data:post.body HIZI NDIO HATUA TANO MUHIMU ZA KIFO { FIVE STAGES OF DEATH}.. ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HIZI NDIO HATUA TANO MUHIMU ZA KIFO { FIVE STAGES OF DEATH}..                                                                    
Katika moja ya makala zilizopita tuliwahi kuongelea dalili muhimu za kifo ambazo ukiziona kwa binadamu yeyote kuna uwezekano mkubwa wa kua amepoteza maisha tayari..
Lakini pia kabla binadamu yeyote ambaye alikua anaumwa hajafa kuna hatua kadhaa za kisaikolojia ambazo lazima azipitie kabla ya kupoteza maisha kabisa..

Zifuatazo ni hatua hizo muhimu
Rejection: hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo mgonjwa mfano anasumbuliwa na kansa labda ya damu akiambiwa kwamba atakufa, hukataa kabisa na hatakubaliana na kauli za madaktari au ukweli halisi kwani anaamini bado atapona japokua ugonjwa wake hautibiki..

Anger: hii ni hatua ya pili ambayo mgonjwa ameshagundua kabisa kwamba atakufa lakini matokeo yake hua na hasira sana, kujutia nafsi yake hata kumlaani mungu na baadhi ya watu ambao binafsi anahisi wamehusika na kifo chake.

Bargaining: hii ni hatua ya tatu muhimu ambayo mgonjwa huyu huanza kuomba msaada ili kujua kama  labda kuna tiba mbadala au suluhisho lingine la tatizo lake, kipindi hiki hua mpole na mnyenyekevu sana.

Depression;  hatua hii ya nne mgonjwa hukata tamaa kabisa na kua na mgandamizo mkubwa wa mawazo, mara nyingi hua haongei tena huku akitumia mda mwingi kutafakari labda huko kaburini kukoje, itakuaje ndugu zake na familia kwa ujumla siku kifo kikifika, kama kuna maisha mengine baada ya kifo na kadhalika.

Acceptance: hii ni hatua ya mwisho ambayo mgonjwa hukubaliana na ukweli wa mambo kwamba lazima afe hata iweje. Kipindi hiki mgonjwa hua na furaha kama kawaida na mara nyingi hupenda kuomba aletewe viongozi wa kiroho ili wamuombee huku aendako, pia huanza kuandika urithi na kuweka mambo yake sawa kabla ya kifo.

Mwisho: ni busara sana kuishi vizuri na watu kwasababu kifo kinakuja kwa kila binadamu{ death will come to all men}.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga


                                                            MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                             
                                                                    STAY ALIVE

0 maoni:

Chapisha Maoni