data:post.body Oktoba 2014 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

JINSI YA KUPANGA UZAZI KWA MWANAUME KWA NJIA YA UPASUAJI{VASECTOMY]….



                                                

Habari za zenu ndugu wasomaji, natumaini mnaendelea na shughuli zenu za kila siku kama kawaida.
Katika mtiririko wetu wa makala za uzazi wa mpango, leo tutaongelea uzazi wa mpango kwa mwanaume.
Watu wengi hua hawajui kama mwanaume pia anahusika pia kufungwa mirija kama ilivyo mwanamke ili asiweze kumpa mimba mwanamke tena na baada ya hapo kuishi maisha ya kawaida kabisa..

Njia hii ni imekua ngumu kidogo kupokelewa kwa tamaduni za kiafrika labda kwa sababu ya imani zilizopo na wanaume kutoathirika moja kwa moja na tatizo la kubeba mimba nyingi..

Jinsi ya kufanya upasuaji..
Upasuaji huu hufanyika kwenye korodani na mirija inayopeleka mbegu za kiume kutoka kwenye korodani kwenda kwenye uume kitaalamu kama vas deferens hukatwa kabisa kuzuia mfumo huo wa uzazi..
Mwanaume huweza kuendelea na shughuli zake za kawaida baada ya wiki moja tu.

Madhara ya njia hii ya uzazi wa mpango..
Yapo madhara madogo madogo ya njia hii ya uzazi wa mpango kama kutokwa na damu, maumivu, na kidonda kuchelewa kupona kwasababu ya kuingiliwa na bacteria{ infection}.
Lakini madhara haya haya huweza kutibika kirahisi sana..

Baada ya upasuaji
Upasuaji huu ni wa moja kwa moja yaani hautaweza kumpa kwanamke mimba tena hivyo ni vizuri kua na uhakika kabla hujaamua kushiriki njia hii,
Ni nchi chache zilizoendelea zilizofanikiwa kurudisha mirija hiyo tena lakini bado uwezekano wa kumpa mwanamke mimba unakua chini yaasilimia 55.
Mwisho; hii ni moja ya njia bora za uzazi wa mpango ambazo hazina madhara kabisa kiafya na huweza kutumika mda na wakati wowote muhusika anapokua tayari..tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga


                                         STAY ALIVE

HIZI NDIO HATUA NANE MUHIMU ZA UVAAJI WA KONDOMU YA KIUME...

                                                                  



Najua wengi wenu mnahisi au mnadhani mnajua sana kutumia condom kuliko kawaida lakini leo naomba niwakumbushe kutumia zana hii na kuwaamsha ambao hawazitumii kabisa.
Pia natoa rai  kwamba condom inazuia magonjwa hatari na mimba ambazo hazikutarajiwa…

Hebu tuone condom ya kiume inavaliwa vipi..

  1. 1.       Hakikisha condom yako haijaisha mda wake wa matumizi yaani expire date, kwan condom iliopitwa na wakati hua inashuka kiwango na uwezo wa kukulinda unakua mdogo sana.
  1. 2.       Fungua taratibu condom yako kwa kuikata sehemu laini ya juu bila kutumia kucha au wembe  isije ikaipasuka.
  1. 3.       Toa condom yako na kwa umakini mkubwa jiandae kuivaa.
  1. 4.       Anza kuvaa condom kwa kuweka juu ya kichwa kisha bana chuchu ya condom ili kutoa hewa{kutofanya hivi ndio chanzo cha kupasuka kwa condom nyingi}  
  1. 5.       Kisha ivishe juu ya uume uliosimama na ujiandae kuivaa kwa njia ya kuivingirisha kwenda chini.   Ishushe condom mpaka chini kabisa ya uume tayari kwa tendo la ndo
  1. 6.       Sasa uko tayari kushiriki tendo la ndoa bila wasiwasi wowote.
  1. 7.       Ukishamaliza kutumia condom vua haraka kabla uume haujalala kisha weka vizuri na kutupa kwenye ndoo ya taka au choo cha shimo..
  1. 8.       Usitupe kwenye choo cha kuflash kama hicho kwani condom huweza kuziba mfumo wa kupitisha kinyesi. kwa maelezo zaidi soma hapa kusoma 

    SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                    STAY ALIVE…

                                  MAWASILIANO    0653095635/0769846183

HIZI NDIO NJIA TANO KALI ZA KUPATA MTOTO WA KIUME..



                                                                   
Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango..
Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa sababu hizi.
Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.
Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…
Kitaalamu mbegu  zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa  ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..
Zifuatazo ni njia hizo tano kali…

1.       Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
                    Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka    mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike  na kutengeneza mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA MWEZI UNAOFUATA SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..
                     Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
 Pima joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..
      Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..

2.       Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako..{sperm count}
Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.
Njia zingine za kuongeza mbegu ni
       weka korodani kwenye hali ya ubaridi:
  kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto  hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na  kuwekalaptop kwenye mapaja

    acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi..
 matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.

3.       Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya fertilization na upande mwingine, muingiliano mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume  kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.

