Kua na ngozi laini na yenye afya ni matamanio ya kila mtu,
bahati mbaya hakuna uchawi katika hili, ili uwe na ngozi inayovutia na nzuri
lazima ufuate kanuni za afya ikiwemo kufanya mazoezi kunywa maji mengi na kula
vyakula vinavyotengeneza ngozi yako kuwa nzuri..
Vyakula vingi ni vizuri kwa afya ya binadamu lakini leo
nataka kuongelea vyakula vinavyofanya baadhi ya ngozi za watu kua laini sana
kulio wengine, wasanii marufu wa nje na ndani ya nchi hutuhumiwa sana kwa kutumia
kemikali kuboresha ngozi zao lakini sio kweli na hii ndio siri yao.
Maparachichi: haya ni matunda ambayo yamekua yakifahamika
miaka mingi kwa kuboresha ngozi, tunda hili lina vitamin e, potassium, folic
acid na mafuta. Mchanganyiko huu hufanya ngozi kua laini sana na kupunguza
uwezekano wa magonjwa ya moyo na kiharusi.
Machungwa: haya yana maji mengi ambayo huupa mwili maji
na vitamin c ambayo ni moja ya vitamin nzuri sana kwa ngozi ya binadamu.
Zabibu; matunda haya huongeza maji mwilini lakini kazi yake
kubwa ikiwa kuzuia madhara ya jua ambayo yanatokea kwenye ngozi..
Samaki; tafiti mpya zimeonyesha kwamba omega 3 ambayo
inapatikana kwenye samaki huuzuia seli za kansa kusambaa mwilini na kuifanya
ngozi kua laini kama ya mtoto mdogo…
Mboga za majani; hizi ni kama mchicha, spinachi, matembele
na zingine nyingi za kijani zina mchanganyiko wa vitamin A, C, K ambazo pia
huongeza kinga ya mwili na kuuia madhara makali yatokanayo na mwanga wa jua..
Mwisho: narudia tena, mambo yote yanayofanya mabadiliko ya
mwili wako bila kutumia dawa sio ya kupata kwa siku moja wala mbili bali
yanatakiwa yawe ndio maisha yako sio ukiona hii makala ufuate kwa wiki moja afu
uache useme dokta muongo hapana inatakiwa iwe ni sehemu ya maisha yako. tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
STAY ALIVE....
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
0 maoni:
Chapisha Maoni