data:post.body JINSI YA KUZUIA VIRUSI VYA UKIMWI NDANI YA MASAA 72 BAADA YA KUHISI UMEAMBUKIZWA.{P.E.P] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JINSI YA KUZUIA VIRUSI VYA UKIMWI NDANI YA MASAA 72 BAADA YA KUHISI UMEAMBUKIZWA.{P.E.P]


                                                                                         
Kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kumeendelea kuwaweka mahali pagumu sana watumishi wa afya kwani siku za usoni wengi wao wataambukizwa na kufa kwa ukimwi kutokana na kazi yao ya kushika damu mda mwingi  wakati wa kazi.. wengi wao hujikata na nyembe za kufanyia upasuaji, kujichoma sindano na kugusa damu kwenye ngozi wakati wanawahudumia wagonjwa wa aina mbalimbali ambao wanaenda kutibiwa kwenye vituo vya afya, mimi mwenyewe nimeshuhudia madaktari wakijichoma au kujikata na nyembe wakati wakifanya uparesheni kubwa kwa watu ambao inafahamika kabisa wameathirika.

  Miaka ya hivi karibuni kuna tumaini kwa watumishi hawa na watu wengine ambao wako nje ya sekta ya afya kujizuia na virusi vya ukimwi baada ya kugundulika dawa za ARV’s ambazo sio tu zinapunguza makali ya virusi vya ukimwi ila vina uwezo wa kuzuia ukimwi kama ukivitumia masaa 72 au siku tatu baada ya kuhisi kuambukizwa. 

Namaanisha nini naposema kuhisi kuambukizwa?
kujichoma na sindano au wembe wakati unahudumia mgonjwa muathirika.
kubakwa na mtu ambaye afya yake haifahamiki.
kufanya ngono na mtu bila kinga kisha ikathibitishwa kwamba mtu huyo uliye lala naye  ni muathirika.
                                                                                                                 
Nini cha kufanya?
Nenda kituo chochote cha afya au hospital ya serikali na waelezee kilichotokea ndani ya masaa 72 baada ya ajali hiyo, kwanza watakupima kujua afya yako na kama ni muathirika tayari wa siku nyingi hautapewa dawa hiyo ila utaanza ushauri ili uanze matibabu{ kama ukiambukizwa leo vipimo huonyesha baada ya miezi mitatu] na kama bado hujaathirika utapewa dawa hzo uzitumie kwa mwezi mmoja{LAMIVUDINE, ZIDOVUDINE na NIVERAPINE} ambazo zitakukinga kwa asilimia mia moja kwa kuzuia virusi kushindwa kuingia ndani ya seli na kuzaliana. kumbuka masaa 72 yakipita dawa hii haitafanya kazi yeyote.. Baada ya miezi mitatu utenda kupima kuhakikisha afya yako.

Watumishi wa afya pia wanamiongozo yao ya kupata dawa hizo kama wakipata ajali hizo maeneo ya kazi, hawa wote wanafahamu utaratibu sina haja ya kuongelea hapa.

Ukweli ni kwamba dawa za ARV zinaweza kutumika kama kinga kwa  watu ambao hawaja athirika kabisa kama wangekua wanazimeza kila siku, tatizo ni kwamba zina madhara makubwa sana ikiwemo kuharibu figo na maini kabisa.

Mwisho: makala hii sio ruhusa ya kuruhusu watu waanze kushiriki ngono zembe kwa sababu dawa zipo, hapana.. endelea kutumia kondomu kwani watu bado wanaendelea kuumiza vichwa kupata dawa kamili ya ugonjwa huu.. nimeandika makala hii ili wewe mwanachi ikitokea umepata matatizo haya uweze kuwahi hospitali na kudai haki zako.kwa maelezo zaidi bofya hapa kusoma
tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga


                         DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                          MAWASILIANO 0653095635/0769846183

                                                    STAY ALIVE
                                                 

Maoni 1 :