Kifungua kinywa ni nini? Hichi ni chakula kinacholiwa
asubuhi mara nyingi kabla watu hawajaanza mizunguko ya kila siku.
Lakini kuna watu kwao imekua utaratibu kutokunywa chai kwa
kusingizia ugumu wa maisha, kua bize sana, au kutozoea kunywa chai asubuhi.
Tabia hii ya kutotumia kifungua kinywa inaambatana na
madhara hatari ya kiafya na kimahusiano na watu wanaokuzunguka…hebu angalia
madhara haya makuu yakutokunywa chai.
Kuongezeka uzito na kua mnene: watu wengi wanajidanganya kwa
kuacha kunywa chai asubuhi wakidhani wanapunguza uzito lakini wanaongezeka
uzito zaidi kwa sababu kuu mbili, kwanza watakula chakula kingi baadae njaa
ikiwa kali sana kwa kudokoa dokoa wakati wa kazi, wakati chakula hicho
wangekila asubuhi kabla ya kazi kingetumika vizuri na mwili kushusha uzito. Sababu
ya pili ni kwamba unaposhinda njaa mwili unahisi kwamba uko kwenye shida ya
chakula hivyo chakula kingi utakachokula baadae mwili unakiweka kama mafuta
kisije kutumika baadae shida ya chakula ikizidi.
Mzunguko wa hedhi usioleweka: gazeti moja nchini marekani
kwa jina la appetite lilifanya utafiti na kugundua wanafunzi wengi wa chuo
ambao hawanywi chai asubuhi husumbuliwa sana na maumivu kipindi cha siku zao,
kukosa hedhi kabisa, lakini pia walisumbuliwa na kupata choo ngumu.
Kuwa na hasira sana: hili liko wazi watu wengi wakiwa na
njaa wanakua na hasira sana na wanaweza kutaniwa kidogo tu na kua wakali sana,
hii inasababishwa na msongo wa mawazo wanaoupata kipindi hiki na mwili kutoa
aina ya homoni inayoitwa adrenaline inayomfanya mtu awe na hasira zaidi.
Kushindwa kufanya kazi kwa umakini; mtu asipokunywa chai asubuhi kuna muda unafika
hawezi kufanya kazi kwa makini kwaani ubongo unakua umepungukiwa nguvu yaani
glucose hivyo huanza kutokwa jasho na kutetemeka sana.
Mwisho: napenda kuwashauri wapunguza uzito wote ambao
mmeachwa kuchwa chai mkidhani mtapungua kwamba mnajidnganya, hakuna kitu kama
hicho.. njia pekee ya kupunguza uzito ni kula chakula kidogo kila mlo hata mara
sita kwa siku hii hufanya mwili
kufanyakazi haraka na kupunguza uzito{metabolism} kuliko kuruka mlo na kulipa
kisasi jioni au kula milo mikubwa ya nguvu..tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
STAY ALIVE
DR .KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO
DR .KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO
0769846183/0653095635....
0 maoni:
Chapisha Maoni