Japokua watu wengi
wanasema ‘’age is nothing but a number’ yaani miaka sio kitu ni nambari
tu ila hii huja tofauti kwa upande wa kubeba mimba na kuzaa.
Miaka ya zamani watu wengi walikua wanazaa kuanzia miaka 18
mpaka 25 wanakua wamemaliza uzazi kabisa na walizaliwa watoto wenye akili sana
kwa njia ya kawaida kuliko miaka ya sasa, lakini kwa sababu ya mambo ya kusoma
shule na ugumu wa maisha wanawake siku hizi hasa wasomi wanachelewa kuzaa hadi
miaka 35 mpaka 40 watu bado hawajamaliza mambo ya uzazi.
Lakini pamoja kua kusoma na kutafuta hela ni muhimu naomba nikukumbushe kwamba mambo
hayo yote yanatakiwa yaende sambamba na uzazi, ukijifanya uko bize sana na
shule na utafutaji wa maisha ujue ipo siku hizo hela zitaishia kwa madaktari wa
uzazi. Kwanini nasema hivi?
Hatari ya kua mgumba; uwezo wa kubeba mimba huanza kupungua
kwenye umri wa miaka 30 na unakua zaidi kwenye miaka 35 na kushindwa kabisa
kubeba mimba kwenye umri wa miaka 40, hata hivyo kansa za kizazi[uterine
fibroids] huongezeka sana kipindi hiki japokua kuna watu wachache sana ambao
wanabahatisha mimba wakiwa na miaka 40.
Hatari ya kutoka kwa mimba: wanawake wengi wanaharibikiwa na
mimba au mimba kutunga nje ya uzazi baada ya miak 30, hii ni kutokana na
kupungua kwa nguvu za mlango wa uzazi, misuli ya kizazi na homoni za uzazi na mpangilio mbovu wa chromosome za mayai.
Uwezekano wa kubeba kuzaa mtoto mwenye mapungufu ya kimwili
na kiakili; mfano ugonjwa wa down syndrome ambao mtoto yai lilirutubishwa
hujikuta na chromosome 47 badala ya 46 ambazo ndio kawaida. Mtoto wa hivi hua
na upungufu wa akili na kushindwa kukua, wengi wao hufa mapema na wengine
kuishi kwa mda wa miaka michache.
hatari ya kuzaa kwa upasuaji na kifo cha mama na mtoto: vifo vya akina mama na
watoto huongezeka mara dufu pale mama anapobeba mimba zaidi ya miaka thelathini
kutokana na kupungua uwezo wa kusukuma mtoto na wakati mwingine kuhitaji kuzaa
kwa uparesheni kuliko angezaa kipindi cha miaka ya ishirini.
Magonjwa ya umri; kila
mtu anafahamu kwamba miaka inavyozidi kwenda mbele kila mtu anakua kwenye
hatari ya kupata magonjwa yasiyotibika kama kisukari, magonjwa ya moyo na
presha ambayo huathiri sana ujauzito kwa hatari ya kubeba mtoto mwenye kilo
nyingi ambaye atahitaji upasuaji na pia hatari kubwa ya kifafa cha mimba.
Itakuchukua mda mrefu sana kubeba mimba; kipindi hichi mayai
yanatoka mara chache sana kutoka kwenye ovari kama yanavyotakiwa kutoka kila
mwezi wakati ukiwa kwenye umri wa miaka ya ishirini na.. hivyo utatakiwa
kuonana na daktari bingwa wa uzazi kuweza kufuatilia mzunguko wako ili kubeba
mimba.
Kushindwa kumuhudumia mtoto vizuri; ukizaa mtoto ukiwa na miaka arobaini, ukifika miaka hamsini atakua na miaka kumi. Miaka hamsini
kwa nchi zetu za kiafrika unakua umebakiza miaka michache sana ya kuishi huenda
ukafa mtoto akiwa hajaanza hata sekondari. Hii inaathiri wazazi wote yaani wa
kike na wa kiume.
Ushauri; kama una miaka zaidi ya thelathini na unategemea
kupata mtoto, ukibeba mimba hakikisha unafanya mahudhurio mazuri ya clinic na
kuonana na daktari mara kwa mara ili akusaidie kufuatilia maendeleo ya mtoto
kabla hajazaliwa lakini ujue uko kwenye hatari kubwa. Kama ndio kwanza uko
kwenye miaka ya ishirini hakikisha umemaliza uzazi kabla ya miaka 30 na utapata
watoto bora zaidi.
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
STAY ALIVE
0 maoni:
Chapisha Maoni