data:post.body Septemba 2014 ~ SIRI ZA AFYA BORA...
  • Karibu kwenye blog ya SIRI ZA AFYA BORA ujifunze mbinu bora za afya ili uweze kuwa na afya bora.

Recent Posts

KABLA HUJAANZA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO HEBU SOMA MTIRIRIKO WA HIZI MAKALA..{FAMILY PLANNING}


.                                                                     

Kama kawaida ndugu msomaji leo tunaendelea na makala za kusisimua na kuelimisha jamii kwenye blog hii, na leo katika SIRI ZA AFYA BORA kutakua na muendelezo wa makala za uzazi wa mpango kwani ni ndefu na zinahitaji umakini mkubwa. Hivyo nakushauri kama unataka kua mtaalamu wa uzazi wa mpango kufuatilia kwa kina sana mfululizo huu.

Uzazi wa mpango ni nini?
Kiufupi hizi ni njia zinazotumika kitaalamu kuzuia mimba ambazo hazikupangwa.
Njia hizo ni nyingi, lakini tutajitahidi kuongelea  njia moja moja ya uzazi wa mpango kwa kila makala, na leo tutazungumzia njia ya uzazi wa mpango  ya sindano kitaalamu kama depo provera.
Hii ni njia ya uzazi wa mpango ambayo dawa hii ya depo provera ambayo ni homoni ya progesterone sawa na inayopatikana kwenye mwili wa mwanamke hutumika kupanga uzazi..
Dawa hii ya sindano huchomwa kila baada ya miezi mitatu kwenye misuli .{mara nyingi huchomwa kwenye mkono kama sindano ya tetenasi}

Jinsi inavyofanya kazi..
Dawa hii huzuia yai la mwanamke kutoka kwenye ovary{kiwanda cha mbegu za mwanamke} kwenda kwenye mfuko wa uzazi.
Pia huzuia mbegu za kiume kupita kwenye shingo la mfuko wa uzazi{cervix}  kwenda kizazi.{uterus}.
Uwezekano wa kuzuia mimba ni zaidi ya asilimia tisini na tisa na hatari ya kupata mimba huongezeka pale mtu anapokosa sindano kwa mda kama ilivyopangwa.

Lini mtu anatakiwa aanze kutumia njia hii?
Mtu anaweza kuanza kutumia njia hii mda wowote ila tu asiwe mjamzito na hua ni vizuri kuanza kipindi wakati mwanamke anaona siku zake za mwezi na hupimwa kipimo cha ujauzito kabisa kabla ya kuanza wakati mwingine..

Wanawake wanaoruhusiwa kutumia njia hii..
  • ·         Mwenye watoto au ambaye hana mtoto.
  • ·         Anayenyonyesha au asiyenyonyesha.
  • ·         Anayevuta sigara au kunywa pombe..
  • ·         Umri wowote baada ya kubalehe.
  • ·         Baada ya mimba kutoka au kutoa mimba.
  • ·         Mwenye virusi vya ukimwi  au presha na wengine wengi.


Madhara ya sindano hii ya kupanga uzazi…
  • ·         Kubadilika kwa mfumo wa kuona siku za mwezi yaani kupata damu nyingi, iliyoganda, na zaidi ya asilimia themanini hawaoni siku zao kabisa.
  • ·         Kuongezeka uzito yaani kilo moja mpaka mbili kwa mwaka.
  • ·         Kichwa kuuma.
  • ·         Mgandamizo wa mawazo.
  • ·         Mtu akiacha kutumia njia hii hawezi kupata mimba hapohapo, wakati mwingine mpaka miezi sita au mwaka.


Vitu ambavyo sio vya kweli vinavyosema mtaani kuhusu njia hii.
  • ·         Humfanya mtu kua tasa.
  • ·         Damu hujaa tumboni mwa mwanamke.
  • ·         Huharibu mimba iliyotungwa…

Mwisho: hii ni moja ya njia nzuri za uzazi wa mpango kwani huchomwa kila baada ya miezi mitatu, sio rahisi kusahau sindano na uwezekano wa kubeba ujauzito ni mdogo sana.
Endelea kufuatilia makala hizi kwa njia nyingine zaidi za uzazi wa mpango. kwa maelezo zaidi soma hapa.tembelea blog yetu ya kingereza hapa www.vibesinc.ga

                                         STAY ALIVE

                               0653095635/0769846183
s

HII NDILO SULUHISHO PEKEE LA KUNUKA MDOMO { BAD BREATH}


                                
                
Watu wengi hawawezi kujua harufu zao za mdomo. lakini harufu za midomo yao ziko wazi kwa watu wengine wanaowazunguka..
Sio rahisi muhusika kufahamu kama ana tatizo hili mpaka aambiwe na wanao mzunguka.
Mtu akishafahamu ana tatizo hili hupata hofu sana na huathirika sana kisaikolojia kwa kuwaza kwamba jamii inamchukuliaje..

