Upofu ni nini?
Kulingana na shirika la afya duniani{WHO}, upofu ni hali ya
kushindwa kuhesabu vidole vilivyoko kwenye umbali wa chini ya mita tatu..
Hali ya upofu Tanzania na duniani kwa ujumla.
·
Zaidi ya watu milioni hamsini duniani ni vipofu
na million mia moja thelathini na tano wana matatizo ya kutoona vizuri.
·
Kila mwaka watu milioni mbili duniani wanakua
vipofu.
·
80% ya upofu unaotokea unazuilika.
·
Nchini Tanzania watu laki nne ni vipofu na
wengine milioni moja na laki mbili wana matatizo ya kutoona vizuri.
·
Data hizi ni kulingana na shirika la afya
duniani.{WHO}
Sababu kubwa za upofu ni zipi?
Cataract {mtoto wa jicho}:
hili ni wingu jeupe ambalo linatokea kwenye lenzi ya jicho,
kisha jicho hushindwa kupitisha mwanga na upofu hutokea.
Cataract husababishwa na magonjwa kama kisukari, umri mkubwa,
kuumia kwa jicho.
Ugonjwa huu huweza kutibika kwa kubadilisha lenzi ya jicho.
Cornear scar {kovu la cornea}:
Hili ni kovu linalotokea kwenye utando mdogo wa juu wa jicho
ambao hupitisha mwanga kumfanya mtu aone. kitaalamu unaitwa cornea.
Sababu kubwa ni kuumia
kwa cornea nchini kwetu ni ugonjwa wa trachoma.
Glaucoma:
Hii ni hali ambayo kuna ongezeko la presha ndani ya jicho
kuliko ile presha inayohitajika, hii husababisha kuharibika kwa neva inayoitwa
kitaalamu kama optic nerve ambayo inahusika na kuona. Jicho la kawaida lina
pressure 12-22mmhg.
Magonjwa mengine yanayoleta upofu ni presha ya damu,
kisukari na ukimwi I.e cytomegalovirus retinitis.
hizi ndio njia rahisi ya kuzuia upofu.
- · Fanya uchunguzi mara kwa mara wa afya yako ili kutambua kama una magonjwa yanayosababisha upofu, na kama ushaugua magonjwa hayo njia nzuri ya kuzuia upofu ni kuhakikisha unafuata ushauri wa kitaalamu jinsi ya kuishi na magonjwa hayo na kufuata matibabu kama inavyotakiwa.
- · Usifanye kazi sehemu yenye mwanga mdogo hii itasababisha macho yako kutumia nguvu nyingi sana kuona.
- · Usisome kitu chochote wakati unatembea.
- · Usiangalie moja kwa moja mwanga mkali kama jua au moto wa kuchomelea.
- · Kama unafanya kazi kwenye kifaa kinachotoa mwanga kaa umbali wa sentimita 25 mpaka 30.
- · Tumia miwani ya jua ukiwa unaendesha pikipiki, baiskeli au gari iliyofunguliwa madirisha kuepusha vumbi na wadudu machoni.
- · Usichangie taulo ya kuogea, ugonjwa wa macho unaweza kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
- · Kama macho yako yamefanya kazi mda mrefu. yapumzishe kwa kuangalia umbali mrefu na kuyageuza huku na kule, weka kitambaa chenye maji ya uvuguvugu machoni ili kuongeza mzunguko wa damu machoni,
- ·
Nenda kwenye uchunguzi wa macho angalau mara
mbili kwa mwaka baada ya kufikisha miaka arobaini. soma hapa kwa maelezo zaidi.t
STAY ALIVE…..
0653095635/0769846183
0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni