data:post.body HIZI NDIZO DALILI ZA MWANZO NA HATUA ZA MASHAMBULIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA BINADAMU.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIZO DALILI ZA MWANZO NA HATUA ZA MASHAMBULIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA BINADAMU..



                                                                     

Maabukizi ya virusi vya ukimwi sio neno jipya sana masikioni mwa watu wengi, ugonjwa huu upo duniani kwa karne kadhaa sasa na umepoteza maisha ya watu wengi sana.
Virusi vya ukimwi vikianza kushambulia mwili hujionyesha na dalili kadhaa mwanzoni lakini pia dalili hizo huja kulingana na hatua nne kuu ambazo shirika la afya duniani lilikaa na kuzipanga baada ya kufanya utafiti wa mda mrefu..

Ugonjwa huu ambao unashambulia sana kinga ya mwili huja na hatua na dalili zifuatazo kama ilivyotajwa.

HATUA YA KWANZA.[STAGE ONE]
Kuvimba kwa tezi zote za mwili.
                        

HATUA YA PILI
Kupungua uzito chini ya asilimia kumi bila sababu maalumu.
Kuugua mara kwa mara magonjwa ya kifua
Fangasi za kwenye ngozi na kucha.
Mkanda wa jeshi
Kuwashwa sana ngozi
                    

HATUA YA TATU
 Kupungua uzito kwa zaidi ya asilimia kumi bila sababu yeyote.
Kuharisha bila sababu zaidi ya mwezi mmoja..
Fangasi za mdomoni
Kifua kikuu.
Upungufu wa damu
Magonjwa ya mdomoni mfano gingivitis..
Homa za mara kwa mara.
                  

HATUA YA NNE..
Kukonda sana ..
Fangasi za koo la chakula..
Kuchanganyikiwa kiakili.
Kansa ya ngozi mfano karposis sarcoma
Kupungua na kuharibika kwa uwezo wa mishipa ya fahamu..
Kuharisha zaidi na zaidi.
upofu wa macho
                  

Kumbuka, mgonjwa akishahamia kwenye hatua Fulani harudi nyuma ataendelea na hatua za mbele.
Moja ya vigezo vya mgonjwa kuanzishiwa dawa za kurefusha maisha ni kufikia hatua ya tatu au ya nne, mgonjwa mjamzito na mtoto mdogo.

Watu wengi wakisoma makala kama hizi wanafikiri ukimwi ni watu Fulani lakini naomba nikwambie msomaji ukimwi upo Na unaua…. japokua ukifuata utaratibu wa matibabu utaishi maisha marefu na ya kawaida kama wengine.

Hivyo unashauriwa kujizuia na ukimwi kama inavyotangazwa kila siku, kupima mara kwa mara na kuanza matibabu haraka kama tayari umesha athirika..kwa maelezo na ushauri zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                          
                                                  MAWASILIANO 0653095635/0769846183

                                                         STAY ALIVE……..

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO[tuma meseji tafadhari]
angalizo; kwanzia sasa, ushauri wowote  kutoka kwa daktari, wa matatizo binafsi kwa njia ya simu utatozwa shilingi 5000, ushauri kwa kufika ofisini kwetu gongo la mboto dar es laam utatozwa shilingi 10000.malipo hayo yatafanywa kwa namba hizo hapo juu.karibuni sana...

Maoni 3 :

  1. moja kati ya dalili za kua na maambukizi ya ukimwi mkivimba tezi. je ni tezi gani hasa huvimba?. na pia tezi hizo hutoa maumivu?

    JibuFuta
    Majibu
    1. tezi za mwili mzima...shingoni,mapajani, kwapani na kadhalika

      Futa
  2. Hii itakuwaje kua mtu kaambiwa anavurusi kisha akaishi miaka zaidi ya 5 na akaongezeka uzito kama kawaida na hatumii dawa zozote za hiv?

    JibuFuta