data:post.body Desemba 2014 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
 • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIZO DAWA KUMI AMBAZO HAZITUMIKI KABISA KIPINDI CHA UJAUZITO…                                                           


Tunaendelea na makala zetu za siri za afya bora na leo tutaongelea dawa ambazo jamii yetu huzitumia mara kwa mara kujitibu magonjwa mbalimbali na hupatikana kirahisi mtaani
Lakini  bahati mbaya baadhi ya dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito kabisa kulingana na madhara makubwa yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.


 • Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo mebendazole hutumika kama mbadala.

 • Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza kusababisha mototo kuzaliwa akiwa hasikii yaani kiziwi.

 • Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa. Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.

 • Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na kusababisha kuzaliwa na motto mwenye viungo pungufu au zaidi.

 • Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya mtoto[organogenesis} na kutoa motto asiye na viungo vya kawaida.

 • Metronidazole au fragile; hii dawa ipo kwenye kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa utengenezaji wa viungo vya mtoto.

 • Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye kikundi maarufu cha prostanglandins analogue, hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu madonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno ikiwemo kutoa mimba kabisa.

 • Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.

 • Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa mtoto.

 • Furesamide: hii ni dawa ambayo inapatikana kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha chini kabisa[intravascular volume depletion].

Mwisho: usitumie dawa yeyote kipindi cha ujauzito bila ushauri wa daktari kwani ni hatari sana kwa maisha yako na mtoto wako kwa ujumla...tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga


                              Mawasiliano: 0653095635/0769846183
 
                                             STAY ALIVE…
                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO