Ukimwi sio ugonjwa mpya masikioni mwa watu kwani uliingia
nchini miaka ya nyuma sana na kuua watu
wengi mno. Japokua kuna watu wengi wamejitangaza sana wakidai wana uwezo wa
kutibu ugonjwa huu lakini mpaka sasa hakuna dawa iliyopatikana ya kumaliza
kabisa ugonjwa huu, lakini bado hatujakata tama kabisa kwani watafiti bado wako
maabara mbalimbali duniani wakijaribu kutafuta dawa ya ugonjwa huu.
Wakati unasoma makala hii huenda umesikia habari nyingi za ukweli
na uongo kuhusu ukimwi lakini haya ndio mambo mengine nakuletea ambayo huenda
ulikua hujui kuhusu ukimwi…
Huwezi kuambukizwa kwa kula chakula chenye damu yenye
virusi: virusi vya ukimwi haviwezi kuishi nje ya seli ya binadamu wala kwenye
joto kali sana. Mfumo wa chakula wa
binadamu una tindikali kali sana na joto ambalo virusi hivyo vikifika tumboni
haviwezi kuishi tena hata kama tindikali hiyo isingekuepo vingekufa kwa kukosa
chakula kwani vinategemea sana chakula cha seli, hivyo maambukizi lazima yapitie kwenye mshipa wa damu au kwenye vidonda.
kati ya watu watano walioathirika mmoja hajijui kama ni mgonjwa: utafiti unaonyesha kwamba kuna watu wengi hawajui kama tayari wameathirika na wanaendelea kuusambaza ugonjwa huu bila kujua, njia salama ya kukwepa ugonjwa huu ni kupima tu na kuanza matibabu mapema kama umeathirika na kama hujaathirika basi tumia kondomu ujikinge.
Ukimwi sio ugonjwa wa watu Fulani ila wa watu wote; ukiwa
hujaathirika unaweza kuhisi wewe ukimwi haukuhusu na kuendelea na ngono zembe
ila naomba nikwambie kuna vijana wadogo wengi sana wameathirika, watoto wengi,
wazee na wamama ambao nao walikua na mawazo kama yako. Bahati mbaya ukimwi hautoi
nafasi ya pili kwa walioathirika kwani walioathirika sasa hivi wasingerudia makosa
kama hawakupata kwa bahati mbaya.
Dalili za ukimwi hua zinajificha wakati mwingine; mtu
akianza kushambuliwa kwa mara ya kwanza hupata dalili za magonjwa kama za
magonjwa mengine ya kawaida kama mafua, homa na kuvimba tezi kisha dalili hizo
hupotea hivyo ni vigumu sana kujitambua au kumtambua mgonjwa bila kupima.
huweza kuchukua zaidi ya miaka kumi kuanza kuugua kabisa au AIDS: mtu anaweza kua na virusi vya ukmwi na wala asionekane mgonjwa na
inaweza ikachukua miaka mingi sana kujionyesha iwapo mtu anaishi vizuri upande
wa mazoezi na chakula.
Kuna virusi vya ukimwi vya aina mbili; kitaalamu tunaita HIV1
na HIV2, lakini mmoja wao yaani HIV1 anashambulia na kuua haraka kuliko HIV2 na
ndio aina ambayo inapatikana zaidi duniani na mtu mmoja anaweza kua na virusi
wote ndio maana inashauriwa kuendelea kutumia kondomu kujikinga na maambukizi mapya ata kama umeathirika.
Mtu mwenye virusi anaweza kuzaa watoto ambao hawana ukimwi:
mwanamke mjamzito aliyeathirika huweza kuanzishiwa dawa ya kumkinga mtoto
aliyeko tumboni kipindi chote cha ujauzito na kumzaa mtoto ambaye yuko salama
kabisa na mtoto huyo akaishi maisha ya kawaida.
Mtu mwenye virusi anaweza kushiriki tendo la ndoa kama
kawaida; lakini hapa lazima atumie kinga ili aweze kuwalinda wapenzi wake na yeye
pia ajilinde na maambukizi mapya na aina nyingine ya virusi vya ukimwi.
Ukimwi sio mwisho wa maisha: kuna magonjwa makali kuliko
ukimwi, ukipata kansa ya maini leo hata mwaka unaweza usimalize hivyo sio
busara kuchukua ukimwi kama vile umehukumiwa kunyongwa hapana bado una nafasi
ya kutimiza malengo yako..
Ukilala na mtu mwenye ukimwi uwezekano wa kuupata ni 0.3% kwa kila unapokutana naye:
watu wengi hujitapa kutembea na watu wengi baada ya kuupata wakidhani wanausambaza lakini naomba nikwambie
kama kila aliyelala na muathirika angepata ukimwi kila basi dunia yote
ingekua imeathirika lakini simaanishi uache kutumia kondom hiyo 0.3% inaweza kua wewe.
Ukimwi huonekana kwenye vipimo baada ya miezi mitatu au sita
ya kwanza; watu wengine huchukua wanawake mtaani na kwenda kuwapima chumbani
kisha kulala nao wakidhani wako salama. Kama mtu kaambukizwa mwezi uliopita
virusi havionekani kwa vipimo na anakua na virusi wengi kuliko ata mtu aliyeko kwenye matibabu hivyo acha kujidanganya.
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO..
DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO..
STAY ALIVE...