data:post.body Novemba 2014 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

HIZI NDIO SABABU KUMI ZINAZOKUFANYA UENDELEE KUISHIWA NGUVU ZA KIUME


                                                                       
Nguvu za kiume ni nini? Huu ni uwezo wa mwanaume kusimamaisha uume wake na kustahimili kwa mda mrefu wakati wa faragha bila wasiwasi wowote…
Kama nilivyoongelea kipindi cha nyuma wanaume wengi wanasumbuliwa na tatizo hili kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.
Idadi kubwa ya watu wamaekua wakihangaika sana na kudanganywa na waganga wa kienyeji kwamba watapona kabisa.
Lakini kuna sababu kadhaa za kibinadamu ambazo uchunguzi wa kitaalamu unaonyesha zinasababisha tatizo hilo kama ifuatavyo…
·         Uvutaji wa sigara:
Hii ina kimelea cha kemikali kwa jina la nicotin ambacho huharibu mishipa ya damu na ile ya fahamu na kukufanya kua mlegevu kabisa wakati wa tendo la ndoa…

·         Ulevi uliopitiliza:
Unywaji wa pombe sana huharibu mishipa ya fahamu yote ya binadamu, ndio maana mtu akishalewa hata akiumia hasikii kwasababu kwa kipindi kile mishipa hiyo ya fahamu haifanyi kazi sawasawa.

·         Kutokufanya mazoezi:
Mwili untegemewa kua safi sana pale damu inapozunguka kila sehemu na kusafisha kila kitu ikiwemo na sumu za vyakula tunavyokula. Usafi huu hufanya mwili kua safi kila Nyanja ikiwemo na nguvu za kiume hivyo kama hufanyi mazoezi huwezi kupata faida hizi.

·         Uzito uliopitiliza:
Kwa jamii zetu za kiafrika kitambi ni kama sifa, lakini naomba nikwambie mtu mwenye kitambi ni mgonjwa na husumbuliwa sana na tatizo la nguvu za kiume kwani uzito alionao humchosha sana na kulala akiwa hoi.

·         Kufanya ngono mara kwa mara na upigaji wa punyeto:
Hamu ya kulala na mwanamke ni kama ulaji wa chakula, tunaamini mtu mwenye njaa kali ndio atakula sana. Hivyo ukifanya ngono na kupiga punyeto mara kwa mara hutakua na hamu ya ngono na nguvu za kiume hutaziona kabisa.

·         Maumivu makali ya mwili na mgandamizo wa mawazo:
tendo la ndoa ni la starehe hivyo linaenda vizuri mwili ukiwa safi kabisa bila shida yeyote . kama unasumbuliwa na maumivu ya mwili ya aina yeyote ile au maumivu ya kisaikolojia kama kuachwa, kufiwa au kukosa kazi basi hautakua na nguvu za kiume za kutosha.

·         Njaa wakati wa tendo la ndoa:
Najua watu wengi watashangazwa na hii pointi, lakini napenda ujue kwamba mwili wa binadamu unajua kutoa vipaumbele. Kama una njaa sana mwili hautahangaika na nguvu zako za kiume kwasababu kuna mambo mengi muhimu ya kufanyika kwenye ubongo.

·         Kulala na mwanamke mchafu na ambaye humpendi:
Naomba utambue kwamba nguvu za kiume si mwili tu, bali hata saikolojia..
Nguvu za kiume huambatana na mapenzi kutoka moyoni kwenda kwa mwanamke husika na usafi wake binafsi. Usitegemee kulala na mwanamke huku umeshika pua kuzuia harufu kali afu upate nguvu za kiume.

·         Ugomvi wa mara kwa mara na mwenza wako:
Kama mahusiano yako na mwenza wako yana matatizo kimsingi mtakua mnaingia faragha na vinyongo moyoni , hali hii hupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa na kuendelea kuishiwa nguvu za kiume.

·         Kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume hovyo:
Dawa za kuongeza nguvu za kiume kama Viagra zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya watu flani na humezwa chini ya usimamizi wa daktari. Wewe unayezimeza hovyo unakosa imani na nguvu zako kiasi kwamba ukizikosa dawa hizo hufanyi kitu kabisa.

Mwisho:  tafuta suluhisho ya tabia nilizozitaja hapo juu na nguvu zako za kiume za mwanzo zitarudi na utaishi kwa amani, usidanganyike na waganga wa kienyeji watamaliza pesa zako. kwa maelezo zaidi na ushauri soma hapa
                                                 tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                               
                       MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                         
                    DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

                                      STAY ALIVE


      



HIZI NDIO NJIA SABA ZA KUACHA PUNYETO KABISA...

