data:post.body ZIFAHAMU KWA UNDANI DAWA ZILIZOTHIBITIKA KUTIBU TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI KWA WANAUME.[PRE MATURE EJACULATION} ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

ZIFAHAMU KWA UNDANI DAWA ZILIZOTHIBITIKA KUTIBU TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI KWA WANAUME.[PRE MATURE EJACULATION}                                                                                         

 
Tatizo la kuwahi kufika kileleni kwa wanaume ndani ya muda mfupi ndio linaloongoza kwa matatizo ya wanaume kitaalamu kama male sexual dysfuctions…tatizo hili linachukua asilimia 95% ya matatizo ya kiume katika kujamiina na kushindwa kuwafikisha wapenzi wao kileleni..naomba niseme tatizo la kuwahi kufika kileleni kwa wanaume sio ugonjwa kama wengi wanavyodhani ila ni hali ya kawaida kimaumbile yaani kama ufupi na urefu. huwezi ukajiita mgonjwa kwa sababu wewe ni mfupi lakini kwasababu ufupi watu hawaupendi ndio maana watu wanajitahidi kuvaa viatu virefu kila siku ili waonekane warefu… sawa na kuwahi kufika kileleni sio ugonjwa ila kwasababu unakufanya usimfikishe mwenzako kileleni inakua ni tatizo kwako lakini sio ugonjwa wewe ndio umeumbwa hivyo kwani kuna wengine hawana hilo tatizo.

Matibabu ya tatizo hili niliwahi kuzungumzia kwamba njia zinazoweza kukusaidia kapona kabisa tatizo hili ni njia za ambazo sio za dawa japokua dawa inakusaidia mwanzoni kama wewe unafika mapema mno, kama hukuona hiyo makala ya jinsi ya kujizuia isome hii hapa....KAMA WEWE MWANAUME UNA TATIZO LA KUFIKA KILELENI HARAKA KABLA MPENZI WAKO HAJARIDHIKA SOMA HAP
Lakini leo ntaenda kuzungumzia dawa ambazo zimethibitika kufanya hii kazi kwa kupunguza msisimko mkali na kufanya hata mtu aliyekua akienda kwa dakika moja kufika dakika kumi na moja na zaidi kama njia nilizotaja zilimshinda kutumia..

Watu wengi hudhani hawana nguvu za kiume kwasababu tu eti akishafika kileleni hawezi kuendelea, ngoja nikuibie siri moja..wanaume wote ukishafika kileleni mara ya kwanza lazima uume ulale yaani hiyo ni kawaida kabisa na ukisikia mtu anasema yeye hua anaunganisha bila kusinyaa kidogo huyo ni muongo mkubwa kwani hiyo ni hali ya kawaida wala sio ya kuogopa.

Tatizo ni nini?
 Watu wengi wanaona hii ni shida kwasababu anafika kileleni kabla mwenzake hajaridhika kisha akigundua mwanamke hajaridhika anapaniki na kutaka kujilazimisha kusimamisha uume  ndipo hali inazidi kua mbaya zaidi. Kitu cha msingi cha kujua ni kwamba usifike kileleni kabla mwenzako hajafika ila ukiona mwenzako kafika na ameridhika basi na wewe malizia ili mpuzike wote angalau kwa dakika kumi mpaka ishirini kabla ya kuendelea wote mkiwa mmeridhika. Hapo utafurahia maisha ya mapenzi lakini ukiwa unajiwahi kila siku kama kuku mpenzi utamuona mchungu.

HEBU TUZIANGALIE DAWA HIZI KWA MAKUNDI..

Dawa za ganzi za kupaka mfano lidocaine cream.
                                        

 hii ni dawa ya ngazi ambayo hupakwa sehemu zenye maumivu kupunguza maumivu..huko kwa wenzetu zipo nzuri sana ambazo wanazitumia wakati wa kujichora tattoo bila maumivu.
Dawa hii hupunguza msisimko mkali kwenye uume kwa kuleta ganzi kidogo na kufanya mtu achelewe kufika kileleni hata dakika 15 na zaidi.
Jinsi ya kutumia; paka kiasi cha lidocaine kwenye kichwa cha uume dakika kumi na tano mpaka nusu saa kabla ya kukutana na mpenzi wako hii itapunguza msisimko na kuchelewa sana kufika kileleni
.
Angalizo: Ukipaka dawa hii lazima uvae condom kwani ukiingia bila condom utamfanya na mwanamke apate hiyo ganzi kidogo achelewe kufika na mzigo mzito utakua juu yako.
Tube moja ya lidocaine cream kabisa inatosha kama kuanzia baada ya mwezi unaweza endelea na njia za asili nilizoonyesha kwenye link hapo juu au kuendelea na dawa mpaka utakapoona unaweza kuendelea bila dawa.

