Kufanya ngono kinyume cha maumbile ni nini?
Hii ni aina ya ngono ambayo mwanamke au mwanaume anaingiziwa
uume mkunduni {samahani kwa ukali wa hili jina]…
Tangu kuanza kwa karne ya 21 swala la kuingiliana kinyume na
maumbile limekua la kawaida sana hata kwa wapenzi wa kawaida yaani msichana na
mvulana, japokua zamani kidogo ilikua ni kwa mashoga tu.
Tabia hii Imesababishwa hasa na video za ngono za nje ambazo
nyingi huonesha ngono hii kama ni ya kawaida na wala haina maumivu lakini ukweli ni kwamba hii sio ngono ya kawaida na huambatana na maumivu makali....utafiti
uliofanyika uingereza imegundulika zaidi ya asilimia thelathini ya wapenzi wa
kawaida wanashiriki aina hii ya ngono.
Lakini pia kumekua na hadithi za uongo hapa nchini kwamba
mwanamke akishiriki aina hii ya ngono basi anaongezeka makalio kitu ambacho sio
kweli kabisa.
Leo ntaongelea madhara makuu ya kushiriki aina hii ya ngono..
Kulegea kwa misuli ya mkundu; mkundu una misuli maalumu
ambayo hubana kinyesi kisitoke wakati umebanwa mpaka utakapofika chooni, lakini
tabia hii hulegeza sana misuli hii na kushindwa kujizuia pale unapokua umebanwa
na kuweza kuadhirika wakati mwingine.
Kansa ya mkundu; virusi maarufu kwa jina la human papilloma
virus wanaopatikana kwenye eneo la mlango wa uzazi huweza kuambukizwa na kwenda
kwenye mkundu na kusababisha kansa ya mkundu. Mashoga wengi wana hatari ya
kupata kansa hii mara kumi zaidi ya wanaume wa kawaida.
Maambukizi ya virusi vya ukimwi: mkundu hauna maji ya
kulainisha njia wakati wa kufanya ngono hivyo hatari ya maambukizi ya ukimwi ni
mara kumi zaidi kuliko mtu anayefanya ngono ya ukeni, hivyo kuendelea kushiriki
ni kuendelea kujihatarisha.
Magonjwa ya njia ya mkojo: tabia ya kuhamisha uume kutoka
kwenye mkundu kwenda kwenye uke husambaza bakteria ambao huweza kupita kwenye
tundu la mkojo na kushambulia kibofu cha mkojo na figo.
Magonjwa ya zinaa; kama zilivyokua aina za ngono zingine,
aina hii huambatana na magonjwa kama kaswende, gonorhoea, na mengine mengi..
Fistula: vidonda visivyouma {ulcers} ambavyo husababishwa na
tabia hii huweza kuleta tundu kati ya uke na mkundu au uke na kibofu cha mkojo,
hali ambayo husababisha choo kubwa kutokea kwenye njia ya uke na mkojo kutoka bila
kuzuilika.
Hemorrhoids: hii ni mishipa ya damu inayovimba mkunduni na
kuleta shida wakati wa kujisaidia haja kubwa, huweza kutibiwa na dawa lakini
upasuaji huhitajika kama dawa zikishindwa{hemorrhoidoctomy}.
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
NAKUTAKIA AFYA BORA WEWE NA FAMILIA YAKO..
Mawasiliano 0653095635/0769846183
STAY ALIVE…..
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]
Je nini hasa madhara anayopata mwanaume anayeingiliwa kinyume na maumbile?
JibuFutamkuu hayo niliyoandika hapo juu ni madhara, unataka nini zaidi?
JibuFuta