                                                                   

Karibuni tena wapendwa wasomaji wa blog hii ya siri za afya bora na kama kawaida leo tena unapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na kiafya..
Makala iliyopita niliongelea madhara yanayosababishwa na kupiga punyeto kama hukusoma hii hapa .https://sirizaafyabora.blogspot.com/2014/11/haya-ndio-madhara-kumi-ya-kupiga.html/haya-ndio-madhara-kumi-ya-kupiga.htmllakini nilipokea simu nyingi ambazo zilitaka pia niongelee suluhisho au jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto kabisa
Punyeto kama tulivyoongea ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote. FANYA YAFUATAYO....                                                  
  •  Acha kuangalia video za ponograph: video hizi ndio chanzo  kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo  na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo  kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako..                                                             Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.
  •  Epuka kukaa nyumbani peke yako; mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
  • Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa, kuishiwa nguvu za kiume na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
  • acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.
  • Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi atakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto. pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.
  • anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine:hii itakufanya ue bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko,  pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala.
  •  mwisho bonyeza hapa kusoma kuhusu matibabu ya ya nguvu za kiume kwa waathirika wa punyeto https://sirizaafyabora.blogspot.com/2015/05/yajue-matibabu-ya-nguvu-za-kiume-kwa.html                                                                                                                                                                                  
                                                             STAY ALIVE

                                  MAWASILIANO 0653095635/0769846183[tuma meseji tafadhali]

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO


HAYA NDIO MADHARA 11 YA KUPIGA PUNYETO…..{ MASTURBATION}




Punyeto ni nini?
Hii ni tabia ambayo mwanamke au mwanaume anajichua sehemu za siri ili kufika kileleni, mara nyingi kitendo hiki hufanyika na muhusika akiwa peke yake chumbani au bafuni.
Wahanga wengi wa tabia hii ni wanaume kwani huanza katika umri mdogo sana kwasababu ya uoga wa kufuata wasichana na kuangalia video za ngono ambazo huwasukuma kufanya vitendo hivi..
Lakini punyeto huambatana na madhara makubwa ya kijamii na kiafya na leo tutaangalia madhara hayo kumi ya punyeto..
  uchovu; baada ya kujichua watu wengi husikia uchovu mkubwa na kupitiwa na usingizi, hii inaweza kuathiri uwezo wako wa kazi au masomo na pia kama wewe unajichua kila siku basi muda mwingi utakua mlegevu tu.
hupoteza nguvu za kiume; somo la nguvu za kiume ni pana sana, yaani sababu za kupoteza nguvu za kiume hua ni nyingi ni lakini inapokuja kwenye punyeto mara nyingi mfanyaji hupoteza hamu ya tendo la ndoa yaani muda wote amaeridhika tofauti na watu ambao hawafanyi tendo hili ambao muda mwingi wanakua na uchu, lakini pia matumizi ya mikono migumu huweza kukuumiza na kuharibu mishipa ya fahamu inayoenda kwenye uume.
utasa wa muda kwa wanaume[temporaly sterility]; punyeto hupunguza sana kiasi cha mbegu kinachopatikana kwenye korodani, mtu anayejichua sana inafika hatua anatoa mbegu kidogo sana ambazo zinakua hazijakomaa kumpa mwanamke mimba.
kusahau sana; watu wengi wanaopiga punyeto wana tatizo la kusahau vitu vodogo vidogo yani short term memory yaani anaweza kuweka simu mezani afu akasahau ameiweka wapi, haifahamiki chanzo kikuu ni nini lakini madhara haya yameonekana wa wahanga.
kumwaga mbegu haraka[premature ejaculation]; watu wanaojichua mara nyingi hutumia muda mfupi sana ili kukidhi haja zao na kuendelea na mambo yao, ukizoea hali hii utamwaga haraka sana siku ukikutana na mwanamke halisi.
hali hii ni mbaya na hutia aibu kwani hutaweza kumridhisha mwanamke yeyote.
msongo wa mawazo; watu wanaopiga punyeto hua wana akili moja, hudhani kwamba leo wanafanya mara ya mwisho na hawatarudia tena, kitu ambacho sio kweli.
mara nyingi hujikuta wanarudia na kujuta sana baada ya kufikia mshindo.
utumwa(addiction); ukishaanza punyeto sio rahisi kuacha japokua inawezekana, muhanga hawezi kukaa muda mrefu asu siku nyingi bila kujichua na ili akili yake ikae sawa itabidi aende sehemu ajichue ili aweze kua kawaida..
huharibu mahusiano; punyeto huweza kufanya wapenzi kutokua na hamu ya kingono kabisa baina yao, kwani kila mtu anajiridhisha kivyavyake.
kutokuwepo na mahusiano mazuri ya tendo la ndoa ni moja ya sababu kuu ya kuharibika kwa mahusiano mengi.
uoga wa kutongoza; wanaume wanaojichua hawajiamini hata kidogo hivyo kusimama na kumfuata msichana ni ngumu sana sababu hawana kiu kubwa sana ya kua na mwanamke, hii ni kwasababu wanaweza kujitosheleza wenyewe.
huchochea mapenzi ya jinsia moja; mara nyigi wanawake hutumia vifaa mbalimbali kujichua, sehemu ambazo wanaishi wanawake watupu kama shule za wasichana vifaa vile inabidi vivaliwe na msichana mmoja ili kumsaidia mwenzake na hapo ndipo wanaanza kutamaniana na kuanza mahusiano ya kudumu.
ajali wakati wa kujichua; hasa upande wa wanawake na mashoga, siku hizi kuna ajali nyingi ambazo hutokea wakati wa tendo hili la kujichua hasa pale vifaa ambavyo sio rasmi kama ndizi, tango, au chupa zinapokataa kutoka ndani ya uke au sehemu ya haja kubwa. hali hii huweza kuhitaji upasuaji mkubwa kundoa vitu hivyo.
kama umeshindwa kabisa kuacha punyeto soma hapa...http://www.sirizaafyabora.info/2014/11/hizi-ndio-njia-saba-za-kuacha-punyeto.html
Mwisho: acha punyeto na uanze maisha mapya kiakili, kimwili na kiroho na acha kusema hii ndio punyeto ya mwisho sitarudia tena,  acha mara moja…
                                   

