Baada ya kuhudumia na kushauri wagonjwa wengi kupitia
mawasiliano ya mtandao wa internet na simu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kwa mafanikio makubwa,
kikundi cha madaktari wa siri za afya bora kwa mara ya kwanza sasa kinakuletea
wewe msomaji huduma hii mpya ambayo kwa sasa imekua na kupata umaarufu nchi
zilizoendelea sana kama marekani, uingereza, Canada, Australia na nyingine
nyingi, hii imesababishwa na uhaba wa madaktari kwenye nchi nyingi duniani
ambao kwa nchi zetu za kimasikini hali ni mbaya zaidi.
Kulingana na uhaba mkubwa wa madaktari nchini Tanzania inaonyesha
kwamba daktari mmoja nchini Tanzania anahudumia wagonjwa elfu hamsini yaani kwa
maana hii zaidi ya wananchi milioni ishirini watakufa bila kumuona daktari
kabisa nchini Tanzania, hivyo tunaamini huduma hii itawapunguzia makali
wananchi wa Tanzania.
Huduma hii ikoje?
Badala ya kwenda hospitali na kupanga foleni sasa unaweza
ukatuma meseji, kutuma email au kupiga simu na kuongea na daktari moja kwa moja
mara tu unapo ugua. Hapo utaeleza dalili zako zinazokusumbua na daktari
atakuuliza maswali muhimu kulingana na tatizo lako kisha atakuelekeza vipimo
vya kwenda kupima maabara ya karibu [kama kuna ulazima] kisha utamsomea majibu
na utalekezwe dawa gani za kwenda kununua na ushauri wa ziada kama utakuwa na
maswali zaidi au kama una tatizo lolote linalohitaji ushauri wa kitaalamu pia
utaongea na dokta akuelekeze mahali pakuanzia.
hizi ndio faida kumi za huduma hii....
Haipotezi mda: siku hizi ukiugua unaweza kujikuta unamaliza
siku nzima hospitali na shughuli zako zingine zikakwama lakini kwa huduma hii unaweza
ukaendelea na shughuli zako huku ukipata matibabu.
Huokoa maisha: unaweza kua na tatizo ambalo linahitaji
kwenda haraka kwenye hospitali ya rufaa mfano saratani, ugonjwa wa moyo,
ugonjwa wa figo, maini na kadhalika hivyo badala ya kwenda kuhangaika kwenye
zahanati ndogo ndogo daktari anaweza kukushauri uwahi mapema kwenye hospitali
kubwa.
Hupunguza gharama ya matibabu: gharama ambayo ungeitumia kwa
nauli kwenda hospitali na kurudi, kutoa rushwa kidogo, gharama za kumuona
daktari ili uweze kuhudumiwa sasa unaweza ukakaa ndani tu na kuhudumiwa vizuri
bila shida yeyote kwa gharama ndogo sana.
Hukupa mda wa kujieleza kila kitu; kama tunavyofahamu
hospitali zetu, unaweza ukaanza kuongea na daktari lakini kabla hujamaliza na
kuuliza maswali anakupa cheti uondoke, lakini kwa huduma hii utaweza kuuliza
swali lolote unalotaka na kuridhika kwa siku hiyo ambayo utakua unaumwa.
Daktari anaweza kuona kwa macho tatizo lako: kukua kwa
teknolojia kumesaidia mambo mengi, kwani unaweza ukapiga picha ya tatizo
ulilonalo kama ugonjwa wa ngozi, kidonda na kadhalika kisha ukatuma kwa watsapp
na ukapatiwa jibu lako hapo hapo na kama kuna utata utapewa utaambiwa uende
hospitali mapema kwani sisi sio waganga wa kienyeji, hatung’ang’anii wagonjwa.
Huduma masaa 24; huduma hii itakufanya uweze kuongea na
daktari muda wowote ata kama masaa ya kwenda hospitalini yameisha na kupata huduma
nzuri kwani hospitali zetu nyingi saa tisa zinakua zimefungwa tayari, nahii inawagusa
sana watu wanaofanya kazi siku nzima na kurudi usiku.
Matibabu ni siri sana; kama wewe ni mmoja watu wanao ogopa
kwenda hospitali kwa kuhofia siri zao kufichuka sasa utaongea na daktari
usiyemfahamu wala hakufahamu na maelezo yako yote yatakua ni siri pia unaweza
kuuliza swali lolote la dawa unazotumia za magonjwa yeyote.
Ni nzuri kuliko kujitibu mwenyewe: hebu fikiria ni mara
ngapi umekua ukitafuta google dalili fulani fulani zinazokusumbua ili uweze
kujitibu na bado hupati jibu la uhakika? lakini kwa huduma hii na utapata ugonjwa
unaokusumbua hapo hapo na kupata matibabu yake.
Haina mipaka: huduma hii itaweza kukupa nafasi ya kuongea na
daktari aliyoko dar es laam au arusha wakati wewe ukiwa mtwara au kigoma pia
itaweza kukuunganisha na madaktari bingwa wa vitengo mbali mbali ambao huwezi
kupata huduma zao kwa sehemu ulipo.
Ni huduma bora na ya kisasa; kwa huduma hii utaweza kutibiwa
kwa dawa mpya na za kisasa kwani daktari anaweza kukwambia ukanunue dawa Fulani
nzuri ambayo hujawahi kuitumia na kukusaidia sana kwa tatizo lako la kiafya.
Jinsi ya kupata huduma..
Ili kupata huduma hii utachangia kiasi cha shilingi elfu
mbili za kitanzania kupitia tigo pesa au m pesa 0653095635/0769846183 kisha utapiga au kutuma meseji kati ya namba kati ya hizi
hizi na kueleza matatizo yako na utahudumiwa haraka
iwezekanavyo kwa njia ya simu au meseji muda wowote ule na daktari moja kwa
moja. pia kama una mgonjwa wako nyumbani kwa wale wanaoishi dar es laam tunaweza kuja kumuona, pia na huduma ya daktari wa familia inapatikana lakini kwa gharama tofauti kidogo kulingana na eneo uliopo. Kumbuka gharama hii itakua ya siku nzima ya siku utakayolipia hata kama
una matatizo zaidi ya kumi lakini haitahusika na matibabu ya siku zingine.
Mwisho tunakukaribisha kwenye hospitali hii inayotembea
ambayo tunaamini itaboresha afya yako kwa kiasi kikubwa sana.bofya maneno ya kijani kusoma zaidi
SECRETS OF GOOD HEALTH
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO
0653095635/0769846183
MAWASILIANO
0653095635/0769846183
STAY ALIVE......
0 maoni:
Chapisha Maoni