Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa miezi sita ya kwanza ili kumjenga mtoto.................................
mifumo mingi ya mwili
inataka virutubisho vingi ili mtoto akue akiwa na akili nzuri. Lakini pia mtoto anatakiwa
aendelee kunyonya kwa miaka miwili hata kama ameanzishiwa chakula kingine kama
uji baada ya miezi sita.
Vifo vya akina mama kipindi cha uzazi na kuacha watoto,
magonjwa kama ukimwi, mama kua na maziwa kidogo na kazi nyingi sababu ya ugumu
wa maisha imefanya wanawake wengi kuanza kutumia maziwa mbadala kama lactogen1
na lactogen2 kuwapa watoto hao ambao hawapati kabisa maziwa ya mama au wanapata
kidogo sana.
Lakini gharama ya maziwa hayo imekua juu sana kiasi kwamba
wanawake wengi wanashindwa kununua maziwa hayo hivyo leo ntatoa elimu ya jinsi
ya kutengeneza maziwa hayo ukiwa nyumbani kwa gharama ndogo sana kama
ifuatavyo.
Mahitaji:
- Maziwa ya ng’ombe
- Maji
- Sukari
- virutubisho.[vidonge vya multivitamin vyenye mchanganyiko wa madini ya vitamin A,iron, folic acid, zinc na mengineyo]
jinsi ya kuchanganya:
- Chukua nusu lita ya maziwa hakikisha maziwa haya ya ng”ombe hayajachanganywa na maji kabisa kwani kuna tabia za wauzaji kuchanganya ili wauze maziwa mengi hivyo nunua kwa mtu unayemuamini sana.
- Changanya maziwa yako na robo lita ya maji kisha chemsha vyote kwa pamoja mpaka yachemke ili kupunguza sodium na calcium nyingi iliyomo kwenye maziwa haya na kuua wadudu wa kwenye maji na kwenye maziwa pia.
- kabla maziwa hayajapoa weka vijiko kumi vya sukari{kijiko cha chai na sio kile cha kulia chakula}.
- Maziwa yakishapoa saga vidonge viwili vya multivitamin kisha changanya na maziwa hayo.{vidonge hivi vinapatikana maduka ya madawa kwa bei ndogo sana, kopo zima lenye vidonge elfu moja halizidi shilingi elfu kumi]
- Sasa unamchanganyiko uleule wa lactogen ambao unaopoteza pesa kila siku kununua dukani, mpe mtoto na kikombe au nyonyo ya dukani.
- Onyo; maziwa hayo hayatakiwi yalale mpaka asubuhi. Kila siku
tengeneza mengine kulingana na mahitaji yako na kama unaona mchanganyiko wangu
unatoa maziwa mengi sana kwa mtoto wako unaweza ukapunguza nusu kwa kila kitu
nilichotaja au kama mtoto wako anakunywa zaidi ongeza vipimo.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0 maoni:
Chapisha Maoni