kifo ni nini?
hii ni hali ya kusimama kwa mifumo yote ya mwili na kushindwa kufanya kazi. mfano: mfumo wa upumuaji, mfumo wa fahamu, mapigo ya moyo, mmeng"enyo wa chakula na kadhalika..
pia ni hali ambayo kwa miaka yote imekua ikitokea kwa binadamu lakini bado ni ngumu sana kuizoea na tunatakiwa tufahamu siku moja wote hali hiyo itatupata.
zifuatazo ni dalili 6 muhimu za kifo
.
- rigor mortis{kukakamaa kwa misuli}: misuli midogo mfano ya kwenye joint za mikono huanza kukamaa kwanza kisha misuli mikubwa kama ya miguuni hufuata sababu ya kutokuepo kwa nguvu ya ATP ambayo inahusika na kuzuia hali hiyo.
2.decapitation{kukatika kwa kichwa}: kukatika kwa kichwa hasa mtu anapopata ajali ni dalili ya moja kwa moja ya kifo. viungo kama kidole, uume, na mikono huweza kurudishwa iwapo vikikatika na vikafanya kazi.

3.decomposition{kuoza}: masaa machache baada ya kifo mwili huanza kutoa enzymes ambazo huanza kutafuna mwili na viungo vya ndani kama utumbo, mapafu na maini zikisaidiana na bacteria. hali ya kuoza inategemea hali ya hewa na chanzo cha kifo husika.
4.incinaration{kuungua}: kuungua kabisa kwa mwili na kushindwa kuutambua mwili husika ni dalili muhimu ya kifo ambayo hua haina maswali.
5. removal of vital organ{kunyofoka kwa viungo muhimu vya mwili}: viungo kama moyo, mapafu, Figo na maini vikinyofoka labda kutokana na ajali fulani hauhitaji kuanza kuhangaika na huduma ya kwanza sababu hicho ni kifo tayari.

6.dependant lividity: huku ni kutuama kwa damu sehemu moja ya mwili baada ya moyo kushindwa kufanya kazi, ambapo kutuama huko hutegemea sana mtu huyo ailikutwa na mauti akiwa amekaa vipi. kutuama huko kwa damu hutegemea mteremko{gravity} wa mfu husika.
kwa maelezo zaidi bofya maneno ya kijani hapa kusoma
SECRETS OF GOOD HEALTH
STAY ALIVE......DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
0 maoni:
Chapisha Maoni