Dawa za kutibu mgandamizo mkubwa wa mawazo mfano paroxetine
                                                           

; dawa hizi hutumika sana kwa watu wenye msongo sana wa mawazo lakini zimegundulika kusaidia sana mtu kufika kileleni hadi dakika 15 saa na zaidi mfano paroxetine. Jinsi ya kutumia, meza kidonge kimoja cha paroxetine masaa manne mpaka sita kabla ya kukutana na mwanamke na utaona mabadiliko makubwa. Dawa hii haiihitaji kuvaa au kutovaa condom na vidonge 30 vinatosha kuanzia baada ya mwezi unaweza  endelea na njia asili nilizokunyesha kwenye link hapo juu au kuendelea na vidonge mpaka utakapoona uko vizuri bila vidonge.

Dawa za maumivu mfano vicodin;
                                   

Hizi ni dawa zinazotibu aina Fulani ya maumivu makali, utafiti ulofanyika umegundua kwamba pamoja na kutibu maumivu makali dawa hii ina uwezo wa kuzuia mtu kufika kileleni kwa zaidi ya dakika kumi na zaidi.
Matumizi yake; meza vidonge viwili vya vicodin masaa saa moja au mawili mpaka matatu kabla ya tendo la ndoa na itakuchukua mda mrefu sana kufika kileleni na utafurahia maisha yako ya kimahusiano na vidonge 50 vinatosha kabisa kama dozi ya kuanzia na  baada ya mwezi endelea na njia za asili nilizotaja kwenye hiyo link hapo juu au endelea na vidonge mpka utakapokua tayari na kuendelea bila vidonge.

Onyo; kama wewe ni mnywaji wa pombe usiguse kabisa dawa hii ni hatari ikichanganyikana na pombe huweza kuleta madhara makubwa sana ya kiafya ikiwemo kupoteza fahamu na degedege.

Mwisho: kama una dukuduku unaweza kuingia mtandaoni  google dawa hizo mfano ’paroxetine for pre mature ejaculation’ili ujiridhishe kabla ya kununua. Uzuri wa fani hii hakuna siri kila kitu kipo wazi na ukitaka unahakikisha mtandaoni.  dawa zote nilizotaja hapo juu zinapatikana kwenye maduka ya madawa na zimethibitishwa na madaktari bingwa wa fani hiyo kufanya hiyo kazi..  lakini dawa hizi ni adimu sana na ghali [sio chini ya elfu hamsini kwa dose ya kutosha mtu mmoja] kuzipata yaani unaweza usizipate kabisa lakini zipo. Lakini ukikosa kabisa wasiliana na sisi tunaweza kujua jinsi ya kukusaidia hata ukiwa mkoani..

Wakati mwingine sio kila dawa inafanya kazi kwa mtu Fulani, unaweza ukakuta dawa moja kati ya hizo ndio ikakufaa zaidi kuliko zote hivyo kama ukinunua moja isikufae vizuri jaribu nyingine.
Kumbuka dawa hizi hazitumiki milele na milele ni za muda tu hivyo nakushauri uzitumie huku unajiweka sawa na zile njia za asili nilizokuonyesha kwenye link hapo juu kwani ukiziweza  zile njia
umemaliza kazi. nakutakia maisha mapya baada ya somo hili.

                                                     STAY ALIVE

                       DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO.

                        MAWASILIANO 0653095635/0769846183

Maoni 2 :

  1. kwa wote wanahitaji namna ya kujikwamua kutoka katika kuangalia picha za ngono, masturbation na kurudisha uume na nguvu za kiume katika hali hakisi ya mwanzo kwa kutumia vyakula na ushauri, tuwasiliane kupitia ushaurinasaha18@gmail.com

    JibuFuta
  2. Dr hzo dawa upatikanaji wake upo kweli?

    JibuFuta