Hali ya kichefuchefu na kutapika kipindi cha ujauzito
inatokea kwa asilimia 70 mpaka 85 ya
wajawazito wote hasa kipindi cha wiki 16 za mwanzoni, kwa jina lingine huitwa
homa za asubuhi na huanza asubuhi mapema na kupotea mchana au wakati mwingine
kuendelea mpaka jioni..
Kuna aina mbili za hali hii..
emesis gravidarum: aina hii mjamzito hujisikia kutapika na
kichefuchefu cha kawaida na huanza asubuhi na kupotea mida ya mchana..
hyperemesis gravidarum: hii ni aina kali ya hali hii ambapo mjamzito
hutapika sana hadi kuishiwa maji , kupungukiwa uzito na kuishiwa madini
mwilini.
Hyperemesis gravidarum hutokea kwa 0.5%-2% ya wajawazito wote hasa wiki ya nane mpaka wiki ya 12 ya kipindi cha ujauzito, hali hii hupotea mpaka wiki ya 20 ya ujauzito na kwa asilimia 10% ya wajawazito.
Sababu za hyperemesis gravidarum { hali ya kutapika na sana}
Chanzo maalumu cha hali hii hakifahamiki lakini kuna
mahusiano makubwa na kuongezeka homoni moja ambayo hutusaidia kujua kama mtu ni
mjamzito wakati akipima kwa kutumia kile kipimo cha mkojo yaani UPT..kuwepo kwa
wingi kwa homoni hii ndio chanzo kikubwa cha kupata kichefuchefu na kutapika
sana.
Homoni hizi huongezeka sana kwa wajawazito kwa hali zifuatazo..
Kubeba zaidi ya mtoto mmoja kwenye kizazi: wanawake
wanaobeba mapacha au watoto zaidi tumboni hutapika sana kuliko wengine wanaobeba mtoto
mmoja sababau ya kuongezeka sana kwa homoni hii.
Mimba zisizo za kawaida: wakati mwingine ukuaji wa mtoto
hutokea vibaya na nyama kubwa hukua tumboni badala ya mtoto kitaalamu kama
molar pregnancy.. halii hii hufanya mama mjamzito atapike sana.
Ukoo; familia zingine zinakua na hali hii kwa kurithi yaani
mama aliyepata hali hii watoto wake wa kike siku wakikua na kuzaa hua na hali
kama hiyo.
Magonjwa mengine: magonjwa kama kisukari cha kipindi cha
ujauzito huambatana na hali hii..
madhara ya hali hii kwa wajawazito..
Kutapika damu.
Kuishiwa maji mwilini.
Utapiamlo.
Kuishiwa madini mwilini..
Kuchanganyikiwa kutokana na kupotea kwa vitamin B1.{ Wernicke’s
encephalopathy}.
Kuathirika kisaikolojia.
madhara kwa mtoto aliyoko tumboni
Mimba kutoka.
Mtoto kuzaliwa kuzaliwa akiwa hajakomaa.
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo.
vipimo vinavyochukuliwa hospitali.
Kupima damu kuhakikisha hakuna malaria
Kupima mkojo kuhakikisha hakuna ugonjwa wa njia za mkojo
mfano UTI
Kupima ufanyaji kazi wa ini{liver function test} mara nyingi huongezeka
katika hali hii.
Kupima kiwango cha madini ya mwili
Kupiga picha ya ultrasound kuangalia hali ya mtoto tumboni..
MATIBABU YA TATIZO HILI…
Kama unasikia kichefu chefu kidogo na kutapika kawaida.
Kwanza unatakiwa ujue hali hii ni kawaida kwa wajawazito
wengi hivyo usiwe na wasiwasi sana.
Kunywa juice, maji au supu mara kwa mara itakusaidia
kuongeza maji na madini ya mwili.
Kula chakula kidogo kidogo chenye protini nyingi mfano
karanga, nyama, samaki,maharage.. epuka vyakula vya mafuta mengi vitakuongezea
tatizo.
Kama unasikia kichefuchefu na kutapika sana.
Kimbia hospitali haraka huko utaongezewa maji mwilini kwa
dripu, utapewa dawa za kuzuia kutapika na madini ya mwili kama vitamin B
complex.. kwa maelezo zaidi bofya hapa kusoma
STAY ALIVE
MAWASILIANO
0653095635/0769846183
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0 maoni:
Chapisha Maoni