4.       Hakikisha mwanamke anafika kileleni:
Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu  zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.

5.       Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation;
Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi  kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation..
                     tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga


                                        MAWASILIANO 0653095635/0769846183
                                                                                         STAY ALIVE..

                                                              DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO[tafadhari tuma meseji]


          karibu kwenye group la watsapp ambalo utakua unapata elimu mbalimbali za afya kama jna kuuliza swali lolote kwa kuchangia shilingi 5000 tu kwa mwezi za kitanzania..gharama hii hulipwa kwa mwaka yaani miezi 12]

HIZI NDIO FAIDA ZA UZAZI WA MPANGO KWA NJIA YA UPASUAJI…


                                                                  

Wasomaji na wafuatiliaji wa siri za afya bora leo tunaendelea na mtiririko wa elimu ya uzazi wa mpango ..na kama kawaida leo tutaongelea njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa mwanamke ya kufunga uzazi kabisa kitaalamu kama BILATERAL TUBE LIGATION.

Njia hii ikoje?
Hii ni njia ambayo mirija inayopitisha mayai ya kike kutoka yanapotengenezwa  {ovary} mpaka kwenye mfuko wa uzazi inafungwa kabisa kwa njia ya upasuaji  ili kuzuia mfumo huu, na mwanamke hawezi kubeba mimba tena.
Hii ni njia nzuri kwa wale ambao hawahitaji kua na watoto tena na ina uhakika wa zaidi ya 99%.

Mwanamke gani anatakiwa kufanyiwa?
Mwanamke yeyote ambaye yuko tayari na ameridhia njia hii ya uzazi wa mpango.

Faida za njia hii ya uzazi wa mpango..
  • ·         ni njia ya moja kwa moja.[permanent}
  • ·         Haihitaji kukumbuka chochote ukishafanyiwa upasuaji.
  • ·         Haina madhara yeyote.
  • ·         Haiharibu ladha ya tendo la ndoa.      
  • ·         Haizuii kunyonyesha wala kuharibu ubora wa maziwa ya mtoto.
  • ·         Ina uhakika mkubwa wa kuzuia mimba.
Madhara ya njia hii…  
Hakuna madhara yeyote ya njia hii kama inavyodanganywa na wengi mtaani cha msingi ue umeamua kwa uhakika kwani mirija ikishafungwa haiwezi kufunguliwa tena..
                                     STAY ALIVE

HIZI NDIO FAIDA NA HASARA ZA MATUMIZI YA VIJITI KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO……..


                                                

Vijiti ni nini?
Hii ni moja ya njia ya uzazi wa mpango ambayo kipande kidogo chembamba cha plastiki ambacho kinakua na homoni ya progesterone kinawekwa ndani ya mkono wa juu.
Upasuaji mdogo usio na maumivu hufanyika kuweka vijiti hivyo..

Aina za vijiti..
Kuna aina kuu mbili za vijiti ambazo ni.

·         Implanon:
Hii ni aina ya kijiti ambayo huwekwa moja kwenye mkono na huzuia mimba kwa uhakika kwa mda wa miaka miatatu.

·         Jadelle:
Hii ni aina ya vijiti ambavyo huwekwa viwili kwa wakati mmoja na huweza kuzuia mimba kwa mda wa miaka mitano.

Jinsi vijiti vinavyofanya kazi..
·         Huzuia mbegu kutoka kwenye ovari kushuka kwenye mfuko wa uzazi kukutana na mbegu za kiume.
·         Huongeza utepe kwenye mlango wa uzazi kuzuia mbegu za kiume kuingia kwenye mfuko wa uzazi..

Faida za kutumia vijiti kama uzazi wa mpango..
  • ·         Huzuia kupungua kwa wingi wa damu{iron dificiency anaemia} kwasababu huzuia damu ya kila mwezi kutoka.
  • ·         Haiharibu au kupunguza ubora wa maziwa.
  • ·         Ni njia ya uhakika.
  • ·         Inazuia mimba kwa miaka mingi.
  • ·         Sio rahisi mtu mwingine kufahamu kama unatumia njia hiyo.
  • ukitoa kijiti tu unaweza kubeba mimba kwa mda mfupi..

Madhara madogo madogo ya njia hiyo ya uzazi wa mpango.
  • ·         Kubadilika kwa mfumo wa kutoka damu mwisho wa mwezi kama kutoka damu nyingi sana, matone ya damu au kukata kabisa kwa damu.
  • ·         Maumivu ya tumbo na kichwa..
  • ·         Maumivu ya matiti,
  • ·         Kuongezeka uzito.
  • ·         Kuongezeka au kuisha kabisa kabisa kwa chunusi.
Mwisho: hii ni moja ya njia bora zaidi za uzazi wa mpango kwasababu haina usumbufu kabisa mpaka miaka mitatu au mitano iishe lakini unaruhusiwa kuondoa kama ukihitaji mototo kabla mda uliopangwa haujaisha.
Ukipata matatizo yeyote makubwa muone daktari haraka..

                      STAY ALIVE