data:post.body HIZI NDIZO SIKU HATARI ZA KUBEBA MIMBA KWA WANAWAKE.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIZO SIKU HATARI ZA KUBEBA MIMBA KWA WANAWAKE..



                                                           

      
Moja ya makala zilizopita niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa kiume na jinsi ya kujua siku za mwanamke za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Leo ntarudia maada hii na naomba msomaji usome kwa makini sana.

Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.

Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao. 

Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka  sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.

Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku  28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.

Kama mzunguko wako ni mrefu labda  siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.

Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni siku yai linashuka hivyo ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.

kama mzunguko wako ni  wa kawaida yaani siku 28 sasa chukua 28 toa 14 unapata 14 yaani siku ya 14 ndio hatari zingine ni siku ya 10,11,12,13,14,15

Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka  ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike. kama mzunguko wako wa hedhi unabadilika badilika soma hapa http://www.sirizaafyabora.info/2015/06/jinsi-ya-kuhesabu-ziku-za-hatari-za.html


                                              

                                                                  STAY ALIVE

                             MAWASILIANO 0653095635/0769846183[tuma meseji tafadhali]

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

Maoni 24 :

  1. mke wangu anapata siku zake tarehe 10, zamani ilikuwa tarehe 14, sasa ni kumi, je hili ni tatizo, pia siku gani kwake ni hatari kupata ujauzito

    JibuFuta
    Majibu
    1. Hilo cyo tatizo ila kubadilika kwa siku zake kuna tokana na vyakula anavyo tumia pamoja na kaz anazo fanya pia kama ana magonjwa ya mara kwa mara hii pia ni sababu kubwa ya mzunguko.kubadilika

      Futa
  2. Mchumba wangu alikuwa akipata tarehe 20,juzi kapata tarehe 15.Je Ni siku zipi nzuri kupata mtoto?

    JibuFuta
  3. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  4. Kwa hiyo kama ulipata tarehe nane ukasex tarehe 17 kama mzunguko ni Sikh 28 in mimba inatokea

    JibuFuta
  5. Swali langu ni kwamba inawezekana mwanamke kuwa na siku tofauti za kuwa katika kipindi cha kuvuja damu{bleed}? Au kwa maana kwamba mwezi uliopita alivuja damu kwa muda wa siku tatu halafu mwezi uliofuatia akavuja siku tano na mabadiliko hayo yanaletwa na nini?

    JibuFuta
  6. Kwa mfano nimeingia tarehe 17jan mwezi february 18 mzunguko wangu utakuwa ni wasiku ngapi na nizip tarehe sahihi za kushika mimba maana napata shida kidogo tafadhal doc.

    JibuFuta
  7. Kama nimekutana na Mke wangu siku ya hatari na nikatoa nje kabla ya kufika kileleni, Je kuna uwezekana wa kupata mimba?

    JibuFuta
  8. Kama nimekutana na Mke wangu siku ya hatari na nikatoa nje kabla ya kufika kileleni, Je kuna uwezekana wa kupata mimba?

    JibuFuta
  9. Ka mwez uliopita nikipata hedh trh13 af mwez ujao trh8apo unakuwani mzunguko wa siku ngapi na trhe za hatar in zip

    JibuFuta
    Majibu
    1. Hapo utachukua hyo 13+?.=30 hvyo utachukua 17 +7 utapata 24hvyo mzunguko wako utakuwa n siku 24

      Futa
  10. Ka mwez uliopita nikipata hedh trh13 af mwez ujao trh8apo unakuwani mzunguko wa siku ngapi na trhe za hatar in zip

    JibuFuta
  11. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  12. Kwaiyo watu ambao mzunguko wao Sio mfupi awawezi kupata mtoto wa kit me

    JibuFuta
  13. Kwa mfano mtu mzunguko wake ni siku 26 siku zake ya zatari ambazo anaweza kupata ujauzito ni zip?

    JibuFuta
  14. Baadhi ya maswali yanajirudia wandugu sio kila mtu ujibiwe kwa kutajwa jina unacho ambhwa hesabu mzunguko wako kwanza kwa mda wa miezi mitatu. alafu urudi kusoma maelezo ya mtaalamu kuanzia mwanzo uajielewa.

    JibuFuta
  15. Jaman nimefanya mapz na mwenzangu,akiwa katika siku zake je mimba itaingi

    JibuFuta
  16. Mkuu nimekupata vizuri sana asant kwa ufafanuzi ngoja tuifanyiee kazi tutafute watoto

    JibuFuta
  17. mimi ni mama mwenye umri wa miaka 43 ni mama wa familya miaka 5 sipendelei tena kupata mtoto kwa mara ya mwisho nimezaa mapacha wenye umri wa miak 2 uzazi wangu wa mpngo ni kalenda lkn mara hii mzunguko wangu umekuwa na siku 22 badala 26 inakuwaje na nifanyeje

    JibuFuta
  18. Kama mtu umenifanya tarehe 21 February na ukuja kufnya 12 march kuna uwezekano wa kupata mimba

    JibuFuta
  19. mpenz wangu aliingia piriod trh 28 baada ya siku tano akuona dam nikafanya nae mapenx piriod ikarud tena kama siku nne tatiz nn hapo

    JibuFuta
  20. mimi huona period tarehe 30 hadi 4 siku hatari ni gani

    JibuFuta