data:post.body SABABU HIZI ZINAWEZA KUKUFANYA USIONE SIKU ZAKO ZA MWEZI KABISA.{AMINORRHEA] ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

SABABU HIZI ZINAWEZA KUKUFANYA USIONE SIKU ZAKO ZA MWEZI KABISA.{AMINORRHEA]
Amenorrhea ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke aliyepevuka na kukomaa maumbile yake ya uzazi kushindwa kuziona siku zake.
Mwanamke anatakiwa aanze kuziona siku zake kati ya miaka 12 mpaka 14.

Hali hii ya kutoona siku huweza kutokea kwa mwanamke ambaye hajawahi kuziona siku zake lakini ameshatimiza vigezo[pimary aminnorhoea] AU kwa mwanamke ambaye ameshawahi kuziona siku zake lakini zimesimama.{secondary amenorrhea}

Kwa mwanamke ambaye ameshawahi kuziona siku zake akikaa miezi mitatu bila kuziona siku zake hiyo ndio itaitwa secondary amenorrhea.

Na mwanamke ambaye hajawahi kuziona siku zake akafikisha miaka 16 bila kuziona hiyo ndio primary amenorrhea.
Tatizo hili linaweza kuzua hofu ya kisaikolojia kwa mwanamke aliyelipata.

 Chanzo ni nini?
 • ·         Kuchelewa kukomaa kwa viungo vya uzazi mfano kizazi, uke na ovari.
 • ·         Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa chakula. i.e tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika hali nzuri maarufu kama leptin kua katika kiwango cha chini sana.
 • ·         Matumizi ya dawa:
 • Dawa zinazotumika kwenye uzazi wa mpango zimeonyesha kusababisha halii hii hasa zile zenye homoni nyingi ya progesterone i.e depo provera
 • ·         Kunyonyesha:Miezi sita ya kwanza ya kunyonyesha mtoto kiwango cha hormone inayohusika kutoa maziwa yaani prolactin hua kwa kiwango cha juu sana na homoni zinazohusika na siku za mwanamke yaani oestrogen na progesterone hua ziko chini sana.
 • ·         Ujauzito:Hii iko wazi kwamba ukishapata mimba ile shughuli ya kusababisha mwanamke kupata siku zake husimama.
 • ·         Magonjwa;Baadhi ya magonjwa ya viungo vya uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kuonekana kwa siku za mwanamke mfano polycystic ovarian syndrome.
 • ·          mgandamizo wa mawazo na kubadilisha mazingira ya kuishi. 

 •       menopause: hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 45 mpaka 60. homoni zinazohusika na na kupata siku za mwanamke hua kwenye kiwango cha chini sana kiasi kwamba haziwezi kufanya kazi yake sawasawa. i.e progesterone na oestrogen                                                                                                                                                       
      
MATIBABABU;
 • Kujua chanzo cha hali hii na kukitatua ndio mzizi mkuu wa kuweza kutibu tatizo hili.
Matibabu mengine ni:
 • ·         Kufanya masaji kwenye tumbo la chini kwa kutumia maji ya uvuguvugu ili kuongeza damu nyingi kupita huko.
 • ·         Kula chakula kisichotokana na damu{vegetarian diet} chenye protini nyingi. Mfano karanga, nazi, maharage na korosho.
 • ·         dawa zenye hormone kadhaa  huweza kutatua tatizo hili kwa wanawake wenye kiwango kidogo au kikubwa sana cha hormone flani.{hormonal imbalance} mfano  microgynon na microlut.soma bonyeza maneno ya ya kijani kwa maelezo zaidi

SECRETS OF GOOD HEALTH


                                                                                                                                                                                             STAY ALIVE
                            DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO 
                             MAWASILIANO 0653095635/0769846183
0 maoni:

Chapisha Maoni