data:post.body Machi 2015 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIZO DALILI ZA MWANZO NA HATUA ZA MASHAMBULIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA BINADAMU..



                                                                     

Maabukizi ya virusi vya ukimwi sio neno jipya sana masikioni mwa watu wengi, ugonjwa huu upo duniani kwa karne kadhaa sasa na umepoteza maisha ya watu wengi sana.
Virusi vya ukimwi vikianza kushambulia mwili hujionyesha na dalili kadhaa mwanzoni lakini pia dalili hizo huja kulingana na hatua nne kuu ambazo shirika la afya duniani lilikaa na kuzipanga baada ya kufanya utafiti wa mda mrefu..

Ugonjwa huu ambao unashambulia sana kinga ya mwili huja na hatua na dalili zifuatazo kama ilivyotajwa.

HATUA YA KWANZA.[STAGE ONE]
Kuvimba kwa tezi zote za mwili.
                        

HATUA YA PILI
Kupungua uzito chini ya asilimia kumi bila sababu maalumu.
Kuugua mara kwa mara magonjwa ya kifua
Fangasi za kwenye ngozi na kucha.
Mkanda wa jeshi
Kuwashwa sana ngozi
                    

HATUA YA TATU
 Kupungua uzito kwa zaidi ya asilimia kumi bila sababu yeyote.
Kuharisha bila sababu zaidi ya mwezi mmoja..
Fangasi za mdomoni
Kifua kikuu.
Upungufu wa damu
Magonjwa ya mdomoni mfano gingivitis..
Homa za mara kwa mara.
                  

HATUA YA NNE..
Kukonda sana ..
Fangasi za koo la chakula..
Kuchanganyikiwa kiakili.
Kansa ya ngozi mfano karposis sarcoma
Kupungua na kuharibika kwa uwezo wa mishipa ya fahamu..
Kuharisha zaidi na zaidi.
upofu wa macho
                  

Kumbuka, mgonjwa akishahamia kwenye hatua Fulani harudi nyuma ataendelea na hatua za mbele.
Moja ya vigezo vya mgonjwa kuanzishiwa dawa za kurefusha maisha ni kufikia hatua ya tatu au ya nne, mgonjwa mjamzito na mtoto mdogo.

Watu wengi wakisoma makala kama hizi wanafikiri ukimwi ni watu Fulani lakini naomba nikwambie msomaji ukimwi upo Na unaua…. japokua ukifuata utaratibu wa matibabu utaishi maisha marefu na ya kawaida kama wengine.

Hivyo unashauriwa kujizuia na ukimwi kama inavyotangazwa kila siku, kupima mara kwa mara na kuanza matibabu haraka kama tayari umesha athirika..kwa maelezo na ushauri zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                          
                                                  MAWASILIANO 0653095635/0769846183

                                                         STAY ALIVE……..

                                 DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO[tuma meseji tafadhari]
angalizo; kwanzia sasa, ushauri wowote  kutoka kwa daktari, wa matatizo binafsi kwa njia ya simu utatozwa shilingi 5000, ushauri kwa kufika ofisini kwetu gongo la mboto dar es laam utatozwa shilingi 10000.malipo hayo yatafanywa kwa namba hizo hapo juu.karibuni sana...

ZIJUE DALILI KUMI ZA MWANZO KABISA ZA UJAUZITO….



                                                                       

Ujauzito ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kubeba kiumbe kwenye mfuko wake wa uzazi, dalili za ujauzito wakati mwingine huweza kuchanganya watu na magonjwa mengine kama malaria na magonjwa ya njia za mkojo hasa mwanzoni mwa ujauzito, lakini pia kuna watu hawazipati dalili hizi na kushtuka mimba ikishakua kubwa kabisa.

Mimi kwa uzoefu wangu nimeshakutana na wanawake watatu katika vipindi tofauti wakiwa na ujazito wa miezi sita bila wao kujua wakihisi ni unene tu..