Sababu zifuatazo zinaweza kumfanya mtu awe na harufu kali ya mdomo..
  • ·         Vyakula na vinywaji:
Pombe na  vileo vingine huacha mabaki mdomoni ambayo huleta harufu kali ya mdomoni pia vyakula vyenye wingi mkubwa wa madini ya sulphur kama nyama, samaki vinapomeng’enywa sulphur hyo husafiri kwenye damu mpaka kwenye mapafu na kutoa harufu ambayo si ya kawaida. Harufu hiyo huweza kudumu kwa masaa 12 mpaka 24.

  • ·         Kitu chochote kinachokausha mate mdomoni:
Mzunguko wa mate mdomoni huzuia bacteria wa mdomoni kukua .
Mdomo unapokauka mfano wakati wa kulala bacteria hao huazaliana haraka kula mabaki mdomoni na na kuacha harufu kali inayopatikana wakati wa kuamka.{morning breath}
Dawa pia zinazokausha mate mdomoni kama furasamide, amitripline na piriton huweza kuleta hali hiyo.
Pia mtu anavyozidi kua mkubwa kiumri uzalishaji wa matemdomoni  unapungua na ii ndo sababu watu wengi wazee wananuka midomo.

  • ·         Magonjwa:
Magonjwa kama kisukari, kifua kikuu,baadhi ya kansa, na magonjwa ya ini huleta harufu kali ya mdomoni.

  • ·         Uvutaji wa sigara na kutopiga mswaki:
Kawaida mtu anatakiwa apige mswaki kila anapomaliza kula yaani kama asubuhi mtu anatakiwa anywe chai kwanza ndio apige mswaki na milo mingine ivoivo.
Pia sigara huacha mabaki yanayofanya mdomo ue na harufu mbaya.


VIPIMO VINAVYOFANYIKA HOSPITALI:
Historia ya mgonjwa inaweza  ikamfanya daktari akatambua chanzo cha harufu ya mgonjwa kama nilivyotaja hapo juu.
Pia kuna baadhi ya vipimo huweza kupimwa kugundua magonjwa flani. Mfano
  • ·         Kupima kikohozi kuangalia wadudu wa kifua kikuu.
  • ·         Kupima damu kama mgonjwa ana kisukari.
  • ·         Uwezo wa figo na maini.{liver and kidney function test}

Wakati mwingine vipimo vinaweza kushindwa kugundua chanzo cha ugonjwa husika.


MATIBABU:

Daktari akishafahamu chanzo cha ugonjwa ni rahisi kuutibu kirahisi.
Mgonjwa anaweza kusafishwa kinywa na daktari wa meno na kuanzishiwa matibabu mengine kulingana na ugonjwa husika.{scaling}

Matibabu mengine:
·          Usafi wa kinywa ni muhimu kwa ajili ya afya ya meno na kinywa kwa ujumla, ni vizuri kupiga mswaki kila baada ya mlo na kumuona daktari wa meno kila baada ya miezi sita.
Kama huwez kupiga mswaki kama hivyo ni bora ata kuosha mdomo tu na maji baada ya kula.

·         Ulimi unaweza kusababisha harufu kali mdomoni, hivyo usiusahau wakati wa kupiga mswaki.

·         Tumia viosha mdomo mara chache kuua bacteria hatari mdomoni.{ mouth washes}

·         Kunywa maji mengi kama glasi nane kwa siku, juice au tafuna jojo kuongeza mzunguko wa mate mdomoni.

                      Nakutakia afya njema wewe na familia yako..
bofya hapa kusoma zaidi

SECRETS OF GOOD HEALTH

                            
                                           STAY ALIVE…
                                 0653095635/0769846183

KUPASUKA KWA KONDOM WAKATI WA TENDO LA NDOA KUNASABABISHWA NA HAYA MAKOSA SITA.


