data:post.body HIZI NDIZO DAWA KUMI AMBAZO HAZITUMIKI KABISA KIPINDI CHA UJAUZITO… ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIZO DAWA KUMI AMBAZO HAZITUMIKI KABISA KIPINDI CHA UJAUZITO…                                                           


Tunaendelea na makala zetu za siri za afya bora na leo tutaongelea dawa ambazo jamii yetu huzitumia mara kwa mara kujitibu magonjwa mbalimbali na hupatikana kirahisi mtaani
Lakini  bahati mbaya baadhi ya dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito kabisa kulingana na madhara makubwa yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.


 • Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo mebendazole hutumika kama mbadala.

 • Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza kusababisha mototo kuzaliwa akiwa hasikii yaani kiziwi.

 • Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa. Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.

 • Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na kusababisha kuzaliwa na motto mwenye viungo pungufu au zaidi.

 • Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya mtoto[organogenesis} na kutoa motto asiye na viungo vya kawaida.

 • Metronidazole au fragile; hii dawa ipo kwenye kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa utengenezaji wa viungo vya mtoto.

 • Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye kikundi maarufu cha prostanglandins analogue, hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu madonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno ikiwemo kutoa mimba kabisa.

 • Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.

 • Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa mtoto.

 • Furesamide: hii ni dawa ambayo inapatikana kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha chini kabisa[intravascular volume depletion].

Mwisho: usitumie dawa yeyote kipindi cha ujauzito bila ushauri wa daktari kwani ni hatari sana kwa maisha yako na mtoto wako kwa ujumla...tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga


                              Mawasiliano: 0653095635/0769846183
 
                                             STAY ALIVE…
                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

Maoni 22 :

 1. Ikiwa nilikutana na mume wangu jana alafu leo ilikuwa ndio siku yangu ya kupata hedhi na cjaiona inawezekana kupata ujauzito?

  JibuFuta
 2. Tumbo langu lina gesi na nina ujauzito wa miez 2 je nisitumie dawa za gesi?

  JibuFuta
 3. Tumbo langu lina gesi na nina ujauzito wa miez 2 je nisitumie dawa za gesi?

  JibuFuta
 4. Inategemea kwan dalili za kuingia kwenye hedhi yko umeziona na kama umeziona sio rahis kupata yai linakua limesha jiengua tayar kutoa bleed

  JibuFuta
 5. Je ukitumia flagil cku mbili baada ya mimba kutunga inaweza haribika mimba??

  JibuFuta
  Majibu
  1. ndio fragile sio dawa nzuri kipindi cha ujauzito

   Futa
 6. kama MTU katumua cipro na doxy akiwa hajajijua kma mjamzito anaweza kupatiwa tiba ya haraka kuzuia madhara yasimpata mtoto

  JibuFuta
 7. Dawa gani atumie akiwa anasikia maumivu makubwa tumboni wakati kasha toa mimba na miguu anahisi kuwaka moto??

  JibuFuta
  Majibu
  1. ni vizuri kwenda hospitali kuhakikisha kama mimba imetoka yote, hata hivyo anatakiwa atumie fragile na amoxicilline baada ya kutoa mimba.

   Futa
 8. Wliouliza wnapataje majibu mbona naona maswali na hakuna majibu na nikibofya kwenye jibu haifunguki

  JibuFuta
 9. Doctor nauliza nilipata hedhi mara mbili ndani ya mwmwe mmoja na iilinitokea hivyh baada ya kumeza p2 kwa hiyo mzungunguko wa hedhi utakuut umeharibikau

  JibuFuta
 10. nimekutana na mwanaume siku ya Saba baada ya kupata hedhi inawezekana nikawa mjamzito?

  JibuFuta
 11. Naomba kujua,nimeanz kuon hedh trh 12 nikakutan na mwanaume trh 22 nip hatarin au

  JibuFuta
 12. Naomba kujua nilianza hedh tar8/12/2019 had trh 12 katikat ya mwez was kumi na mbili nikameza p2 tarehe 11 nikakutana na mwanaume nipo hatarin au

  JibuFuta
 13. Je ni dalili gan hutokea akati tayari kameza vidonge vya kutoa mimba

  JibuFuta
 14. Nilipata hedhi tar 21 nkakutan n mwanaume tar 4 j ntapat mimba??

  JibuFuta
 15. Mimi nilifanya mapenzi nikiwa kwwnye siku Zangu toka Apo sijaingia kwenye siku Zangu saiv Nina mienzi mitatu naweza pata mimba

  JibuFuta
 16. Mimi ni mjamzito nimemez dox jan zitaleta madhara

  JibuFuta