubwa
sana wa kumzaa mtoto mwenye pumu baadae, ugonjwa ambao huua haraka kama
usipopata ufuatiliaji wa kutosha.
Ugonjwa wa kifafa; japokua ugonjwa hu huweza kusababishwa na
magonjwa mengine kama homa ya uti wa mgongo, ulaji wa nyama ya nguruwe na
kadhalika ugonjwa huu umeonekana kufuata koo Fulani za watu yaani kama unaenda
kuoa kwenye ukoo ambao unafahamu kuna wagonjwa wa kifafa uwezekano wa kuzaa
watoto wenye kifafa upo hivyo ni vema kuingia unajua.
Umbilikimo: huu ni ugonjwa wa kurithi ambao watu wanazaliwa
sana kitaalamu unaitwa achondroplasia, wazazi wa watto hawa ambao hua na mikino
na miguu mifupi sana huweza kua kawaida kabisa lakini kutokana na kurithi
vimelea vya ugonjwa huu hujikuta wanamzaa mtoto huyu na mtoto huyu baada ya
muda Fulani akioa anazaa mtoto wa hiv hivi kwani mzazi mmoja tu huweza
kusababisha hali hii.
Magonjwa ya upofu; kuna koo ambazo watoto huzaliwa na
vimelea vya hali ambayo husababisha upofu baadae au ikasababisha upofu hata
kabla ya mtoto kufikisha miaka mitano. Mtoto huzaliwa na mtoto wa jicho
kitaalamu kama congenital cataract ambayo huziba jicho taratibu na baadae mtu
hataona kabisa na unaweza ukakuta ukoo una vipofu wengi na chanzo husika
hakifahamiki.
Mwisho; haya ni baadhi ya magonjwa tu ambayo labda yameathiri watu wengi kwenye jamii zetu lakini yapo mengine mengi ambayo siwezi kuyataja na makala hii haijaandikwa kuwatenga au kuwasema vibaya
watu wenye matatizo haya kwamba wasioe au wasiolewe lakini ni kujaribu kuongea
ukweli na kuepusha watu wenye tatizo moja kuzaa mtoto kwani ni kujiongezea
matatizo tu kama nilivyosema hapo mwanzoni na kuleta viumbe ambavyo vinakuja
duniani kuteseka sana. Ni bora waendelee kuzaliwa carriers yaan wanaobeba
vimelea bila kuugua kuliko kuendelea kuwazaa wagonjwa.hivyo kama wewe unajua kwenu kuna shida fulani ni bora kuzaa na mtu ambaye kwao hamna shida kabisa kwani ukizaa na mtu mwenye matatizo kwao pia ni hatari zaidi na kama ukiamua kukaidi na kuzaa hivyohivyo uzae unajua kwamba haya magonjwa yapo. niwape pole ambao tayari ni wagonjwa wa hali hizi na wale wenye ndugu wenye hali hizi.dunia inatambua maumivu yenu...kwa maelezo zaidi soma hapa
STAY ALIVE….
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni