Vijiti ni nini?
Hii ni moja ya njia ya uzazi wa mpango ambayo kipande kidogo
chembamba cha plastiki ambacho kinakua na homoni ya progesterone kinawekwa
ndani ya mkono wa juu.
Upasuaji mdogo usio na maumivu hufanyika kuweka vijiti
hivyo..
Aina za vijiti..
Kuna aina kuu mbili za vijiti ambazo ni.
·
Implanon:
Hii ni aina ya kijiti ambayo huwekwa moja
kwenye mkono na huzuia mimba kwa uhakika kwa mda wa miaka miatatu.
·
Jadelle:
Hii ni aina ya vijiti ambavyo huwekwa
viwili kwa wakati mmoja na huweza kuzuia mimba kwa mda wa miaka mitano.
Jinsi vijiti vinavyofanya kazi..
·
Huzuia mbegu kutoka kwenye ovari kushuka kwenye
mfuko wa uzazi kukutana na mbegu za kiume.
·
Huongeza utepe kwenye mlango wa uzazi kuzuia
mbegu za kiume kuingia kwenye mfuko wa uzazi..
Faida za kutumia vijiti kama uzazi wa mpango..
- · Huzuia kupungua kwa wingi wa damu{iron dificiency anaemia} kwasababu huzuia damu ya kila mwezi kutoka.
- · Haiharibu au kupunguza ubora wa maziwa.
- · Ni njia ya uhakika.
- · Inazuia mimba kwa miaka mingi.
- · Sio rahisi mtu mwingine kufahamu kama unatumia njia hiyo.
- ukitoa kijiti tu unaweza kubeba mimba kwa mda mfupi..
Madhara madogo madogo ya njia hiyo ya uzazi wa mpango.
- · Kubadilika kwa mfumo wa kutoka damu mwisho wa mwezi kama kutoka damu nyingi sana, matone ya damu au kukata kabisa kwa damu.
- · Maumivu ya tumbo na kichwa..
- · Maumivu ya matiti,
- · Kuongezeka uzito.
- · Kuongezeka au kuisha kabisa kabisa kwa chunusi.
Mwisho: hii ni moja ya njia bora zaidi za
uzazi wa mpango kwasababu haina usumbufu kabisa mpaka miaka mitatu au mitano
iishe lakini unaruhusiwa kuondoa kama ukihitaji mototo kabla mda uliopangwa
haujaisha.
Ukipata matatizo yeyote makubwa muone
daktari haraka..
STAY ALIVE
Je baada ya kutoa hivyo vijiti kabda ya 3yrs unaweza kupoteza hedhi na huna mimba? I mean ukawa haubleed tangu day utoe hiyo kijiti
JibuFutaMoza Masoud
Futaje hivi vijiti vina weza kusababisha kuvimaba kwa ngozi yani kama umepitiwa na mdudu na kwashwa?
JibuFutaNdan ya mdagan kijiti kinaanza kufanya kaz mwilin
JibuFutaAngel benard
Futakwanini kijiti huzuia kutoka damu ya mwezi
JibuFutaAsante kwa somo zuri mimi natumia njia ya vijiti na nimesoma kuwa njia hii inaweza kukupa chunusi na mimi nina tatizo hilo nimekuwa na chunusi nyingi tofauti na awali. Je kuna dawa ya kuweza kuondoa tatizo hili?
JibuFutaMimi tangu nimeweka sijisikii vizuri.kichwa kinauma.nakonda
JibuFutaMim ndio kwanza nimiweka yan ndio mara yang ya kwanza na leo ni siku ya 4 ..nmeanza kuskia kma tumbo kuuma.
JibuFutaNatumia njia hiyo ya kijiti nikiwa nafanya tendon LA ndoa naumia sana toka niweke wakat kabla cjaweka nilikuwa nipo vzur
JibuFutaMm baitumia hii njia na niko vizur tu. Labda kuongezeka uzito ingaw sidhani km imesababishwa na vijiti
JibuFutaMimi tangu niweke njiti nimekonda sana
JibuFutaMm nimeanza kutumia mwezi wa9 mwaka huu nableed mwezi mzima je nifanyeje
JibuFutaHalafu nataka nifanye mazoezi maana nimenenepa Sana je sio tatizo, watu wananiambia nisifanye mazoezi vijiti havitaki shida, shida je nikweli?
JibuFutaHatuoni majibu ya maswali yalioulizwa
JibuFuta