data:post.body HII NDIO SULUHISHO YA MAUMIVU KIPINDI CHA HEDHI.{DYSMENORRHEA} ~ SIRI ZA AFYA BORA...

Recent Posts

HII NDIO SULUHISHO YA MAUMIVU KIPINDI CHA HEDHI.{DYSMENORRHEA}Dysminorrhea ni nini?
Haya mi maumivu makali anayoyapata mwanamke siku chache  kabla ya kuingia na kipindi ambacho yupo kwenye siku zake.

Kuna aina kuu mbili za maumivu hayo kutokana na chanzo chake.
Primary dysmenorhea…
Haya ni maumivu ambayo hayana sababu maalumu lakini wataalamu wanadhani yanasababishwa na homoni inayoitwa kitaalamu kama prostaglandins kutoka kutoka kwenye mfuko wa uzazi.{endometrium}
Secondary dysminorrhea..
Hii ni aina  ya maumivu ambayo hutokea kutokana na ugonjwa flani hasa unaoathiri umfuko wa uzazi mfano pelvic inflammatory diseases, underdeveloped genital organs, cervical stenosis, asherman syndrome.

Vipimo vinavyofanyika hospitali.
Utrasound scan:
Hichi ni kipimo cha ambacho hupiga picha kuangalia mfuko wa uzazi kama una tatizo lolote ambalo linalohusiana na maumivu hayo.
Mgonjwa hutakiwa kunywa maji mengi kujaza kibofu cha mkojo kabla ya picha hiyo.
                                                 

Matibabu:
  •    Kutibu ugonjwa unaosababisha maumivu hayo ni njia nzuri zaidi.{secondary dysminorrhea}
  • Matibabu huweza kua antibayotiki kulingana na ugonjwa husika  hadi upasuaji wakati mwingine.
Matibabu kwa maumivu ambayo hayasababishwi na ugonjwa wowote.{primary dysiminorrhea}
 ·         Fanya massage kwa nusu saa kila siku{kipindi cha maumivu}  kwenye tumbo la chini ili kuongeza mzunguko wa damu.{dry massage}
                                        

·         Tumbukia kwenye sinki la maji ya moto kwa nusu saa au saa moja kipindi cha maumivu au weka maji ya moto kwenye mpira maalumu kisha weka juu ya tumbo.
                                                       

·         Funga tumbo na kitambaa cha kawaida au mkanda maalumu.
                                                 

·         Tumia dawa za maumivu kama diclopa, ibuprofen, meloxicam pale maumivu yanapokua makali sana.
        Kikundi cha dawa za anticholinergic mafano colirem na hyoscine butylbromide pia ina msaada sana katika shida hii.
Onyo: dawa zote unazozifahamu zina madhara kwa matumizi ya kibanadamu hivyo usitumie dawa yeyote bila maelekezo ya kitaalamu.

Mwisho nakupa pole wewe unayesumbuka na shida hii, ila ukifuata maelekezo hayo hapo juu vizuri, utaishi kwa furaha kuliko mwanzoni..
kwa maelezo zaidi soma hapa

SECRETS OF GOOD HEALTH


                             DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO..      
                              
                                        0769846183\ 0653095635.

                                                    STAY ALIVE…0 maoni:

Chapisha Maoni