data:post.body JINSI KUZUIA MIMBA KUTUNGA BAADA YA KUFANYA NGONO BILA KINGA.{EMERGENCY CONTRACEPTIVES PILLS] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

JINSI KUZUIA MIMBA KUTUNGA BAADA YA KUFANYA NGONO BILA KINGA.{EMERGENCY CONTRACEPTIVES PILLS]

                                       


Karibuni tena ndugu wasomaji wa SIRI ZA AFYA BORA, Kama tulivyosema mara ya mwisho kwamba tutakua tukiongelea makala za uzazi wa mpango kwa mda flani ili kuweka swala hili sawa kwa watu ambao hawafahamu.
Leo tutakua tukiongelea jinsi ya kuzuia ujauzito kama njia ya uzazi wa mpango kwa mwanamke aliyetembea na mwanaume na kua na wasiwasi amebeba mimba baada ya tendo hilo.

 Mwanamke huyu ni yupi?
  • ·         Ambaye hakutumia kinga wakati wa tendo la ndoa.
  • ·         Ambaye amebakwa au kulazimishwa kingono
  • ·         Ambaye kondomu imepasuka wakati wa tendo la ndoa.
  • ·         Ambaye ametumia vibaya njia yake ya uzazi wa mpango kama sindano au vidonge.
  • ·         Kama mwanaume alishindwa kuchomoa wakati wa kutoa mbegu.

Jinsi ya kutumia dawa baada ya matukio hayo.
dawa hizo zinatakiwa zitumike ndani ya siku tatu baada ya makosa hayo hapo juu kufanyika.
Dawa hii hufanya kazi ya kuchelewesha yai kushuka kwenye mfuko wa uzazi ili mbegu za kiume zikutwe zimeshakufa.

Dawa hizo ni zipi?
dawa  nzuri kuliko zote inaitwa p2, inapatikana maduka ya madawa.meza kidonge kimoja kisha meza kingine baada ya masaa 12 na utakua salama.

Madhara madogo madogo ya dawa hizo…
  • ·         Kichefuchefu
  • ·         Tumbo kuuma
  • ·         Kuchoka sana
  • ·         Kichwa kuuma
  • ·         Kizunguzungu
  • ·         Kutapika
  • ·         Maumivu ya matiti.
kwa maelezo zaidi bonyeza maneno ya kijani hapa hap kusoma.

SECRETS OF GOOD HEALTH

                                                         STAY ALIVE
                                           MAWASILIANO 0653095635/0769846183

Maoni 6 :

  1. nimeelewa kwa nguvubya tano

    JibuFuta
  2. Je ni sawa kumeza dawa izo zaidi ya mara moja kwa mwez .....

    JibuFuta
  3. Ahsante saana kwa mafundisho adimu, mungu akubariki kwa huduma bora,

    JibuFuta
  4. Plse dr, Nina mpenzi ana tatizo la kutofill anythings, pale mnapokuwa falagha, yani hadi una maliza tendo yeye haisi chochote na imefika mahali amejikatia tamaa, plse Naomba msaada wako kaka,

    JibuFuta
  5. Mi2 nimemeza baada ya masaa 24 je inaweza kusaidia?

    JibuFuta