data:post.body (SAIKOLOJIA) HIZI NDIO NJIA KUMI NA MOJA ZA KUMSAHAU MPENZI ALIYEKUUMIZA.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

(SAIKOLOJIA) HIZI NDIO NJIA KUMI NA MOJA ZA KUMSAHAU MPENZI ALIYEKUUMIZA..                                                                      

Miaka inavyozidi kwenda mbele uhuru wa binadamu unaongezeka sana kutokana na sera za demokrasia na kudidimia kwa maadili ya kidini, hivyo kuwapa watu nafasi kubwa ya kuingia kwenye mahusiano mapema.

Hali hii pia imechangia kwa ongezeko la kuumizwa kimapenzi kwa watu wengi sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa za fedha, usaliti,umbali kati ya wapenzi, shinikizo la wazazi, utofauti wa dini, mitazamo tofauti kati ya wapenzi na kadhalika.

Madhara makubwa sana yamekua yakisababishwa na hali hii ya kuachana ikiwemo watu kujiua hasa vijana, kuathirika kisaikolojia, kufeli mitihani, kuacha kazi na kupoteza muelekeo wa kimaisha kabisa. 
Leo naenda kuongelea jinsi ya kumsahau mpenzi wako uliye achana naye na kuanza maisha mapya yenye furaha na amani kama zamani..

 Usiyazuie machozi yako:
Maumivu haya yatakufanya ulie sana na kujilaumu kwanini ulipenda lakini ni vizuri kulia sana kadri unavyoweza kwani hii itakupa ahueni na kupunguza maumivu makali unayoyapata.
Futa namba zake:
Kuendelea kua na namba zakekutakufanya uendelee kumpigia ili abadilishe mawazo yake hii itakufanya uumie zaidi hasa kama hakutaki tena na huenda ana mtu mwingine badala yako. Hata kama umezikariri kichwani usiziandike tena kwenye simu yako.

Kua bize na mambo mengine;
Fanya mazoezi, katembelee sehemu ambazo hujawahi kwenda na rafiki zako, angalia filamu za mapigano, sikiliza miziki isiyohusiana na mapenzi. Hii itakufanya usahau mapema kuliko kukaa nyumbani peke yako na kuwaza sana kuhusu mpenzi wako.

Usifiche hisia zako:
Kama umeachwa usione aibu, ongea na ndugu na jamaa zako na uwambie ukweli kuhusu yaliyokutokea, hii itakufanya upunguze mzigo wa nawazo kichwani kwako na utahisi hali ya wepesi moyoni mwako hasa kwa ushauri utakaopata. Pia unaweza kuwaona wataalamu wa ushauri kwa ushauri zaidi.

Usitafute mpenzi mwingine kuziba pengo lake haraka.:
Watu wengi huchukua wapenzi wapya haraka ili kuzuia maumivu lakini hii sio njia sahihi kwani siku maumivu yako yakiisha utagundua kwamba hauna mapenzi ya kweli juu ya huyu mpenzi wako mpya na utaishia kumuumiza tena huyo uliyemchukua.(mwanamke anaweza kujifunza kumpenda mtu lakini mwanaume asipokupenda mwanzoni hawezi kujifunza kukupenda hata iweje)

Andika mapungufu yake kwenye karatasi:
Jaribu kukumbuka matatizo na mapungufu ya huyo mpenzi wako hii itakufanya uone kwamba hakuna madhara uliyoyapata ila faida na itakupunguzia machungu yako.

Msamehe mpenzi wako ata kama hajakuomba msamaha:
Njia pekee ya kua huru kihisia ni kusamehe, visasi moyoni havitakusaidia kabisa kuondokana na maumivu na utajikuta unawaza kufanya mambo ya ajabu ambayo yanaweza kukuletea matatizo ikiwemo kumuua au kumjeruhi. 

Kaa mbali na vitu vinavyokukumbushia kuhusu mpenzi wako:
Sikiliza nyimbo mpya, weka mbali picha zake na zawadi zote alizokupa, usitembelee sehemu ambazo zinakukumbusha kuhusu yeye. Kua na marafiki wapya ambao hawakumfahamu mpenzi wako.(simaanishi uwaache marafiki wa zamani), pia usijaribu kua rafiki wa mpenzi uliyeachana nae kwani utajikuta unaumia zaidi labda baadae sana ukishasahau.

Usiseme mabaya kuhusu mpenzi wako au familia yake:
Hii ni hali ya mpito tu, ukianza kupost vitu vya ajabu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano yako haitakusaidia kitu bali kujiabisha kwa jamii na siku maumivu yakiisha utajuta sana kwanini uliandika mambo hayo. Hili ni tatizo sugu kwa watu wengi walioachana kupost vitu kama kumkomesha mpenzi wake wa zamani. Naomba nikwambie mapenzi hayana kisasi kama umeachwa, umeachwa tu. kumbuka silence is the best weapon..