                                                          
habari za asubuhi wadau, matumaini yangu mko vizuri na shughuli zenu..Kama tulivyosoma kwenye makala iliyopita kuhusu imani potofu zilizopo kuhusu condom,  leo somo hilo litaendelea baada ya wadau wengi kunipigia nakuuliza maswali mengi hasa kwanini condomu hua zinapasuka ovyo wakati wa tendo la ndoa,  na bila kufanya kosa nikawaandalia majibu yao kama ifuatavyo…

  • ·         Usiifungue condom yote afu ndio uivae kwani hutaweza kuivaa kirahisi na hata ukiivaa itaingiza hewa ambayo utaifanya ipasuke ndani ya mda mfupi.

  •      Usitumie mafuta yeyote ya kuongezea kwenye condom kwani utaharibu material yake ya latex na kuipasua kirahisi.

  • ·         Usitumie condom iliyobadilika rangi kwani ni dalili kwamba imeharibika au kuisha mda wake na huweza kupasuka katikati ya tendo la ndoa.

  • ·         Usitumie condom inayoonekana kukakamaa au kua kavu sana kwani inaweza ikapasuka kirahisi kwa kukosa mafuta.

  • ·         Usitumie condom mara mbili kwani inakua imeshapoteza uwezo wake wa mwanzo wa kimatumizi.

  • ·         Usianze tendo la ngono kabla mwanamke hajawa tayari kuingiliwa kwani ukavu uliokuepo huko ndani ya uke huweza kuifanya ipasuke.

  mawasiliano 0653095635/0769846183

                                             STAY ALIVE
                                           

HIVI NDIO VITU SABA VYA UONGO AMBAVYO WATU WANAVIFAHAMU KUHUSU KONDOMU.


Condom ni nini?
Huu ni mpira uliotetengenezwa kitaalamu na raba inayoitwa latex mara nyingi..
Hutumika katika tendo la ndoa kuzuia magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi pia kuzuia mimba ambazo hazikupangwa.
Kuna condom za kike na za kiume japokua matumizi ya kondom za kike hua ni adimu sana.
Ikitumika vizuri condom huweza kuzuia kwa  zaidi ya 95% ya maambukizi ya ukimwi ambayo yangeweza kuambukizwa bila kutumia condom.
Lakini kwa sababu watu wengi hawapendi kutumia kondom wametunga uongo mwingi kushawishi wengine wasitumie, na ufuatao ndio uongo huo.

1.       Condom inapunguza raha ya tendo la ndoa:
Ukweli ni kwamba kondom husaidia sana wanaume ambao wana tatizo la kufika kileleni kabla wenzi wao hawajaridhika hivyo hufanya tendo hilo kua la raha kwa wote.

2.       Condom imewekewa virusi vya ukimwi ndani
Ukweli ni kwamba kondom haina virusi hivyo na hata kama vingekuepo visingeweza kuishi ndani ya condom kwasababu kondom haina chakula cha kulisha virusi na haiwezekani virusi kuishi kwenye mazingira yale, lakini pia condom kazi yake ni kuzuia virusi hivyo.

3.       Condom huweza kupotea ndani ya mwili wa mwanamke:
Kitu kama hicho hakipo na hata ikitokea ikabaki bahati mbaya  ndani ya uke inaweza kutolewa na kidole kimoja tu kirahisi.

4.       Condom ni ndogo sana na haiwatoshi wanaume:
Ukweli ni kwamba condom inaweza kuvalishwa kwenye kichwa cha mtu mzima bila kupasuka ata kidogo.

5.       Condom hupasuka sana:
Condom hufanyiwa vipimo na shirika la viwango TBS kabla ya kuingizwa sokoni, hivyo ikitumika kwa kufuata maelekezo haiwezi kupasuka.

6.       Condom ina matundu kuruhusu virusi vya ukimwi:
Kama nilivyosema mwanzo condom zinafanyiwa vipimo maalumu kabla hazijasambazwa na haziwezi kua na matundu hayo,

7.       Condom inawasha na kuchubua sehemu za siri:
Ni watu wachache sana wana shida hii na kama wewe ni mmoja wao unaweza ukamuona daktari akakupa ushauri au ukatumia aina nyingine ya kondomu yenye material tofauti.



MWISHO;  utumiaji wa kondomu ni bora kwa afya yako ya leo na baadae…wewe kijana au mzee unayesoma hapa nakushauri utumie kinga hiyo kila unapokutana kingono ili uitunze afya yako na kupanga uzazi kirahisi kwani taifa linakutegemea sana...kwa maelezo zaidi bonyeza maneno haya ya kijani kusoma

SECRETS OF GOOD HEALTH


  
                                     STAY ALIVE
                          065`3095635/0769846183