.
Kusahau sana ni hali inayoweza kumfanya mtu akajichukia
sana, kukosa raha na kua na mawazo sana afanye nini kupambana na adha hiyo..
Hii ni hali ambayo inaathiri watu wengi sana yaani wakubwa
na wadodo kulingana na chanzo lakini inakua mbaya zaidi mtu anavyozidi
kuongezeka umri kwani seli za ubongo zinazidi kupungua zaidi.
Kuna hali kitaalamu inaitwa dementia ambayo hutokea mara
nyingi katika umri mkubwa na huambatana na kusahau kuliko pitiliza yaani
kupotea katika mazingira unayoyafahamu, kusahau majina ya kawaida kabisa kama
embe, pazia, kiti na meza, kurudia kuuliza swali la aina moja kila siku, na
kuchanganyikiwa lakini hali huu huletwa na magonjwa Fulani mfano Alzheimer's
disease{hii hali ni hatari na hutibiwa kitaalamu}
Lakini watu wengi hawafiki huko, ila watu wengi sasa
wanasahau vitu vya kawaida sana yaani unakuta mtu kaenda na baiskeli au gari
sehemu afu karudi kwa mguu na kuvisahau huko, mtu anasoma sasa hivi afu
akifunika kitabu amesahau, unaweka pochi sehemu unasahau uliweka wapi, unameza
dawa afu baadae hukumbuki kama ulimeza au vipi, unasahau pesa mfukoni, unapewa
kazi afu unasahau kuifanya na kadhalika..
Hali hizi sasa zinawatesa watu wengi na hawajui wafanye
nini, lakini kuna tabia kadhaa ambazo zinaambatana na hali hizi kama
ifuatavyo..
Kukosa usingizi: binadamu anatakiwa apumzike mpaka masaa
nane kwa siku moja, lakini kutokana na ugumu wa maisha watu hujikuta wanalala
mpaka masaa manne kwa siku. Hii huathiri uwezo wa kufikiri na kusahau kirahisi
sana.
Madawa: dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali hua na madhara
madogo madogo ambayo yanaleta kusahau.. mfano dawa za kutibu presha kama
captopril, dawa za kutibu madonda ya tumbo mfano cimetidine na dawa za kutibu
mgandamizo wa mawazo mfano amitriptyline.
Ulevi: unywaji wa pombe uliopitiliza huharibu uwezo wa
kumbukumbu za mda mfupi yaani kusahau kitu umekifanya mda huo huo hivyo
inashauriwa kunywa pombe kiafya. Yaani bia mbili kwa siku mwanaume na bia moja
kwa siku mwanamke ambazo hazina alcohol zaidi ya asilimia tano zinatosha kiafya.
Mgandamizo wa mawazo: kitu chochote kinachokufanya ushindwe
kutuliza akili, kitakufanya usahau sana na kushindwa kupata kumbukumbu
ulizoziweka siku za nyuma.
Upigaji wa punyeto: tatizo hili la kusahau kwasababu ya
punyeto ndio chanzo kikuuu kwa vijana wengi chini ya miaka 35 kwani tabia hii
huambatana na maumivu ya kichwa, uchovu mwingi na kusahau kusiko kwa kawaida. HIZI NDIO NJIA SABA ZA KUACHA PUNYETO KABISA...
Uvutaji wa sigara: sigara ina kemikali iitwayo nikotini
ambayo huenda kwenye ubongo na kuua seli za ubongo na kumfanya mtu asahau sana.
Kutokua makini; tatizo la kufanya mambo haraka haraka huleta
kusahau sana, kama wewe una mambo mengi amka mapema uyafanye ila ukianza
kukimbia kimbia njiani ndio chanzo kikuu cha kusahau mambo mengine, pia tabia
ya wanafunzi kusoma kwenye kelele sana au huku wanasikiliza mziki hujikuta
hawaambulii kitu baada ya kufunika daftari.
