data:post.body Aprili 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

FAHAMU MADHARA MAKUU MATANO YA KULAMBA SEHEMU ZA SIRI.



                                                                         

Kukua kwa kasi ya utandawazi kumeleta maendeleo makubwa ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Pamoja na hayo yote kuna mambo ya ambayo waafrika tumeyaiga nikiimanisha ambayo sio jadi yetu pia ni hatari kiafya hapa nikimaanisha kulambana sehemu za siri kabla ya ngono bila kujua madhara makubwa yasababishwayo na tabia hiyo.

Leo hii kuna watu hawaridhiki na kufanya ngono bila kulamba au kulambwa sehemu hizo za siri lakini leo naomba nikupe madhara makuu ya kushiriki aina hii ya ngono..

Kansa ya koo: kirusi ambacho kinasababisha kansa ya mlango wa uzazi kwa mwanamke huweza kuambukizwa na kushambulia koo la chakula na kusababisha kansa ya koo, ambayo  ziku zote husababisha kifo kwani haina matibabu ya kuponya kabisa.

Magonjwa ya zinaa; haya ni kama gonorea, kaswende na herpes simplex ambayo huanza kwa kushambulia mdomo na yamekutwa kwa watu wengi sana ambao hushiriki sana aina hii ya ngono .

Magonjwa ya ini; virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ini maarufu kama hepatitis B huweza kuambukizwa kwa njia hii ya kulamba sehemu za siri, huu ni ugonjwa hatari ambao husababisha kansa ya maini mwishoni.

Ugonjwa hatari wa ukimwi: japokua tafiti zinasema sio rahisi kuathirika na ugonjwa wa ukimwi kwa njia ya kulamba sehemu za siri ila uwezekano upo wa kupata ukimwi kwa kupitia maji maji ya ukeni au ya uume na michubuko ya mdomoni ya mlambaji.

Magonjwa ya kinywa; bacteria wengi wanaopatikana kwenye sehemu za siri huweza kushambulia sehemu ya wazi ya jino na kusababisha kuoza kwa jino na maumivu makali sana ya meno

Mwisho; haya ni baadhi ya magonjwa yanayofahamika mpaka sasa hivi yatokanayo na aina hii ya ngono…mengine bado yanafanyiwa utafiti sehemu mbalimbali. Onyo; usijaribu au kuiga mambo usiyoyajua kwani unajihatarishia afya yako wewe na mwenzi wako.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                             Mawasiliano; 0653095635\0769846183

                                              STAY ALIVE………

                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO




KAMA UMESHAWAHI KUTOA MIMBA FANYA HAYA MAMBO MATATU.

                                                                 



Makala iliyopita niliongelea madhara sita ya kutoa mimba, kutokana na jamii yetu kukumbwa sana na janga hili la utoaji wa mimba hasa kwa mabinti wadogo ambao wengi wao wapo vyuoni na mashuleni.

Kutokana na maswali mengi niliyoulizwa nini cha kufanya kwa ambao tayari wameshatoa mimba nimeamua niandike makala hii. Mambo yenyewe ni haya…
  • Nenda hospitali uonane na daktari;  ukitoa mimba kuna madhara mengi yanayofuatia ikiwemo ugumba, na kuharibika viungo vya uzazi.. nenda ukapige picha ya ultrasound kuangalia hali ya viungo vya uzazi, na kama vinaumwa vianze kutibiwa mapema iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika. Pia pima magonjwa mengine ya kuambukizwa ikiwemo ukimwi, kaswende na gono kwani ni magonjwa yanayo ambatana na ngono zembe. usiogope hakuna daktari wa kukupeleka polisi kwa kutoa mimba..
  • Onana na mtaalamu wa ushauri: kama una mawazo mengi kwanini umetoa mimba na unajutia maamuzi yako au moyoni unahisi umefanya kosa kubwa kwa binadamu au mungu wako nenda unana na mshauri na atakusaidia kurudi katika hali yako ya kawaida.
  • Chagua njia ya uzazi wa mpango:  kuna watu wameshatoa mimba mpaka tano sasa hivi, mimi naona huo ni uzembe kwani kuna njia nyingi sana za kuzuia ujauzito. Kama huwezi kondomu njia ya kijiti ni nzuri kuliko zote kwani siku ukitaka mtoto unakitoa kijiti na kunasa mimba haraka. njia ya kalenda ni nzuri pia ila wengi hawaiwezi na inataka umakini sana hivyo achana nayo..Acha kusikiliza kelele za watu eti njia hizo zina madhara kwani hizo ni imani potofu na ukipuuzia utaendelea kutoa mimba zaidi kitu ambacho ni hatari kiafya.
  •  tumia virutubisho vya uzazi; mara nyingi kutoa mimba huharibu mfumo wa homoni za uzazi wa wanawake na  maumbile ya uzazi.hali hii ni hatari na ndio hufanya wanawake wengi kushindwa kubeba mimba siku za usoni. tumia virutubisho vya multmaca ambavyo vimesaidia sana kurudisha hali ya homoni katika kawaida yake na kusaidia kubeba mimba kwa wanaozitafuta.  tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                            
        
     
                                   DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                         MAWASILIANO 0653095635\0769846183

                                                      STAY ALIVE….

HAYA NDIO MADHARA SITA YA KUTOA MIMBA….



                                                                         


Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..kwa maelezo zaidi.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                                
                                                               STAY ALIVE…
                                             Mawasiliano 0653095635/0769846183
                                            DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

HIZI NDIZO SIKU HATARI ZA KUBEBA MIMBA KWA WANAWAKE..



                                                           

      
Moja ya makala zilizopita niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa kiume na jinsi ya kujua siku za mwanamke za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Leo ntarudia maada hii na naomba msomaji usome kwa makini sana.

Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.

Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao. 

Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka  sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.

Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku  28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.

Kama mzunguko wako ni mrefu labda  siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.

Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni siku yai linashuka hivyo ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.

kama mzunguko wako ni  wa kawaida yaani siku 28 sasa chukua 28 toa 14 unapata 14 yaani siku ya 14 ndio hatari zingine ni siku ya 10,11,12,13,14,15

Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka  ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike. kama mzunguko wako wa hedhi unabadilika badilika soma hapa http://www.sirizaafyabora.info/2015/06/jinsi-ya-kuhesabu-ziku-za-hatari-za.html


                                              

                                                                  STAY ALIVE

                             MAWASILIANO 0653095635/0769846183[tuma meseji tafadhali]

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO