.
Kama kawaida ndugu msomaji leo tunaendelea na makala za
kusisimua na kuelimisha jamii kwenye blog hii, na leo katika SIRI ZA AFYA BORA
kutakua na muendelezo wa makala za uzazi wa mpango kwani ni ndefu na zinahitaji
umakini mkubwa. Hivyo nakushauri kama unataka kua mtaalamu wa uzazi wa mpango
kufuatilia kwa kina sana mfululizo huu.
Uzazi wa mpango ni
nini?
Kiufupi hizi ni njia zinazotumika kitaalamu kuzuia mimba
ambazo hazikupangwa.
Njia hizo ni nyingi, lakini tutajitahidi kuongelea njia moja moja ya uzazi wa mpango kwa kila makala,
na leo tutazungumzia njia ya uzazi wa mpango ya sindano kitaalamu kama depo provera.
Hii ni njia ya uzazi wa mpango ambayo dawa hii ya depo provera ambayo ni homoni
ya progesterone sawa na inayopatikana kwenye mwili wa mwanamke hutumika kupanga uzazi..
Dawa hii ya sindano huchomwa kila baada ya miezi mitatu
kwenye misuli .{mara nyingi huchomwa kwenye mkono kama sindano ya tetenasi}
Jinsi inavyofanya
kazi..
Dawa hii huzuia yai la mwanamke kutoka kwenye ovary{kiwanda
cha mbegu za mwanamke} kwenda kwenye mfuko wa uzazi.
Pia huzuia mbegu za kiume kupita kwenye shingo la mfuko wa
uzazi{cervix} kwenda kizazi.{uterus}.
Uwezekano wa kuzuia mimba ni zaidi ya asilimia tisini na
tisa na hatari ya kupata mimba huongezeka pale mtu anapokosa sindano kwa mda
kama ilivyopangwa.
Lini mtu anatakiwa
aanze kutumia njia hii?
Mtu anaweza kuanza kutumia njia hii mda wowote ila tu asiwe
mjamzito na hua ni vizuri kuanza kipindi wakati mwanamke anaona siku zake za
mwezi na hupimwa kipimo cha ujauzito kabisa kabla ya kuanza wakati mwingine..
Wanawake wanaoruhusiwa
kutumia njia hii..
- · Mwenye watoto au ambaye hana mtoto.
- · Anayenyonyesha au asiyenyonyesha.
- · Anayevuta sigara au kunywa pombe..
- · Umri wowote baada ya kubalehe.
- · Baada ya mimba kutoka au kutoa mimba.
- · Mwenye virusi vya ukimwi au presha na wengine wengi.
Madhara ya sindano
hii ya kupanga uzazi…
- · Kubadilika kwa mfumo wa kuona siku za mwezi yaani kupata damu nyingi, iliyoganda, na zaidi ya asilimia themanini hawaoni siku zao kabisa.
- · Kuongezeka uzito yaani kilo moja mpaka mbili kwa mwaka.
- · Kichwa kuuma.
- · Mgandamizo wa mawazo.
- · Mtu akiacha kutumia njia hii hawezi kupata mimba hapohapo, wakati mwingine mpaka miezi sita au mwaka.
Vitu ambavyo sio vya
kweli vinavyosema mtaani kuhusu njia hii.
- · Humfanya mtu kua tasa.
- · Damu hujaa tumboni mwa mwanamke.
- · Huharibu mimba iliyotungwa…
Mwisho: hii ni
moja ya njia nzuri za uzazi wa mpango kwani huchomwa kila baada ya miezi
mitatu, sio rahisi kusahau sindano na uwezekano wa kubeba ujauzito ni mdogo
sana.
Endelea kufuatilia makala hizi kwa njia nyingine zaidi za
uzazi wa mpango. kwa maelezo zaidi soma hapa.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga
STAY ALIVE
0653095635/0769846183
s
s
0 maoni:
Chapisha Maoni