MATIBABU
Matibabu ya yasiyo ya dawa {non pharmacological treatment]
Kuacha tabia hizo juu ni njia bora zaidi ya kurudi katika
hali yako ya kawaida japokua itakuchukua mda mrefu kidogo.lakini pia kuna njia
za kufanya ili kuweza kukumbuka vitu baada ya kuacha tabia hizo hapo juu kama
ifuatavyo.
Weka alarm; simu na saa nyingi zina alarm hivyo kama kuna
kitu unataka kukifanya mda Fulani basi weka alamu ambayo ikiita tu utakumbuka
sababu kwanini uliiweka.
Tumia kalenda: watu wengi tuna kalenda nyumbani lakini
hatuzitumii. Kama una mpango wa kukutana na mtu Fulani siku mbele zijazo
zungushia tarehe hiyo na kalamu itakusaidia kuona kila siku na kukumbuka.
Andika kwenye karatatasi; ukiamka asubuhi hebu andika mambo
yote unayotegemea kuyafanya kwa siku nzima kisha weka mfukoni, hii itakusaidia
kufanya vitu kwa mipango makini.
Fanya hicho kitu kitu sasa hivi: kama unataka kufanya kitu Fulani
na hauna kazi nyingine kwa sasa basi kifanye sasa hivi ili usisahau tena
baadae.
Tafuta mtu wa kukumbusha; anaweza kua mtu yeyote unayeishi
nae, unaweza kumwambia mambo unayotaka kufanya ili awe anakukumbusha kila siku.
Usipokee kazi kama una kazi nyingi:mtu akikuomba msaidie
kitu na unaona ratiba zako zimejaa kataa na umwambie ukweli kwani ukiikubali
kazi hiyo utasahau..
Fanya mambo taratibu na umakini mkubwa: tabia ya kufanya
vitu haraka haraka ndio hufanya mtu asahau sana, hebu kua makini na wakati
mwingine jisemee moyoni. Mfano ukiweka simu kwenye droo sema moyoni ‘nimeweka
simu kwenye droo’ itakusaidia kukumbuka.
tumia virutubisho:hivi ni virutubisho vinavyoongeza na kusaidia usambazaji wa damu kwenye ubongo wa binadamu, hutengenezwa na mimea asilia na havina kemikali kabisa.mfano ginkgo plus amabao ni mmea ambao hupatikana nchi za ulaya..mmea huu pamoja na kuongeza kumbukumbu hutumika kama ant aging huku nchi za uchinna yaani huchelewesha mtu kuonekana mzee. dose ya virutubisho hivi ni kimoja kwa mwezi.
Mwisho; mchanganyiko wa matibabu ya dawa[pharmacological treatment}
na yale yasiyo ya dawa {non pharmacological treatment} hufanya kazi haraka na
kwa ufasaha kuliko kutumia aina moja pekee ya matibabu.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
STAY ALIVE
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
STAY ALIVE
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]
Mimi nina henry Lovie kutoka Los Angeles, mimi nina kushukuru kwa Dr Maji kwa ajili ya kusaidia mimi na kusaidia yangu ili kukomesha chanya [+ ve ] carrier wangu virusi vya ukimwi. Nasema ni Mungu kutuma kwangu , wiki iliyopita nilikwenda kwa karibu na hospitali kwa kuangalia hali yangu, ilikuwa jambo la kushangaza kwamba maabara fundi au maabara ya sayansi alisema kuwa mtihani ni HIV -ve . Unaweza kuwasiliana naye katika drwaterhivcurecentre@gmail.com au namba ya simu +2349050205019 ushauri wangu ni kuwasiliana naye na kuhakikisha kuwa ninyi kizazi VVU huru, shukrani kubwa kwa Dr Maji.
JibuFutaChapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
JibuFutaChapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
JibuFutaasante sana
JibuFutaNataka dawa niwe nasahau
JibuFuta