
Unyonyeshaji sahihi ni upi?
Huu ni onyonyeshaji wa mtoto ambao humfanya aridhike na
maziwa aliyokunywa , awe na afya bora na ukuaji unaoendana na umri. Yaan ukuaji
na ukomavu wa ubongo na mwili wote kwa ujumla.
Wanawake wengi hua wananyonyesha tu, lakini tafiti
zinaonyesha watoto wengi wahanyonyeshwi kama inavyotakiwa.
Kawaida mtoto anatakiwa anyonyeshwe mda mfupi baada ya
kuzaliwa maziwa ya mama tu bila kuchanganya kitu chochote kwa miezi sita kisha
huweza kumuanzishia chakula laini kama uji huku akiendelea na maziwa ya mama
angalau kwa miaka miwili.
Njia sahihi ya kunyonyesha ni ipi?
- · Titi linatakiwa liguse kidevu cha mtoto.
- · Mdomo ufunguke wote vizuri.
- · Lip ya chini iwe imefunguka kwenda nje.
- · Chuchu ionekane zaidi juu ya mdomo kuliko chini ya mdomo.
Utajuaje kama mtoto ameridhika baada ya kunyonya?
- · Mtoto ataacha kunyonya mwenyewe.
- · Mtoto anapoteza hamu ya kunyonya na kuonekana kama ana usingizi.
Dalili za kuonyesha mtoto ananyonya vizuri.
- · Ananyonya taratibu na kupumzika.
- · Utamuona mtoto anameza maziwa.
dalili kwamba mtoto hanyonyi vizuri ni zipi?
- anannyonya haraka haraka na kuzamisha mashavu kwa ndani kama anapiga mluzi.
- · Hautaona kama anameza maziwa.
- · Mwisho wa kunyonya mtoto haridhiki na kuanza kulia au kunyonya kwa mda mrefu.
0 maoni:
Chapisha Maoni