                                  MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                                 
                                                                STAY ALIVE 

                                       DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO

HII NDIO JINSI YA KUZUIA UJAUZITO KWA KUTUMIA MTOTO…..



                                                        
    
Makala zilizopita zimetaja njia nyingi za uzazi wa mpango ambazo zinaweza kutumika kupanga uzazi kwa mwanamke ikiwemo faida zake na hasara zake.
Leo katika mtiririko wa njia za uzazi wa mpango tutaongelea njia  ya kuzuia mimba kwa kunyonyesha mtoto mdogo baada ya kujifungua.

Njia hii inafanyaje kazi?
Tafiti zinaonyesha kwamba mama baada ya kujifungua huchelewa kupata siku zake za mwezi na kipindi hiki kunakua na homoni nyingi kitaalamu kama prolactin hormone ambazo hufanya kazi kinyume na homoni za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo ndizo chanzo kikuu cha kuruhusu yai kwa ajili ya kutunga mimba.
Homoni hii ya prolactin kazi yake kubwa ni kuruhusu utengenezwaji na kuruhusu maziwa ya mama kutoka ili mtoto anyonye..

Uhakika wa njia hii..
Njia hii ina uhakika wa kufanya kazi kwa asilimia 98 bila kusababisha ujauzito kwa mtu anayeitumia ila tu afuate masharti yote yanayohusika na njia hii ya uzazi wa mpango.

  
         Masharti hayo ni yapi?
  • ·         Mtoto awe ananyonya maziwa ya mama tu: kunyonya huku ndo kutafanya homoni hii ya prolactin kuendelea kuzuia hizi homoni zingine za uzazi kufanya kazi, hivyo mama anashauriwa amnyonyeshe mtoto wake angalau kila baada ya masaa manne.
  • ·         Mama awe hajaona siku zake kabisa baada ya kujifungua: kama mama ameshaona siku zake ni dalili ya wazi kwamba homoni za uzazi zimeanza kazi hivyo asitumie kabisa njia hii.
  • ·         Miezi sita iwe haijapita baada ya kujifungua:  baada ya miezi sita kuna uwezekano mkubwa wa homoni za uzazi kuanza kazi hivyo kama miezi sita imepita mama anashauriwa atumie njia zingine za uzazi wa mpango kama kondomu.
       Madhara ya njia hii…
·         Njia hii haina madhara yeyote kiafya ila hutegemea sana unyonyeshwaji wa mtoto hivyo mama   akizembea kunyonyesha kama alivyoelekezwa anaweza kubeba mimba nyingine..tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
                                 MAWASILIANO 0653095635/ O769846183…
                                                     STAY ALIVE