Niliwahi kuongelea jinsi ya kuhesabu siku za hatari kwa
mizunguko ya siku 28 kwa wale ambao mizunguko yao haibadiliki kwenye makala
za nyuma kama hukuiona makala hiyo soma hii hapa na ujifunze jinsi ya kuhesabu mzunguko
lakini kuna watu wengi ambao mizunguko yao ya
miezi inatofautiana sana, labda mwezi huu siku 27 mwezi ujao siku 30.
Kama mizunguko inatofautiana kama nilivyoongea hapo juu,
kama kawaida unatakiwa uangalie mzunguko wako kwa miezi sita ili uweze kujua
mzunguko mrefu zaidi na mzunguko mfupi zaidi. Mfano mwezi wa kwanza mzunguko
siku 30, mwezi wa pili mzunguko siku 32, mwezi wa tatu mzunguko siku 27, mwezi wa
nne mzunguko siku 28, mwezi wa tano mzunguko siku 32, mwezi wa sita mzunguko
siku 29.
Kwa mizunguko hiyo, mzunguko mrefu kuliko yote ni siku 32 na
mzunguko mfupi kuliko yote ni siku 27. Kupata siku zako za hatari….
Mzunguko mrefu siku 32 toa 10 unapata 22.
Mzunguko mfupi siku 27 unatoa na 18 unapata 9.
Hivyo siku zako za hatari ni siku ya 9 mpaka siku ya 22 ya
mwezi husika zilizobaki ni salama.
Hizo namba za kutoa yaani 10 na 18 ni costant yaani hazibadiliki ,
tumia kama zilivyo.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
STAY ALIVE
Kwa mfano unakuta mwezi huu umeziona tarehe 5 mwezi mwingine25
JibuFutaNaomba jibu
JibuFuta