Dalili za ujauzito husababishwa na kuongezeka kwa kwa hormone za uzazi ndani ya mfumo wa damu wa mwanamke..lakini kabla ya kwenda kuhakikisha ujauzito na vipimo vitu vifuatavyo huonekana kwanza kwa mwanamke husika..

·         Kukojoa mara kwa mara

·         Kutoona siku za hedhi

·         Kichefuchefu na kutapika

·         Matiti kuuma na kuvimba

·         Kuchoka sana bila kazi

·         Kupoteza hamu ya kula

·         Kupata hasira au furaha ndani yam da mfupi.{mood swings}

·         Kizunguzungu

·         Kuongezeka joto la mwili.

·         Kuongezeka kwa uwezo wa kunusa harufu.

Ukiona dalili hizi kimbia ukahakikishe na vipimo kwani inweza kua tayari umepandikizwa kiumbe ndani ya mfuko wa uzazi..tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                                                           STAY ALIVE

                           DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO


(SAIKOLOJIA) HIZI NDIO NJIA KUMI NA MOJA ZA KUMSAHAU MPENZI ALIYEKUUMIZA..



                                                                      

Miaka inavyozidi kwenda mbele uhuru wa binadamu unaongezeka sana kutokana na sera za demokrasia na kudidimia kwa maadili ya kidini, hivyo kuwapa watu nafasi kubwa ya kuingia kwenye mahusiano mapema.

Hali hii pia imechangia kwa ongezeko la kuumizwa kimapenzi kwa watu wengi sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa za fedha, usaliti,umbali kati ya wapenzi, shinikizo la wazazi, utofauti wa dini, mitazamo tofauti kati ya wapenzi na kadhalika.

Madhara makubwa sana yamekua yakisababishwa na hali hii ya kuachana ikiwemo watu kujiua hasa vijana, kuathirika kisaikolojia, kufeli mitihani, kuacha kazi na kupoteza muelekeo wa kimaisha kabisa. 
Leo naenda kuongelea jinsi ya kumsahau mpenzi wako uliye achana naye na kuanza maisha mapya yenye furaha na amani kama zamani..

 Usiyazuie machozi yako:
Maumivu haya yatakufanya ulie sana na kujilaumu kwanini ulipenda lakini ni vizuri kulia sana kadri unavyoweza kwani hii itakupa ahueni na kupunguza maumivu makali unayoyapata.
Futa namba zake:
Kuendelea kua na namba zakekutakufanya uendelee kumpigia ili abadilishe mawazo yake hii itakufanya uumie zaidi hasa kama hakutaki tena na huenda ana mtu mwingine badala yako. Hata kama umezikariri kichwani usiziandike tena kwenye simu yako.

Kua bize na mambo mengine;
Fanya mazoezi, katembelee sehemu ambazo hujawahi kwenda na rafiki zako, angalia filamu za mapigano, sikiliza miziki isiyohusiana na mapenzi. Hii itakufanya usahau mapema kuliko kukaa nyumbani peke yako na kuwaza sana kuhusu mpenzi wako.

Usifiche hisia zako:
Kama umeachwa usione aibu, ongea na ndugu na jamaa zako na uwambie ukweli kuhusu yaliyokutokea, hii itakufanya upunguze mzigo wa nawazo kichwani kwako na utahisi hali ya wepesi moyoni mwako hasa kwa ushauri utakaopata. Pia unaweza kuwaona wataalamu wa ushauri kwa ushauri zaidi.

Usitafute mpenzi mwingine kuziba pengo lake haraka.:
Watu wengi huchukua wapenzi wapya haraka ili kuzuia maumivu lakini hii sio njia sahihi kwani siku maumivu yako yakiisha utagundua kwamba hauna mapenzi ya kweli juu ya huyu mpenzi wako mpya na utaishia kumuumiza tena huyo uliyemchukua.(mwanamke anaweza kujifunza kumpenda mtu lakini mwanaume asipokupenda mwanzoni hawezi kujifunza kukupenda hata iweje)

Andika mapungufu yake kwenye karatasi:
Jaribu kukumbuka matatizo na mapungufu ya huyo mpenzi wako hii itakufanya uone kwamba hakuna madhara uliyoyapata ila faida na itakupunguzia machungu yako.