Fikiria faida za kuishi bila mpenzi:
Kua peke yako kuna faida nyingi ikiwemo kua huru na maamuzi yako, kuchagua marafiki unaotaka, kujikinga na magonjwa ya zinaa,kuishi maisha unayotaka bila kuhofia kukosolewa, unaweza kuzima simu yako ata wiki nzima bila hofu, kulala peke yako bila bugudha, kupunguza msongo wa mawazo ambao hutokana na ugomvi wa mara kwa mara.

tumia dawa za kupunguza mawazo; wakati mwingine maumivu ya kuachana na mpenzi yanaweza kua makali sana, mtu akshindwa kupata usingizi, kufanya kazi zake, kukosa furaha kabisa na kulia kila siku. hii huathiri sana mfumo wa maisha husika na huweza kusababisha mtu kuamua kujiua kabisa kama mnavyosikia watu waliojiua sababu ya mapenzi. ndio maana kuna dawa maalumu za watu wenye msongo wa mawazo. ukitumia dawa hii mwili unatulia na ubongo unapumzika sana. itakupa usingizi na kila ukiamka unakua na furaha upya na unaendelea na maisha yako kama kawaida. dawa hizi zinaharakisha sana kusahau na kuendelea na maisha yako haraka kuliko kujaribu kupambana mwenyewe.mfano wa dawa hizo ni bupropion,clomipramine na doxepin. zinapatikana maduka makubwa ya madawa kwa gharama kubwa kidogo lakini ni bora kuliko kuendelea kupoteza muda kumuwaza mtu ambaye hakutaki tena kwani hiyo ni gharama kubwa zaidi.

Amini utapata mwingine;
Katika dunia hii hakuna mtu alizaliwa kwa ajili ya mtu fulani..kila mtu anaweza kutengeneza mahusiano na mtu yeyote Yule na yakawa mazuri..jipe mda wa kutosha usiwe na haraka fanya mambo yako.. BELIVE ME, ANOTHER TIME WIL COME..NEW LIFE, NEW LOVE AND NEW HAPPYNESS.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                     Mawasiliano 0653095635/0769846183

                                                  STAY ALIVE…..
                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

Maoni 20 :

 1. thank you man

  JibuFuta
 2. Thanks a lot, it is helpful

  JibuFuta
 3. Thankx alot ! I think from now am going tostay safely

  JibuFuta
 4. Really nice never know before tanks for care us we heart broken

  JibuFuta
 5. Kama ikitokea mmeachana lkn mnaish mtaa mmoja na kila siku mnonana hii inakufanya uumie zaid pale unapomwona labda yupo na mpz mwingine sasa utafanueje

  JibuFuta
 6. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma

  Kwaheri Gerd Ulrich

  JibuFuta
 7. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
  *penda uchawi
  * kama unataka ex wako nyuma
  * Acha talaka
  *kuvunja mawazo
  * huponya viharusi na magonjwa yote
  * uchawi wa ulinzi
  *Ugumba na matatizo ya ujauzito
  Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
  Whatsapp: +2349046229159

  JibuFuta
 8. Thanks umenip njia

  JibuFuta
 9. Mume wangu amerudi!!! Baada ya miaka 1 ya ndoa iliyovunjika, mume wangu aliniacha na watoto wawili na maisha yangu yalivunjika. Nilitaka kuyamaliza, nusura nijiue maana alituacha bila chochote. Nimekuwa nimevunjika kihisia wakati huu wote na maisha yanaonekana kutokuwa na maana. Siku moja mwaminifu, nilipokuwa nikivinjari mtandao, nilikutana na baadhi ya shuhuda kuhusu Dk DAWN. Baadhi ya watu walishuhudia kwamba alimrudisha mpenzi wao wa zamani, wengine walishuhudia kwamba anarejesha tumbo na kuponya magonjwa kwa mimea. Nilipendezwa zaidi na upatanisho na mume wangu, ambao Dk. DAWN aliwezesha kumrudisha mume wangu ndani ya siku 3. Sasa mume wangu amerudi na tumekuwa tukiishi kwa furaha tangu wakati huo. Shukrani zote kwa Dk DAWN. Hapa, ninaacha mawasiliano yake kwa kila mtu. Maana kuna changamoto za aina yoyote,
  Barua pepe ( dawnacuna314@gmail.com )
  Whatsapp: +2349046229159

  JibuFuta