Unaweza ukahisi ni maigizo au stori za kusadikika lakini kwa
mara ya kwanza mwaka 2008, daktari gero hutter
alimfanyia oparesheni mgonjwa
timothy ray brown ya kubadilisha vimelea
vya mifupa vinavyotengeneza damu mwilini kitaalamu kama bone marrow baada ya
kuugua kansa ya damu kwa mda mrefu {leukemia] pamoja na ukimwikwa pamoja , mgonjwa huyo alipata bone
marrow zingine kutoka kwa baadhi ya watu ambao kinga zao za mwil zimeonyesha
kukataa kabisa maambukizi ya ukimwi yaani hawawezi kuambukizwa hata iweje.
Tangu mwaka 1990 wanasayansi wamegundua watu wa kaskazini
mwa ulaya ambao kinga za mwili zimekataa kabisa maambukizi ya ukimwi.
Mgonjwa huyo aliishangaza dunia baada ya kukutwa hana virusi
vya ukimwi hata kidogo kwenye damu yake baada ya upasuaji huo, madaktari waliokua wakimuhudumia
walihisi labda virusi wanaweza kua wamejificha kwenye ubongo, maini, na sehemu
zingine za mwilini hivyo walichukua sehemu za maeneo hayo kupima{biopsy} lakini
hawakukuta kirusi hata kimoja.
“matokeo yanaonyesha mgonjwa huyu amepona ukimwi kabisa’ jarida la journal blood liliandika…. “kwa
matokeo haya naweza kusema tumefanikiwa kutibu ukimwi kwa mara ya kwanza
duniani” liliongezea jarida hilo.
Lakini njia hiyo haiwezi kuwatibu ukimwi watu wengine kwani
ni hatari sana na uwezekano wa kufa wakati wa uparesheni hiyo ni asilimia
ishirini, na oparesheni ililenga kutibu kansa na sio ukimwi hivyo madaktari duniani walikataa njia hiyo ambayo kama ingetumika
kwa wagonjwa wote huenda ukimwi ungetokomea kabisa duniani.
Mpaka sasa hivi waathirika wa ukimwi duniani ni milioni 33
na ugonjwa huu umeua watu zaidi ya milioni 25 tangu ulipogunduliwa miaka ya 1980.
Ni dawa za ARV tu ndio zinawasaidia kurefusha maisha lakini hakuna chanjo ya ugonjwa
huu mpaka sasa.
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
STAY ALIVE
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635\0769846183
Chapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
JibuFuta