Wasomaji na wafuatiliaji wa siri za afya bora leo
tunaendelea na mtiririko wa elimu ya uzazi wa mpango ..na kama kawaida leo
tutaongelea njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa mwanamke ya kufunga uzazi
kabisa kitaalamu kama BILATERAL TUBE LIGATION.
Njia hii ikoje?
Hii ni njia ambayo mirija inayopitisha mayai ya kike kutoka
yanapotengenezwa {ovary} mpaka kwenye
mfuko wa uzazi inafungwa kabisa kwa njia ya upasuaji ili kuzuia mfumo huu, na mwanamke hawezi
kubeba mimba tena.
Hii ni njia nzuri kwa wale ambao hawahitaji kua na watoto
tena na ina uhakika wa zaidi ya 99%.
Mwanamke gani
anatakiwa kufanyiwa?
Mwanamke yeyote ambaye yuko tayari na ameridhia njia hii ya
uzazi wa mpango.
Faida za njia hii ya
uzazi wa mpango..
- · ni njia ya moja kwa moja.[permanent}
- · Haihitaji kukumbuka chochote ukishafanyiwa upasuaji.
- · Haina madhara yeyote.
- · Haiharibu ladha ya tendo la ndoa.
- · Haizuii kunyonyesha wala kuharibu ubora wa maziwa ya mtoto.
- · Ina uhakika mkubwa wa kuzuia mimba.
Madhara ya njia hii…
Hakuna madhara yeyote ya njia hii kama inavyodanganywa na
wengi mtaani cha msingi ue umeamua kwa uhakika kwani mirija ikishafungwa haiwezi kufunguliwa tena..
STAY ALIVE
0 maoni:
Chapisha Maoni