Msamehe mpenzi wako ata kama hajakuomba msamaha:
Njia pekee ya kua huru kihisia ni kusamehe, visasi moyoni havitakusaidia kabisa kuondokana na maumivu na utajikuta unawaza kufanya mambo ya ajabu ambayo yanaweza kukuletea matatizo ikiwemo kumuua au kumjeruhi. 

Kaa mbali na vitu vinavyokukumbushia kuhusu mpenzi wako:
Sikiliza nyimbo mpya, weka mbali picha zake na zawadi zote alizokupa, usitembelee sehemu ambazo zinakukumbusha kuhusu yeye. Kua na marafiki wapya ambao hawakumfahamu mpenzi wako.(simaanishi uwaache marafiki wa zamani), pia usijaribu kua rafiki wa mpenzi uliyeachana nae kwani utajikuta unaumia zaidi labda baadae sana ukishasahau.

Usiseme mabaya kuhusu mpenzi wako au familia yake:
Hii ni hali ya mpito tu, ukianza kupost vitu vya ajabu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano yako haitakusaidia kitu bali kujiabisha kwa jamii na siku maumivu yakiisha utajuta sana kwanini uliandika mambo hayo. Hili ni tatizo sugu kwa watu wengi walioachana kupost vitu kama kumkomesha mpenzi wake wa zamani. Naomba nikwambie mapenzi hayana kisasi kama umeachwa, umeachwa tu. kumbuka silence is the best weapon..

Fikiria faida za kuishi bila mpenzi:
Kua peke yako kuna faida nyingi ikiwemo kua huru na maamuzi yako, kuchagua marafiki unaotaka, kujikinga na magonjwa ya zinaa,kuishi maisha unayotaka bila kuhofia kukosolewa, unaweza kuzima simu yako ata wiki nzima bila hofu, kulala peke yako bila bugudha, kupunguza msongo wa mawazo ambao hutokana na ugomvi wa mara kwa mara.

tumia dawa za kupunguza mawazo; wakati mwingine maumivu ya kuachana na mpenzi yanaweza kua makali sana, mtu akshindwa kupata usingizi, kufanya kazi zake, kukosa furaha kabisa na kulia kila siku. hii huathiri sana mfumo wa maisha husika na huweza kusababisha mtu kuamua kujiua kabisa kama mnavyosikia watu waliojiua sababu ya mapenzi. ndio maana kuna dawa maalumu za watu wenye msongo wa mawazo. ukitumia dawa hii mwili unatulia na ubongo unapumzika sana. itakupa usingizi na kila ukiamka unakua na furaha upya na unaendelea na maisha yako kama kawaida. dawa hizi zinaharakisha sana kusahau na kuendelea na maisha yako haraka kuliko kujaribu kupambana mwenyewe.mfano wa dawa hizo ni bupropion,clomipramine na doxepin. zinapatikana maduka makubwa ya madawa kwa gharama kubwa kidogo lakini ni bora kuliko kuendelea kupoteza muda kumuwaza mtu ambaye hakutaki tena kwani hiyo ni gharama kubwa zaidi.

Amini utapata mwingine;
Katika dunia hii hakuna mtu alizaliwa kwa ajili ya mtu fulani..kila mtu anaweza kutengeneza mahusiano na mtu yeyote Yule na yakawa mazuri..jipe mda wa kutosha usiwe na haraka fanya mambo yako.. BELIVE ME, ANOTHER TIME WIL COME..NEW LIFE, NEW LOVE AND NEW HAPPYNESS.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                     Mawasiliano 0653095635/0769846183

                                                  STAY ALIVE…..
                                  DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO