chunusi ni nini?
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi, hali hii husababishwa na kutengenezwa kwa mafuta mengi chini ya ngozi kuliko kawaida na kuziba kwa vinyweleo vya ngozi.
chanzo ni nini?
- hii husababishwa na kuongezeka hormone za uzazi aina ya testosterone kwa jinsia zote hasa hasa kipindi cha kubalehe na kuvunja ungo kwa jinsia zote lakini genetics au kuzaliwa katika ukoo fulani kumegunduliwa kuchangia kupata chunusi kwa zaidi ya 80% ya wahanga. ugonjwa wa chunusi ni tatizo kubwa sana kwa vijana, huweza kusababisha msongo wa mawazo na hata kujiua. mwaka 2015 tafiti zilionyesha kwamba watu milioni 633 duniani wanasumbuliwa na kuweka ugonjwa huu wa 8 kati ya magonjwa kumi duniani yanayopatikana kwa watu wengi.
- kurithi; baadhi ya koo zimeonekana kua na chunusi nyingi zaidi kuliko koo zingine, hii imeonyesha kwamba ugonjwa huu unafuata ukoo.
- kushambuliwa na bacteria; bacteria wa propionibacterium acne wameonyesha kusababisha chunusi kwa kuingilia mfumo wa ngozi kuhifadhi mafuta.
- chakula; ulaji wa chakula chenye sukari nyingi kama soda,biskuti,pipi,chocolate na kadhalika, ulaji wa chumvi nyingi na matumizi ya vyakula vyenye viungo sana na pilipili huleta chunusi.
- msongo wa mawazo; kama tulivyosema mwanzo kwamba kuna mahusiano makubwa kati ya chunusi na kiwango cha homoni mwilini, msongo wa mawazo husababisha kuharibika kwa mfumo wa homoni mwilini na kuleta chunusi.
- mazingira; kuziba ngozi kwa kuvaa helemeti au kofia huweza kusababisha chunusi kwa kuzuia mafuta kutoaka ndani ya ngozi
- dawa; baadhi ya dawa huongeza sana chunusi zilizopo na kua nyingi zaidi mfano predinisolone, dexamethasone, hydrocortisone, isoniazid,
matibabu.
matibabu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo....matibababu kwa chakula, matibabu ya kimwili na matibabu ya dawa za hospitali.
matibabu ya chakula..
- ondoa chumvi kwenye chakula chako au kula chumvi kidogo sana.
- epuka ulaji wa sukari na vyakula vyote vya kukaanga kama chips, maandazi na chapati.
- epuka nyama za wanyama wote unazozifahamu, viungo vya bonga i.e pilipili, na stimulants ie kahawa.nb: unaweza kula samaki kama huwezi kuvumilia bila kula nyama.
- pendelea kula vyakula vya asili kama wali, ugali, mchicha, maharage, njegere vikiwa vimeungwa mafuta kidogo sana pia kula kwa wingi karoti mbichi kwasababu zina vitamin A ambayo ni nzuri sana kwa ngozi
- kunywa maji mengi ili kuondoa sumu zote mwilini na kulainisha ngozi.
matibabu yasiyo ya dawa.
- acha ngozi yako ipate jua la asubuhi na jioni kila siku.
- weka sura yako kwenye mvuke wa maji ya moto kila siku.
- shiriki mazoezi ya aina yeyote hata kama ni kuruka kamba tu angalau utokwe jashoo kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.
antibotics; hizi ni dawa ambazo hutumika hasa kuwaua bacteria wanaosababisha chunusi, ni nzuri lakini zisitumike zaidi ya miezi mitatu kwani zinaweza kuleta madhara mengine mfano erythromycin,doxycline,minocyline na tetracycline.
dawa za homoni; kwa wanawake dawa zinazotumika kwenye uzazi wa mpango zile zenye mchanganyiko wa oestrogen na progesterone huweza kuwasaidia kupunguza kiasi cha homoni za adrogens mwilini, dawa spreronalactone pia hutumika kutibu chunusi lakini dawa hizo zisitumike kipindi cha ujauzito au konyonyesha kwani zina madhara kwa watoto.
retinoids; hizi huondoa na kuzuia kukusanyika kwa seli zilizokufa na kuziba vinyweleo vya ngozi, ni moja ya dawa ambazo wagonjwa wa chunusi hushauliwa kuanza nazo kabla ya kutumia dawa zingine mfano wa dawa hizi ni tazarotone,retinol,adapalene na isotretinon. dawa hizi zina kiasi kikubwa sana cha vitamin a ambazo ni nzuri kwa ngozi.
dawa zingine; dawa zingine zinazotumika na benzy peroxide, salicyclic acid,azelaic acid,
mchanganyiko wa dawa; utafiti umeonyesha kwamba matumizi ya dawa moja hua hayana matokeo mazuri kama mtu akichanganya dawa, mfano;
benzy peroxide na antibiotics zimeonyesha matokeo mazuri
matumizi ya retinoid na antibiotic hua na matokeo mazuri
benzy peroxide na retinoid pia zimeonyesha matokeo mazuri
mwisho:
mara nyingi chunusi huisha watu wakifikisha umri wa miaka 20 na kwenda mbele japokua huweza kuendelea kwa baadhi ya watu hivyo kama unaona huwezi gharama za dawa ziache tu zitaisha zenyewe, mimi binafsi niliwahi kusumbuliwa sana na chunusi nilipokua umri wa kubalehe lakini baadae ziliisha zenyewe...watu wengi hawaponi chunusi kwasababu ya kupenda kutumia njia moja tu ya matibabu {dawa},bila kuchanganya na njia zingine za kiafya kama nilivyotaja hapo juu lakini pia wengine hukosa uvumilivu na kujikuta wanatumia dawa muda mfupi na kuacha bila kuipa muda..mara nyingi chunusi hua zinakuja kwa chanzo fulani na kwakua huku kwetu sio rahisi kujua chanzo ni nini basi mgonjwa hulazimika kujaribu dawa mbalimbali kabala hajapata inayomfaa yeye.
MAWASILIANO 0653095635/0769846183
DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO
Doctor Mimi Nina chunusi nyingi sana Ila ngoja niache zitatoka zenyewe tu
JibuFuta